BabWoo
New Member
- May 22, 2024
- 2
- 1
Huwezi zungumzia sekta zenye mchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu bila kuitaja sekta ya utalii. Imekua ikichangia pato la taifa na ajira kiujumla. Licha ya uwepo na utajiri wa maliasili na vivutio vya utalii sekta hii imekua ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazozuia ukuaji wake wa haraka na endelevu. Zifuatazo hatua mbalimbali ambazo zitaifanya Tanzania ifikie ndoto ya kuwa kivutio kikubwa cha utalii duniani na kujenga uchumi imara.
1. Kutengeza na kuboresha Miundombinu.
Barabara na Usafiri:
- Kuimarisha na kujenga barabara za lami na zenye nakshi ya asili kama za mawe kwa maeneo yenye miamba, madaraja ya kibunifu ya mbao kwa maeneo yenye miti mingi na barabara zote zinazounganisha maeneo muhimu ya kitalii na miji mikubwa.
- Hii inajumuisha barabara kuelekea kwenye mbuga na hifadhi za taifa, barabara za kupanda milima iliyopo nchini, ziwekewe creative na artistic crafts zenye kuitangaza ‘Sanaa na Utalii’ wa Tanzania.
- Kupanua na kuboresha viwanja vya ndege vya kimataifa na vile vilivyo karibu na maeneo ya utalii kama vile Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro.
- Kuongeza na kuboresha vyombo vya usafiri vya kisasa vitavyoweza kufacilitate huduma za kuwafikisha watalii na wataalamu wa sekta hii katika mahala wanapohitaji kwa ufanisi mkubwa wa kazi.
Huduma za Msingi:
- Kuweka miundombinu bora ya maji safi, vyoo na umeme katika maeneo ya kitalii ili kuboresha huduma za hoteli na maeneo ya malazi.
- Kuongeza upatikanaji wa mawasiliano bora (internet na simu) katika maeneo ya kitalii. Hususani yale yalio mbali na miji mikubwa. Ikiwezekana hata kuwa na potable routers zenye minara kurahisishia watalii kupata mtandao na kututangaza zaidi.
2. Kuboresha Huduma za Utalii na Ukarimu
Mafunzo ya Wafanyakazi
- Kutoa mafunzo ya hali ya juu kwa wafanyakazi wa sekta ya utalii kwenye vyuo vya utalii na ukarimu nchini. Mafunzo hayo ya-base kwenye kulenga matakwa ya watalii na manufaa ya taifa kutoka katika utalii.
- Kufanya warsha na semina za mara kwa mara kwa wafanyakazi ili wawe na ujuzi wa kisasa na huduma bora kwa wateja.
- Kutoa tuzo kwa wadau na taasisi zote zilizofanya vyema katika kukuza, kutangaza na kudumisha utalii kwa ndani na nje ya nchi
Ubora wa Huduma:
- Kuhimiza uwekezaji katika hoteli za nyota tano na kuhimiza ubora katika huduma za malazi, chakula, na usafiri wa watalii.
- Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa huduma za kitalii ili kuhakikisha viwango vya juu vinazingatiwa.
3. Utunzaji wa Mazingira
Utalii Endelevu:
- Kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na teknolojia rafiki kwa mazingira kwenye maeneo ya kitalii. Kwa mfano, kutumia nishati ya jua kwenye hifadhi kama ya Serengeti yenye tambarare kubwa na miale ya kutosha.
- Kuimarisha utalii wa ikolojia kwa kukuza vivutio vya asili, kama vile mbuga za wanyama na hifadhi za bahari.
Dhibiti Athari za Mazingira:
- Kuweka sheria kali za kudhibiti uchafuzi wa mazingira, ikiwemo taka ngumu na maji machafu kutoka kwenye hoteli na migahawa.
4. Masoko na Uhamasishaji
Kampeni za Kimataifa:
- Kufanya kampeni za matangazo kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na majukwaa ya kidijitali kama vile mitandao ya kijamii, tovuti za utalii, na blogu za usafiri.
