Mbinu wanazotumia shule binafsi kufaulu sana

mashizo

Member
Joined
Feb 24, 2009
Posts
43
Reaction score
32
Habari zenu wana JF,
Hapa nitaelezea kwa kina mbinu wanazotumia shule nyingi za binafsi ambazo huwa zinafanya vizuri.
Mimi binafsi nimesoma shule ya Feza Boys miaka kadhaa iliyopita na kwa sasa ni Engineer japokuwa wazazi wangu walikuwa maskini sana, shule iligharamia kila kitu kuanzia form one mpaka form six.

1) Wanafunzi kuwa na vitabu vya masomo yote kwa kila mwaka wa masomo.
shule inatoa vitabu kwa wanafunzi wote kila mtu na kitabu chake toka mtu akiwa form one.Pia wanapewa vitabu vyote kila mwaka yaani wakiwa form two, three na four.

2) Wanafunzi kuwa na muda wa kujisomea kila siku.
Wakati nikiwa pale wanafunzi wote lazima kila siku wasome madarasani jioni baada ya mlo wa jioni.
Kusoma wanaanza saa moja jioni mpaka saa nne usiku na kuna viongozi ambao wanakuwa wanasimamia wanafunzi kusoma na kuwasaidia pale wanaposhindwa kuelewa kitu wanachokisoma

3) Mitihani ya kila wiki
Kila wiki kuna mtihani mmoja wa somo moja kwa kila darasa. Kwa mfano kama wiki hii mkifanya physics basi next week mnafanya english au somo lingine lolote. Wanafunzi wote wanaofanya vizuri kwa kila darasa uitwa mbele na wanaofanya vibaya pia. Mtu akiwa wa mwisho zaidi ya mara tatu basi mzazi wake uitwa na kupewa taarifa na wanajadili jinsi ya kumsaidia huyu mwanafunzi

4) Wanafunzi kukatazwa kutumia simu
wanafunzi hawaruhusiwi kumiliki simu kipindi chote cha shule. Wanaruhusiwa kuwa nazo ila lazima waziweke kwa viongozi maalum wa maadili ya wanafunzi na wanazitumia pindi tu pale ambapo wanahitaji kuwasiliana na wazazi wao.

5) Wanafunzi kuwa na nidhamu kwa walimu na kati ya wanafunzi kwa wanafunzi
Wanafunzi wanafundishwa maadili mema kati yao wenyewe kwa wenyewe au kwa watu wengine. Kama mtu hana nidhamu shule inamfukuza ata kama baba yake akiwa na uwezo wa kifedha namna gani

6) Mazingira mazuri ya shule
Shule kuwa na mazingira mazuri pia inachangia kwa kiasi kikubwa ufaulu wa wanafunzi. Mwanafunzi anapokuwa katika mazingira mazuri ata akili pia ufurahia na inakuwa rahisi kujifunza vitu kirahisi sana.

7) Waalimu bora na wenye motisha ya kufundisha
Waalimu wanalipwa vizuri hivyo wanafundisha kwa moyo wote na wanakuwa happy kufundisha, pia tabia za usikivu za wanafunzi uwafanya waalimu kupenda kazi zao

Baada ya kuelezea baadhi ya sababu tajwa hapo juu. Mimi binafsi naona serikali inaweza kufanya baadhi ya mambo hapo juu na idadi ya wanaofeli kila mwaka inaweza kupungua na kutengeneza vijana wenye upeo mkubwa kwenye mambo mengi.

1) Serikali iwanununulie vitabu wanafunzi - kila mwanafunzi awe ana vitabu vyake kwa ajili ya masomo yote. Uwezo wa kufanya hivi tunao ata ikibidi serikali kukopa lakini kutengeneza taifa la wanafunzi wenye upeo na uelewa kwani ni azina ya vizazi vijavyo

2) Serikali pamoja na taasisi mbalimbali zihamasishe wanafunzi watumie muda mwingi waweze kujisomea badala ya kuhamasiha maaparty kama ya kina diamond na mambo mwengine ya starehe. Party wanafunzi wanaweza kwenda ila kipindi cha likizo ambacho watakitumia kurifresh mind zao baada ya kupiga msuli semester nzima.

