MLEMVYA RASHID
Member
- Aug 1, 2013
- 89
- 11
MBINU 10 ZA KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU TANZANIA(MAKALA,,,MWANANCHI)
Makala haya yanaangazia baadhi ya mikakati inayoweza kunusuru elimu ya watoto wetu, ili hatimaye waweze kupata stadi na ujuzi wa siyo tuu kushindana na wenzao katika soko, lakini waweze kukabiliana na changamoto za maisha.
Hali ya elimu nchini hairidhishi. Matokeo yasiyoridhisha ya wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne katika miaka ya karibuni, yanatosha kuwa kiashiria cha hali mbaya inayoikabili sekta ya elimu.

Mitalaa
Mtalaa wa Taifa haukidhi tena mahitaji ya jamii pana. Mitalaa inapaswa kuboreshwa ili ishabihiane na mahitaji ya jamii kubwa na mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea.
Wananchi wengi wanaonekana kutaka kurudi kwenye mtalaa unaoendana na elimu ya kujitegemea, ili wahitimu waandaliwe kujitegemea na kumudu changamoto ndani ya jamii yao, hata kama watakosa fursa za kuendelea mbele waweze kuishi maisha yenye ustawi.
Matumizi ya kitabu kimoja
Wananchi wengi wanadai kuwa mfumo wa matumizi ya vitabu vya aina nyingi hauna tija kwa kuwa unawafanya wanafunzi wajifunze dhana zinazotofautiana wakati wakitarajiwa wafanye mtihani wa aina moja.
Kwa mfano, iwapo kitabu kimoja kitasema, ini ni sehemu ya ubongo na kitabu kingine kikasema ini linapatikana tumboni, maana yake ni kwamba watoto watakuwa wanachanganyikiwa.
Kwa hiyo, kuna haja ya kuifanyia marekebisho sera ya matumizi ya vitabu vya kiada iliyopo kwa sasa ili iwe kama ilivyokuwa zamani ambapo kitabu cha aina moja chenye ubora kilikuwa kinatumika nchi nzima.
Ubora wa vitabu
Ubora katika vitabu ni jambo nyeti na la muhimu. Vitabu ndiyo kiongozi kikubwa kwa walimu na ,hivyo waandishi wa vitabu lazima wazingatie ubora na ukweli wa maarifa.
Wakati soko huria la utengenezaji na usambazaji wa vitabu lililenga kupunguza uhaba mkubwa wa vitabu, kuna haja ya kudhibiti ubora wa vitabu ili kuhakikisha kuwa vitabu vinavyopendekezwa kutumika shuleni vinakuwa na ubora unaohitajika.Lugha ya kufundishia
Watoto hujifunza vizuri zaidi iwapo wataimudu lugha ya kufundishia. Vivyo hivyo kwa walimu wakati wa kufundisha. Suala hili linapaswa kutazamwa kwa makini zaidi ili kuhakikisha kuwa lugha ya kufundishia inafahamika vyema kwa walimu na wanafunzi.
Suala la lugha ya kufundishia limekuwa likiibua mijadala mizito na kwamba mwafaka umekuwa haufikiwi katika suala hili.
Kuna haja kwa Serikali kuchukua hatua madhubuti katika kuongoza majadiliano kuhusu lugha ya kufundishia katika mfumo wetu wa elimu ili kufikia mwafaka.
Vifaa vya kufundishia, kujifunzia
Ukosefu wa nyenzo na vifaa vya kufundishia na kujifunzia ni kikwazo katika utekelezaji wa mtalaa. Tatizo hili ni kubwa zaidi kwa vitabu vya sayansi na maabara. Ukosefu huu hauwezi kupuuzwa .
Kuna haja kwa wasimamizi katika sekta ya elimu kutilia mkazo suala la upatikanaji wa nyenzo za kutosha za kufundishia na kujifunzia katika shule zetu, kwa kuwa bila upatikanaji wa nyenzo hizo muhimu, ufanisi katika utekelezaji wa mtalaa hautakuwepo.
Mazingira ya shule
Kuna haja kwa wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya watoto wawe na furaha na amani. Shule inapaswa kuwa sehemu ambayo itawafanya watoto wafanikiwe kitaaluma na kimaisha.
Mafunzo kwa walimu
Kama kweli tunahitaji elimu bora hatuwezi kukwepa kuandaa walimu bora. Na walimu bora wanatokana na msingi bora wa mafunzo bora ya kutosheleza na yanayoendana na mtalaa na dira ya maendeleo za nchi.
Walimu wakiandaliwa visivyo watatoa elimu ya ovyo ovyo na hatimaye tutakuwa na wasomi bandia wanaofanya kazi ovyoovyo na kuwa na maendeleo duni.Muda wa mafunzo kwa walimu tarajali lazima uwe kamilifu. Wakufunzi wao lazima wawe bora, na mafunzo kwa walimu kazini lazima yafanyike kwa ukamilifu wake bila kuleta visingizio .
Kama sekta nyingine wanapata semina, kozi fupifupi kwa nini walimu wasipate mafunzo hayo?
Hakuna njia ya mkato. Ili fedha inayotengwa na Serikali kwenye elimu ilete tija basi mafunzo ya walimu ni muhimu ili kuandaa watekelezaji wazuri wa sera ya elimu.
Walimu na mazingira ya kazi
Mazingira mazuri ya kazi ndicho kigezo muhimu zaidi kinachoamua kiwango cha moyo wa kujitolea walio nao walimu katika kufundisha na matokeo yake kigezo hiki huwa na nguvu katika kuleta matokeo mazuri ya wanafunzi kitaaluma.
Bila kurekebisha hili uwekezaji mkubwa katika elimu hautaleta tija katika taaluma ya ualimu na elimu kwa jumla. Serikali na wadau wengine washirikiane kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya walimu.
Pia kuwepo usimamizi thabiti kuhakikisha kuwa walimu wanatimiza wajibu wao. Hii itasaidia kujituma zaidi na kuleta ufanisi katika kazi. Masilahi ya walimu yaboreshwe na pia walimu wapandishwe madaraja na kulipwa stahili zao bila kucheleweshwa
Motisha kwa walimu
Jitihada mahsusi za baadhi ya walimu zitambuliwe na walimu hao watuzwe ili kuwatia moyo na kuwahamasisha wengine kufanya kazi yao kwa bidii. Kujituma na kuwajibika ni sehemu muhimu ya maadili ya walimu, hivyo inawapasa walimu wote nchini wazingatie hili, hata kama wana hoja ama madai mengine ya msingi.
Utekelezaji wa sera na mipango
Nchi haiwezi kuendelezwa na watu wachache wanaopata fursa za kipekee kwenye shule chache huku elimu ya jamii pana ikiwa shakani.
Hakuna haja kulumbana wala kuingiza siasa katika elimu, bali Serikali itekeleze mipango na sera zilizopo na kuboresha mapungufu kwa kushirikisha wadau.Makala haya ni rejea ya maelezo yaliyomo katika kijitabu kiitwacho Hali ya Elimu Tanzania: Utafiti na uhalisia vinatuambia nini kilichochapishwa na Shirika la HakiElimu