Pole sana kwa huyo dada aliyefanyiwa ubaya na dada wa kazi...amrudishe kwao huyo msichana wa kazi hafai kuendelea kuishi naye. Kama bado haujabahatika kutendwa na wasichana wa kazi mshukuru mungu lakin lisemwalo lipo na kama halipo basi laja jihadhari nalo.
Dada wa kazi ni sawa na binadanu yoyote yule ,wana mazuri yao na wana mapungufu yao kama tulivyo mimi na wewe.
Ni kweli kuwa kuna baadhi ya waaajiri wa wadada wa kazi wana watreat vibaya sana hao wasaidizi wa kazi, lakin pia
kuna baadhi ya waajiri wanaishi vizuri sana na wasichana wa kazi. Wanathamini uwepo wa mfanyakazi, wanampenda,wanamjali,wanamsilikiza,wanamfundisha,wanamwelekeza, anakuwa sehemu ya familia yao katika raha na shida.
Ukipata mfanyakazi mzuri mshukuru mungu na jitahidi kadri ya uwezo wako kuishi naye vizuri, lakin pia ukipata mfanyakazi mwenye tabia mbaya asiyerekebishika basi suluhisho ni kumwondoa tena kwa utaratibu mzuri,mrudishe mpaka nyumbani kwao kama ulivyomchukua usimfukuze kama mwizi hata kama kakufanyia vibaya...ipo siku ataukumbuka wema wako japo yeye alikufanyia ubaya.
Kwa jinsi tulivyo busy kutafuta pesa (kikazi au kibiashara) wasichana wa kazi ni watu muhimu sana majumbani mwetu, na ukipata msichana mzuri wa kazi unaweza usione shida sana kulea watoto wako,pia unaweza kupata kishawishi cha kuzaa watoto idadi unayopenda uwe nayo,,lakin kama haujabahatika msichana mzuri basi hata suala la kuzaa linaweza kukupa shida kidogo hasa ukifikiria kulea mtoto/watoto pamoja na majukumu mengine ya kazi.
Japo wasichana wa kazi ni wengi lakin wanaojitambua,thamini,penda kazi yao na kuwajibika ipasavyo ni wachache sana,,wengi wana nia na malengo mabaya kila waingiapo nyumbani kufanya kazi.