Mbinu za Kuishi muda mrefu bila Kufa kwa Njaa hata kama huna kazi

Mbinu za Kuishi muda mrefu bila Kufa kwa Njaa hata kama huna kazi

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusiana na hali mbaya ya kiuchumi na wengi kudai wanakula mlo mmoja kwa siku. Wataalam tumekaa chini na kungalia namna ambavyo unaweza survive kwa muda mrefu pasipo kufa kwa njaa. Kufa kwa magonjwa au ajali hiyo ni mipango ya muumbaji lakini kwa njaa tena nchini Tanzania ni uzembe wako.

Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo wataalamu toka vyuo vikuu mbalimbali vya kitaani wameziainisha. nami mwanaume wa shoka a.k.a gudume nakuletea baada ya kuendesha semina ya miezi sita kujadili mambo haya.

1. Hakikisha kwanza unawatafuta marafiki zako woooote wa kuanzia shule ya msingi, shule ya sekondari o-level , sekondari A- level na kama ulifanikiwa pia chuo. kuwa na namba zao au ufahamwa wanapoishi. Ni rahisi.

Ukimpata A atakuelekeza anapoishi B, Ukimpata B atakuelekeza anapoishi C, ukimpata C atakuelekeza D na kuendelea mpaka utakapokuja kumpata Z then utarudi AA atakuelekeza alipo AB, AB atakuelekeza alipo AC na kuendelea.

2. Anzisha kundi la whatsapp au kama lipo tayari jiunge. Kuwa mchangiaji na mtu mwenye ukaribu sana na wadau wengine wa humo ndani. Anza kusisitiza kuwa kundi liwe la maendeleo na inabidi mkumbukane.

3. Panga list ya kuwatembelea watu majumbani kwao. anza maybe na wa shule ya msingi. hakikisha tu una nguo zako nzuri za kutokea. Halafu anza kuwatembelea majumbani kwao kwa chakula cha mchana anza na akina mama au wanawake. Asilimia kubwa utakuta wapo nyumbani kwao.

Mpigie simu mwambie sister nipo mitaa ya huku kwenu nimeona nitumie nafasi hii kuja kuwasalimia akina Uncles. Ukienda kwake mida ya saa sita nakuhakikishia siku hiyo chakula cha mchana utapata hapo. Kama ni mjanja una story nyingi ukishiba unamwambia aaaah sister..

Umenimaliza kabisa hapa hata kusimama siwezi sijawah kushiba hivi toka nimezaliwa. Mwambie ngoja upumzike kidogo mida mida ikienda muulize shemeji huwa anarudi saa ngapi akisema saa moja au saa mbili mwambie ngoja nimsubirie kabisa tufahamiane. Unagonga na cha usiku.

4. Hapo unaangalie next target atakuwa nani siku ifuatayo. naye jipange kama ulivyofanya leo utakuta umesogeza week au masiku mengi tu ili mradi uwe na uwezo wa kutembea na labda nauli kiasi kama 1000 kwa ajili ya dharura.

5. Kama una majirani hakikisha unakuwa karibu sana na majirani zako. Ukisikia kuna jirani anaumwa lazima ujue mida mizuri ya kwenda kumsalimia. Kama ni mchana nenda kuanzia saa sita na nusu hivi na hakikisha unamsalimia na kukaa kaa naye mpaka saa nane au nane na nusu huo muda lazima chakula cha mchana kitaliwa. Ukishakula unakaa kama nusu saa hivi unaaga.

Lakini kama inabidi kwenda kumuona jioni basi nenda mida ya saa moja na nusu. hapo ukikaa kaa mpaka saa tatu lazima mida ya kula itaangukia humo. Piga msosi wako wa kutosha. Ili ule chakula kingi hakikisha unamsifia sana jamaa kuwa kweli mke wake anajua kupika. hujawah kula chakula kile toka uzaliwe.huku ukiongeza tena kwa mara nyingine.