3) Serikali ikae chini na waalimu na itatue madai yao ya msingi - mwalimu ata awe anajua vitu kiasi gani lakini kama hana motisha ya kufundisha basi ni kazi bure tu.

4) Serikali ijifunze kutoka kwa shule binafsi na serikali zinazofanya vizuri.

5) Serikali iongeze idadi ya shule za bweni ambazo pia lazima ziwe na usimamizi mzuri na sheria ambazo inabidi zifuatwe.

6) Wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni - hii ni pamoja na kujua mwanao mwelekeo wake ukoje toka akiwa form one hii itasaidia mzazi kuchukua hatua stahiki mapema zaidi maana mwanafunzi anaeelekea kupata sifuri huwa anajulikana toka mwanzo.
 
Ni kweli hao jamaa wako thorough sana ukilinganisha na walimu wa shule za serikali. huenda wanapewa motisha ili wafanya hivyo
 
tulipoambiwa elimu ya bure inawezekana tukabisha na matusi juu. lakini ukitazama kiuhalisia tuna uwezo kabisa wa kufanya yote haya isipokuwa tu hatuko tayari kwa sababu ya mfumo mbovu wa serikali yetu dhaifu.
 
Hakuna elimu ya bure.

Serikali inafanya kama vile elimu ni ya bure (kwa kutokugharimia vitabu, mahitaji ya walimu kielimu na kitija, maabara, nk) na ndiyo kisa cha matokeo tunayoyasikia.

Utawasikia watu wengine wakidai shule za binafsi zishushe ada na hata kufikia kulingana na za serikali. Wanachodai ni sawa na kutaka watoto wote wafanane kwa kukosa elimu. Cha kudai ni serikali igharimie kuboresha shule zake.
 
" Waalimu bora na wenye motisha ya kufundisha
Waalimu wanalipwa vizuri hivyo wanafundisha kwa moyo wote na wanakuwa happy kufundisha"


Hili ndilo kuu walimu wanadedicate muda wao wote kwa wanafunzi.
Hivyo huwapa mafunzo ya kutosha na kuwasimamia vyema katika kazi zao, pia kuwafundisha descipline ya kusoma
 
Umesahau mbinu nyingine ya kuchakachua mitihani shule binafsì

mkuu mzalendo shule binafsi hawachakachui ata kidogo mimi nimesoma miaka sita na hakuna ata siku niliyoona watu wakichakachua. kwa mfano sisi enzi zile ili mtu aendelee kidato cha mbele lazima awe na average pass mark ya 55% na mtu wa mwisho class yetu alikuwa na 58% apo ndio utajua kwa nini shule binafsi zinafanya vema. na matokeo yalipotoka ya form four mtu wa mwisho alikuwa na two ya point kumi na nane.
 
Anachosema mashizo ni sahihi serikali inaouwezo wa kuwekeza kwenye elimu,tatizo la viongozi wetu ni kulewa madaraka na umimi uliokidhiri.

Ubinafsi wa kujilimbikizia mali na kudharau watoto wa mtanzania wa kawaida au maskini.Watanzania kupitia wabunge wetu tuamke sasa maana asubuhi inapita na ndio tupo kwenye soko la Afrika Mashariki.
 
Mengi ya uliyoyataja hapo ndio tulikuwa tunapatiwa kwenye shule za secondari za serikali miaka ya mwanzo ya 90. Isipokuwa vitabu ndio vilikuwa havitoshi lakini walimu walikuwa very happy na wanajitolea hadi kufundisha usiku bila hela. Ukikosa PREPO unashugulikiwa ipasavyo.

Kwa wakati huu serikali hii ya huyu jamaa wa Msoga na MaCCM wengine ushauri wako watuona kama nguvu za giza. Haya yote uliyoandika wanayafahamu vizuri sana, lakini kwa kuwa maCCM ni mafreemasonry yanafurahia kuwa the more wanafunzi wanafeli the more wanakuwa maskini na umaskini wa mtanzania ni mtaji wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…