Mfano, kuanzisha shindano maalumu la kupromote utalii ambapo washindi watapata ofa ya kutembelea vivutio vya utalii bure ama kwa gharama nafuu.
Maonesho ya Utalii:
- Kushiriki kwenye maonyesho ya kimataifa ya utalii kama vile ITB Berlin na WTM London ili kuongeza ufahamu na kuvutia watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
- Kuandaa maonesho ya ndani na kimataifa yanayolenga kuonyesha utajiri wa vivutio vya utalii vya Tanzania.
Matumizi ya DIASPORAS na INFLUENCERS
- Kufanya kazi na washawishi maarufu wa kijamii au watu maarufu ambao wanaweza kusaidia katika kukuza Tanzania kama marudio ya kuvutia kwa watalii.
- Kuwapa elimu ya utalii diaspora wote wa kitanzania na kuwapa mbinu madhubuti za kuutangaza utalii wa nchi yetu popote watakapokuapo zaidi kwa kutumia mitandao.
5. Kuimarisha Sera na Sheria
Sera za Utalii:
- Kuunda sera zinazovutia wawekezaji wa nje na wa ndani katika sekta ya utalii, ikiwa ni pamoja na vivutio vya kodi na motisha za kifedha.
- Kuhakikisha kuwa sera zinazingatia uhifadhi wa mazingira na haki za wenyeji.
Sheria Madhubuti:
- Kuweka sheria kali za kupambana na ujangili na biashara haramu ya wanyamapori ili kulinda maliasili za kitalii.
- Kuimarisha sheria za usalama kwa watalii ili kujenga mazingira salama kwa wageni wote.
6. Ushirikishwaji wa Jamii
Faida za Kiuchumi:
- Kuanzisha miradi ya utalii wa kijamii ambapo jamii za wenyeji zinahusishwa moja kwa moja na kunufaika na mapato ya utalii. Kama vile kuwatumia wenyeji kama tour guiders na wakufunzi wa tamaduni katika utalii.
- Kutoa mikopo midogo midogo na mafunzo kwa jamii za wenyeji ili waweze kuanzisha biashara zinazohusiana na utalii, kama vile kuuza bidhaa za kitamaduni hususani karibu na maeneo yenye wingi wa shughulu za kiutalii.
Elimu kwa Jamii:
- Kuendesha kampeni za uhamasishaji na elimu kwa jamii kuhusu faida za utalii na umuhimu wa kuhifadhi vivutio vya kitalii.
- Kuweka vituo vya taarifa na elimu kwa watalii na wenyeji kuhusu utalii endelevu.
7. Ubunifu na Uvumbuzi
Vivutio Vipya:
- Kukuza na kutangaza michezo ya maji kama vile kupiga mbizi, safari za boti, na kuteleza kwenye mawimbi katika maeneo kama Zanzibar na Pwani ya Kaskazini.
- Kutangaza maeneo ya kihistoria kama vile Magofu ya Kilwa na Bagamoyo kwa watalii wanaopenda historia.
Teknolojia ya Kidijitali
- Kutumia teknolojia kama vile programu za simu za mkononi, drones na tovuti zinazowezesha watalii kupata taarifa na kufanya maombi ya huduma za kitalii.
- Kuanzisha mifumo ya malipo ya kidijitali ili kurahisisha shughuli za watalii.
- Kutumia teknolojia kama vile mitandao ya kijamii, programu za utalii, na teknolojia za ubunifu kama vile ukweli halisi na ukweli ulioboreshwa (Virtual Reality) kuongeza ufahamu na kuvutia watalii.
Kwa kuchukua hatua hizi, Tanzania inaweza kuimarisha sekta ya utalii na kujenga mazingira yanayowavutia watalii kutoka duniani kote, hivyo kuleta maendeleo endelevu kwa taifa.

Upvote
7