Mbinu ya kuteua na kutengua viongozi Serikalini iliwahi kufanywa Ulaya Mashariki miaka ya 90 baada ya kuvunjika Umoja wa Kisoviet. Ni njia za hadaa

Mbinu ya kuteua na kutengua viongozi Serikalini iliwahi kufanywa Ulaya Mashariki miaka ya 90 baada ya kuvunjika Umoja wa Kisoviet. Ni njia za hadaa

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
KWa sasa Mada kuu ni Tengua hamisha, Tengua badilisha, tengua, teua, tengua baada ya mwezi tengua.

Nchi za Ulaya Mashariki baada ya kuanguka kwa Ujamaa zilijikuta katika hali mbaya ya kiuchumi na kushindwa kutoa huduma muhimu kwa raia wao. Hii ilitokana na kuwa hawakuwa na maendeleo makubwa kama Ulaya Magharibi.

Njia ilio tumiwa ilikuwa ni kutengeneza matukio kila baada ya muda fulani au siku kadhaa ili kuwafanya raia kutumia muda mwingi kudiscus matukio na kusahua kujadili maswala muhimu kama ukosefu wa ajira, huduma duni za afya, udmfisadi, tatizo la maji na matatizo mengine. Mfano ilikuwa ikizuka tatizo la ufisadi ili kulizima ilikuwa inatengenezwa Bonge la tukio na watu wanahamisha mada faster.

Njia walizo tumiani ni hizi hizi za kufanya teuzi kubwa za kushitukiza, kufukuza watu kazi, saa zingine hata kutengeneza tukio kubwa sana la mauji. matukio ya kutengeneza ya ajali. haya yote ilikuwa ni mkakati wa kuwafanya wananchi kutumia muda mwingi kujadili matukio au kuhamisha mada.

Sas Samia anacho fanya ni kile kile, teua, hamisha, tengua, tengua hamisha teua. Haya yote hayana impact kwa raia still matatizo yako pale pale. Ila sasa yanasaidia kutengeneza mada za wajinga kudiscus baada ya kuwa wameshiba ugali.

Bahati nzuri sasa kwa Tanzania kuna pia mada ya Yanga na Simba hii ni sapoti kubwa sana kwa watawala. Wajinga wakisha shiba vitumbua lazima waanze mada za yanga na Simba huwezi wakuta wanakadili mambo ya maana.

Hizi teua, tengua, hamisha teua hazina tija, matatizo yako pale pale hakuna unafuu hata chembe na ni njia za kucheza na akili za wajinga tu.

Ni njia ya kutengeneza
matukio ili raia wapate mada za kujadili. Wajinga sana sisi
 
Msukule humuamini mhuni hasa akifanya Jambo kinyume na ilivyo kawaida yake.
#Manipulation.
 
Hatujasahau bandari zetu zilivyotiwa najisi!!
 
Mto mada naye anajikuta bingwa wa geopolitics hahah!
 
Walau huko nyuma kungekuwa na mitandao ya kijamii ningekuelewa,,,naona unaleta porojo chief
 
Lazima awaweke watu busy masikio na macho katika tengua tengua. Unadhani mambo yanayoendelea EA yatawaacha salama, kila mmoja lazima anywe kikombe cha shubiri. Nilitabiri baada ya Gen Z wa Kenya next ni Uganda ikawa. Natabiri tena kituo kinachofata ni Tz...
 
Kwahiyo kwa mtazamo wako,hizi teuzi na tengua ni kuwaweka watu busy?
 
Na hii njia human ina workout sana, watu tumesha sahau mambo ya mpina na bashe. Ila kweli wahuni siyo watu, Bashe bado yupo ofisini
 
Na hii njia human ina workout sana, watu tumesha sahau mambo ya mpina na bashe. Ila kweli wahuni siyo watu, Bashe bado yupo ofisini
Hii njia ina workout mbaya mno, nani anajadili swala la Sukari? nani anajadili Bandari? nani anajua kama pesa zimepigwa BOT au la?
 
Back
Top Bottom