Mbinu za kuangua vifaranga kwa njia ya Kienyeji

mkuu@chasha kuku wangu aliatamia mayai 12 lakini cha kushangazaza alitotoa kifaranga 1 tu je ni makosa gani yaliyofanyika hapo? au ni kawaida kutokea ivyo?

Pole sana mkuu, Kuna sababu kama mbili tatu hivi.

1. Mayai kutokuwa na mbegu- Hapa majogoo ni machache sana au ni wengi kiasi kwamba wanafukuzana tu na hakuna wanacho kifanya.

2. Mayai yalipitiliza muda wake wa kutakiwa kuatamiwa- Mara nyingi siku 7 ndo the best baada ya siku saba hatch bility huanza kupungua sana.

3. Mayai hayakuhifadhiwa vizuri-Hapa kuna ishu ya mayai kushikwa na maji, Mafuta, au kuwekwa sehemu yenye joto kubwa na kazalika
-Hakikisha mayai yanahifadhiwa vizuri kwenye tray sehemu iliyo chongoka iwe chini.

4. Kuku wako ni mzembe- Kuna kuku kwa kweli huwa hawana sifa za kuatamia mayai vizuri, utakuta kila mara yuko nje
 

mkuu Chasha ufafanuzi tafadhali hapo no.2, una maana tuwekee kuku mayai 7 tu ya mwisho kutagwa?
 
Last edited by a moderator:
mkuu Chasha ufafanuzi tafadhali hapo no.2, una maana tuwekee kuku mayai 7 tu ya mwisho kutagwa?


Mkuu kwa kawaida yai likitagwa inatakiwa ndani ya siku liwe tiarayi limewekwa kwa mashine au kuku kaanza kulalai, baada ya siku saba hatch bility inanza kushuka, ingawa unaweza kuta hata la siku 10 lina totolewa ila mara nyingi hatchibility inakuwa kubwa kwa mayai yenye only 7 day baada ya kutagwa. Na hata kuku mara nyingi yale mayai aliyo taga ya kwanza huwa hayatotolewa, ukikuta kuku katotoa vifaranga kadhaa za kaacha baadhi ya mayai mara nyingi huwa ni yale ya mwanzo kutagwa.

Ni vizuri yale mayai ya mwisho kutagwa ndo awekewe kuku na yale ya mwanzo unaweza kula au kuuza,
 


Mkuu Chasha
Pamoja na hayo kuna baadhi ya kuku hutaga na kufunga lakini hawaatamii kama wengine.
Je kuku kama hawa unatushaurije?

Je ni kweli kuna Chakula cha kuku kinaitwa Layers ambacho ukiwapa kuku wa wowote awe wa kienyeji au wa kisasa watataga sana tafadhali naomba ufafanuzi.
 
Last edited by a moderator:

Pamoja mkuu nayapitia maelezo haya taratibu mpaka yakae kichwani. thanks
 

Mkuu kuku wanaotaga bila kuatamia ni chotara, ila kienyeji pure wanaatamia, ingawa kuna chotara wanao lalia na hawa ni wale wanao chukua tabia za kuku wa kienyeji.
Hawa wanaotaga bila kulalia ni lazima mayai yao wapewe kuku wanao atamia au tumia mashine.

Kuhusu msosi wa layermash ni kweli ni kwa ajili ya kuku wanao taga, ila kwa kuku wa kienyeji hata ukiwalisha vipi watataga then wataanza kuatamia, so hawawez taga mfululizo kama kuku wa mayai
 
Last edited by a moderator:
Nashuku kwa kuileta hii madaa. Nimepata shule nzuri hapa.
 
nasikia kuna kuku wa kienyeji kutoka nje wapo nchini wanataga sana alafu wanaatamia mayai. Niambie kama unafahamu lolote kuhusu kuku hawa.
 
Mkuu Chasha. Mm nna kuku wanatetea sana lkn coni matokeo kwa maana ya kutaga. Kipindi cha nyuma mmoja alikuwa anatetea badae kaacha na saivi tena wanatetea tu japo wanakula vzuri na jogoo wangu ni mzuri. Mkuu ivi hii ni nn? Naomba uzoefu na ushauri...
 
Mkuu jaribu kuingia hapa uone kama utaweza kutengeneza kitu kama hiki. Ikiwa ni kwa matumizi binafsi na sio kwa biashara naona itakufaa
www.nif.org.in/bd/product-detail/rural-egg-incubator

 

Wana umuri gani? Make kuku wa kienyeji some time hufikia hadi miezi 7 -8
 
Mkuu jaribu kuingia hapa uone kama utaweza kutengeneza kitu kama hiki. Ikiwa ni kwa matumizi binafsi na sio kwa biashara naona itakufaa
www.nif.org.in/bd/product-detail/rural-egg-incubator


Hakuna link mkuu.
 
Kuku akishasikia sauti ya kifaranga baada ya siku mbili hutoka kwa maana anajua ameshaangua hivyo unaweza kuharibu mayai.

ukimunyanganya vifaranga na kuviweka mbari baada ya kutotoa. lazima aludi kwenyekiota chake hatakama hakina mayai
 
mkuu@chasha kuku wangu aliatamia mayai 12 lakini cha kushangazaza alitotoa kifaranga 1 tu je ni makosa gani yaliyofanyika hapo? au ni kawaida kutokea ivyo?

huenda haukumuandaa. utitiri chawa na viroboto, ni sababu nyingine ya kuku kuto totoa vizuri.
 

namba (2) si kweli. kitaaramu mayai yasizidi siku 14, japo kuku anaweza akatotoa hata mayai 18, aliyo taga mwenyewe. wafugaji wanao fuga kijadi. vijijini, watakubariana na Mimi. kwani huko kuku hutotoa vifaranga vingi tu. nikipata nafasi nitaweka chapisho la kitabu nilicho kitoa (SUA) ili tuelimike ote, nilichelewa kutoa mchango wangu huu kwakuwa nilipigwa BN, asanteni.
 


Tunakusubiri mkuu.
 
Njia za kienyeji ni za kutumia kuku, na zaidi ya kutumia kuku ni kutumia mashine, kuhusu mashine ni kweli ni ghari sana ila unaweza jipanga ukanunua hata ya mayai 45 au mayai 60 ambazo hazizidi laki 30000.
Mkuu, habari za jioni?

Mkuu naomba kufahamu, solar za aina gani zinaweza kuendesha hizi mashine?

uwezo wa kununua hiyo mashine ninao, naomba kwanza mwongozo wa solar.
 

mkuu hapo kwenye red, kuku wa hivyo unaweza kum-handle namna gani? halafu,

ratio inayotakiwa hasa kati ya jogoo na tetea ni ipi mkuu? yani kuku jike wangapi wanatakiwa wamilikiwe na jogoo mmoja ili kuokoa vita kati ya majogoo?

asante..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…