"Mbinu za Jadi za Kichina za Kutengeneza Chai na Desturi Zinazohusiana” zilizowasilishwa na China tarehe 29 Novemba, zilipitishwa kwenye Mkutano wa 17 wa Kamati ya Kiserikali ya UNESCO ya Kulinda Urithi wa Utamaduni Usioshikika uliofanyika huko Rabat, Morocco, na kuorodeshwa kuwa Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu na UNESCO. Hadi sasa, China ina jumla ya vitu 43 vilivyoorodheshwa ikishika nafasi ya kwanza duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China Wang Chenyang amesema anafurahishwa kwa kusikia habari hii kwani kwa mara nyingine tena inaonesha mchango muhimu wa ustaarabu wa China kwa utamaduni wa binadamu.