6. Kama kwa jirani hamna mgonjwa basi msome jirani yako ni mshabiki wa team gani, anapenda chama gani, au kama ni wa dini sana yeye ni msimamo gani. Kama ni wadini ifikapo mida ya saa moja moja ukijua amerudi au saa mbili nenda na kitabu husika cha dini. Mwambie kuna mistari akufafanulie au nenda na nia ya kupata maombe au neno la Mungu.

Hapo na chakula utakula. mwambie pia una tatizo ambalo unataman ungekuwa unapata maombi kila mara siku hiyo mkiomba kesho rudi mwambie umepata nafuu muombe tena. keshokutwa nenda kamshukuru mida ile ile. Siku tatu chakula cha usiku umekula kwake.

7. Kama ni mwanamichezo hakikisha una ratiba ya VPL,Laliga,Seri A, Bundesliga na ile ya France na EPL fuatilia sana michezo ikifika mida ya michezo tia team kwake nusu saa kabla. Mwambie TV yako imeungua unataka uone Simba jana Kampiga mtu Mkono/ Kofi (magoli 5) au week iliyopita alimpiga mtu week (magoli 7) unataka kuona. hasa goli la mzamiru mwambie ni goli ambalo kuna Morinyo ameliona anataka kulinunua.

Hapo ni kwa mshabiki wa simba. kama ni wa yanga.... Mwambie umesikia habari za tshishimbi...yule jamaa ni balaa...kile kiku kuku kina mpa uwezo mkubwa wa kulisakata gozi na kuonesha mautundu. Alitakiwa akacheze mpira mwezini sijui kwa nini alikuja hapa afrika....anza kumpa historia. Muda wa kula unakula unaondoka zako.

8. Kama ni wa siasa nenda na habari za tundu lissu, nenda na habari za makinikia,magwangala na maboso nenda na habari za magufuli namna anavyowanyoosha wapinzani.

ONYO.. unapaswa kujua mwenyeji wako anapendelea nini na yupo kambi gani. hakikisha umesoma sana magazeti na umepitia JF ukapata habari nyingi humu. then nenda kashushe nondo.utafika wakati wakula mtakula utarudi kwako kulala

9. Kama ni jamaa mlisoma naye shule kwenye maongezi mkumbushe jinsi alivyokuwa ana akili, mjanja, watu wanamwogopa,wanawake wanampenda au wanaume wanampenda. Jinsi ambavyo ulikuwa unataman uwe kama yeye, jinsi ambavyo alikuwa mpole na mstaarabu.

Kama anapenda sana sifa hapo mkumbushe jinsi ambavyo pia aliwah kuwadunda jamaa flan shuleni,alivyokuwa anawagegeda mademu(kama alikuwa ameshaanza hiyo michezo) huwez kosa la kuzungumzia ikiwa umeamua seriously.

10. Jaribu sana kuhudhuria misiba, sherehe n.k uwe update na mambo mbalimbali yanayoendelea mtaani au duniani. ukiweza kuzingatia haya. unaweza jikuta suala la kula halikusumbui sana. hakikisha umepanga ratiba yako vizuri.

ANGALIZO: Hakikisha kuwa unavaa vizuri, na usionekane kama ni mtu mwenye shida. pia ukiweza kupata majina hata 250 kuanzia marafiki wa chekechea, shule ya msingi,sekondari o level na sekondari a level, kama ulienda chuo pia huko. kusanya majina mengi. jaribu kutafuta magroup pia huko tengeneza marafiki wapya. na uwe mtu wa watu,jishushe, uwe mnyenyekevu. ukitimiza haya. unaweza ishi popote pale bila shida.

Haki zote zimehifadhiwa.
Epuka plagiarism ukichukua andiko hili tambua na juhudi za mwandishi ndugu yangu.
 
