Pre GE2025 Mbeya yaanza mchakato wa kuligawa jimbo la Mbeya Mjini alipo Tulia Ackson na kupata jimbo lingine la Uyole

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Wameona wamtengee kabisa Tulia jimbo asipate tabu ya kusumbuana na Sugu, maana wanajua ataibika!

====


Halmashauri ya Jiji la Mbeya imependekeza kuanza mchakato wa kuchunguza na kuligawa Jimbo la Mbeya Mjini kupata jimbo jipya la Uyole, katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2025.

Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Dk Tulia Ackson ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU).

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mchakato huo ukikamilika na kukidhi vigezo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) italitangaza jimbo jipya, jambo ambalo litakuwa jawabu la matakwa ya wakazi wa Mbeya Mjini.

Akizungumza niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa jiji hilo, John Nchimbi leo Machi 11, 2025 katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani, Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala jijini humo, Nicodemus Tindwa amesema hatua hiyo ni baada ya kupokea barua kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

Mwananchi
 
Sugu ½ Tulia½
Kazi na utu, tunasonga mbele
 
Niliona hilo suala mapema sana.


Chagua kwa uangalifu 2025
 
Bora Waongeze na jimbo lingine MBALIZI 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…