LUSAJO L.M.
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 272
- 129
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba CCM wameandaa mikakati michafu kuhakikisha kwamba wanashinda Uchaguzi wa Ubunge jimboni Ubungo kwa gharama zozote. Wamekaa kikao na kukubaliana yafuatayo kuhakikisha mgombea wao anashinda:
Tutazidi kuwapa taarifa jinsi mambo yanavyoendelea.
kny: JOHN J. MNYIKA.
- Kugawa kila mtaa Shilingi za Kitanzania Milioni Moja (TZS 1,000,000/=) ya kuhonga wananchi tarehe 29 na 30 Oktoba, 2010. Tunayo majina ya baadhi ya wasambazaji.
- Wamepanga kupita na gari Tarehe 30 Oktoba 2010 na pia kutumia Mabalozi kusambaza uvumi kuwa Mnyika ameamua kumwachia Hawa Kiti cha Ubungo.
- Wamekubaliana watumie polisi kuweka rumande vijana vijiweni mpaka jumatatu kupunguza kura.
- Mabalozi wameelekezwa watafute watu wawili wa kupiga kura vituo hewa. Tayari CHADEMA imevitambua vituo hewa na kuandika barua ya kuvikataa.
Tutazidi kuwapa taarifa jinsi mambo yanavyoendelea.
kny: JOHN J. MNYIKA.