Umeandika kwa weledi lakini unatengeneza 'utegemezi' kwa unao washauri kwa namna hiyo hauoni mtu akizoea hayo maisha inakuwa kama ni 'ulemavu' fulani

Ni labda 'solution'ya muda hiyo lakini wewe umeiweka kama 'life style ' ya mtu kwa kipindi kirefu cha maisha yake mkuu

Nafikiri tupeane ushauri wa kupambana ktk njia chanya bila kuja kushusha heshima na hadhi zetu kama binaadam maana hiyo 'life style' ina mwisho
 
hahah asee nimecheka kimoyo moyo sijui kwanini siku hizi nachekeshwa na vitu vya hovyo
 
Haki ya baba kuanzia leo sitaki kutembelewa na marafiki zangu wa shule ya msingi!! Kumbe ndio mbinu zenu hizoooo...
 
Na kweli maisha yamebadilika kwa wengi

Tunaona mengi awamu hii
 
kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusiana na hali mbaya ya kiuchumi na wengi kudai wanakula mlo mmoja kwa siku. wataalam tumekaa chini na kungalia namna ambavyo unaweza survive kwa muda mrefu pasipo kufa kwa njaa. kufa kwa magonjwa au ajali hiyo ni mipango ya muumbaji lakini kwa njaa tena nchini Tanzania ni uzembe wako. Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo wataalamu toka vyuo vikuu mbalimbali vya kitaani wameziainisha. nami mwanaume wa shoka a.k.a gudume nakuletea baada ya kuendesha semina ya miezi sita kujadili mambo haya.

1. hakikisha kwanza unawatafuta marafiki zako woooote wa kuanzia shule ya msingi, shule ya sekondari o-level , sekondari A- level na kama ulifanikiwa pia chuo. kuwa na namba zao au ufahamwa wanapoishi. ni rahisi. ukimpata A atakuelekeza anapoishi B, Ukimpata B atakuelekeza anapoishi C, ukimpata C atakuelekeza D na kuendelea mpaka utakapokuja kumpata Z then utarudi AA atakuelekeza alipo AB, AB atakuelekeza alipo AC na kuendelea.

2. Anzisha kundi la whatsapp au kama lipo tayari jiunge. kuwa mchangiaji na mtu mwenye ukaribu sana na wadau wengine wa humo ndani. anza kusisitiza kuwa kundi liwe la maendeleo na inabidi mkumbukane.

3. panga list ya kuwatembelea watu majumbani kwao. anza maybe na wa shule ya msingi. hakikisha tu una nguo zako nzuri za kutokea. then anza kuwatembelea majumbani kwao kwa chakula cha mchana anza na akina mama au wanawake. asilimia kubwa utakuta wapo nyumbani kwao. mpigie simu mwambie sister nipo mitaa ya huku kwenu nimeona nitumie nafasi hii kuja kuwasalimia akina Uncles. ukienda kwake mida ya saa sita nakuhakikishia siku hiyo chakula cha mchana utapata hapo. kama ni mjanja una story nyingi ukishiba unamwambia aaaah sister..umenimaliza kabisa hapa hata kusimama siwezi sijawah shiba hiv toka nimezaliwa. mwambie ngoja upumzike kidogo mida mida ikienda muulize shemeji huwa anarudi saa ngapi akisema saa moja au saa mbili mwambie ngoja nimsubirie kabisa tufahamiane. unagonga na cha usiku.

4. hapo unaangalie next target atakuwa nani siku ifuatayo. naye jipange kama ulivyofanya leo utakuta umesogeza week au masiku mengi tu ili mradi uwe na uwezo wa kutembea na labda nauli kiasi kama 1000 kwa ajili ya dharura.

5. kama una majirani hakikisha unakuwa karibu sana na majirani zako. ukisikia kuna jirani anaumwa lazima ujue mida mizuri ya kwenda kumsalimia. kama ni mchana nenda kuanzia saa sita na nusu hivi na hakikisha unamsalimia na kukaa kaa naye mpaka saa nane au nane na nusu huo muda lazima chakula cha mchana kitaliwa. ukishakula unakaa kama nusu saa hivi unaaga. lakini kama inabidi kwenda kumuona jioni basi nenda mida ya saa moja na nusu. hapo ukikaa kaa mpaka saa tatu lazima mida ya kula itaangukia humo. piga msosi wako wa kutosha. ili ule chakula kingi hakikisha unamsifia sana jamaa kuwa kweli mke wake anajua kupika. hujawah kula chakula kile toka uzaliwe.huku ukiongeza tena kwa mara nyingine.

6. kama kwa jirani hamna mgonjwa basi msome jirani yako ni mshabiki wa team gani, anapenda chama gani, au kama ni wa dini sana yeye ni msimamo gani.kama ni wadini ifikapo mida ya saa moja moja ukijua amerudi au saa mbili nenda na kitabu husika cha dini. mwambie kuna mistari akufafanulie au nenda na nia ya kupata maombe au neno la mungu. hapo na chakula utakula. mwambie pia una tatizo ambalo unataman ungekuwa unapata maombi kila mara siku hiyo mkiomba kesho rudi mwambie umepata nafuu muombe tena. keshokutwa nenda kamshukuru mida ile ile. siku tatu chakula cha usiku umekula kwake.

7. kama ni mwanamichezo hakikisha una ratiba ya VPL,Laliga,Seri A, Bundesliga na ile ya France na EPL fuatilia sana michezo ikifika mida ya michezo tia team kwake nusu saa kabla. mwambie TV yako imeungua unataka uone Simba jana Kampiga mtu Mkono/ Kofi(magoli 5) au week iliyopita alimpiga mtu week(magoli 7) unataka kuona. hasa goli la mzamiru mwambie ni goli ambalo kuna Morinyo ameliona anataka kulinunua. hapo ni kwa mshabiki wa simba. kama ni wa yanga.... mwambie umesikia habari za tshishimbi...yule jamaa ni balaa...kile kiku kuku kina mpa uwezo mkubwa wa kulisakata gozi na kuonesha mautundu. alitakiwa akacheze mpira mwezini sijui kwa nini alikuja hapa afrika....anza kumpa historia. muda wa kula unakula unaondoka zako.

8. kama ni wa siasa nenda na habari za tundu lissu, nenda na habari za makinikia,magwangala na maboso nenda na habari za magufuli namna anavyowanyoosha wapinzani.ONYO.. unapaswa kujua mwenyeji wako anapendelea nini na yupo kambi gani. hakikisha umesoma sana magazeti na umepitia JF ukapata habari nyingi humu. then nenda kashushe nondo.utafika wakati wakula mtakula utarudi kwako kulala

9. kama ni jamaa mlisoma naye shule kwenye maongezi mkumbushe jinsi alivyokuwa ana akili, mjanja, watu wanamwogopa,wanawake wanampenda au wanaume wanampenda. jinsi ambavyo ulikuwa unataman uwe kama yeye. jinsi ambavyo alikuwa mpole na mstaarabu. kama anapenda sana sifa hapo mkumbushe jinsi ambavyo pia aliwah kuwadunda jamaa flan shuleni,alivyokuwa anawagegeda mademu(kama alikuwa ameshaanza hiyo michezo) huwez kosa la kuzungumzia ikiwa umeamua seriously.

10. jaribu sana kuhudhuria misiba, sherehe n.k uwe update na mambo mbalimbali yanayoendelea mtaani au duniani. ukiweza kuzingatia haya. unaweza jikuta suala la kula halikusumbui sana. hakikisha umepanga ratiba yako vizuri.

ANGALIZO: hakikisha kuwa unavaa vizuri, na usionekane kama ni mtu mwenye shida. pia ukiweza kupata majina hata 250 kuanzia marafiki wa chekechea, shule ya msingi,sekondari o level na sekondari a level, kama ulienda chuo pia huko. kusanya majina mengi. jaribu kutafuta magroup pia huko tengeneza marafiki wapya. na uwe mtu wa watu,jishushe, uwe mnyenyekevu. ukitimiza haya. unaweza ishi popote pale bila shida.

Haki zote zimehifadhiwa.

epuka plagiarism ukichukua andiko hili tambua na juhudi za mwandishi ndugu yangu.
Swali langu. MAISHA HAYO TILL WHEN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom