Mbinu za kupata utajiri wa kudumu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
BILA shaka ukiulizwa leo kama unataka kuwa tajiri, jibu lako litakuwa ni NDIYO! Lakini je, tunaelewa maana ya utajiri na namna ya kuwa tajiri? Hili ni swali ambalo majibu yake yanawasumbua wengi. Mada hii itakusaidia kupata mwanga wa maana na namna ya kuutafuta utajiri.

Wengi wanaamini kuwa ili mtu awe tajiri lazima awe na bahati ya kipekee. Watu wengi hudhani kuwa hawawezi kuwa matajiri mpaka watumie mizizi ya Bagamoyo, Tanga au Sumbawanga. Wengine huamini kwamba ili uwe tajiri, ni lazima uoe au uolewe na tajiri. Zipo imani nyingi juu ya utajiri, wengine wanaamini lazima uwe na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];zali', ufanye biashara ya magendo, ukwepe kodi, uibe, utoe uhai wa mtu au utumie njia nyingine haramu ndiyo uupate utajiri.



SIRI YA UTAJIRI HII HAPA


Siri kubwa ya mtu kuufikia utajiri wa kweli na wa kudumu, ni kuanzisha biashara yenye faida ambayo utakuwa na uwezo wa kuimiliki na siyo biashara ikumiliki wewe. Ukifanikiwa kuanzisha biashara yako, jambo la muhimu kuliko yote ni kuhakikisha unaipangilia ili iweze kujiendesha au kuendeshwa na watu wengine bila wewe kuhusika nayo moja kwa moja lakini kila kitu kiwe chini ya usimamizi na udhibiti wako.

Ukiwa na biashara inayojiendesha yenyewe, utakuwa na uwezo wa kuanzisha biashara nyingine zaidi, yaani ya pili. Hii ya pili ikifikia uwezo wa kujiendesha kama ile ya awali, sasa utakuwa na uwezo wa kufungua biashara ya tatu n.k.

Biashara ni kama mchezo fulani unaosisimua na inatakiwa ufurahie mchezo huo. Hivyo ndivyo wafanyavyo wajasiriamali wakubwa duniani kama akina Salim Bhakhresa na Reginald Mengi kwa hapa Tanzania, Aliko Dangote wa Nigeria, Mukhesh

Dhirubai Ambani wa India, Carlos Slim wa Mexico au Richard Brandson wa Uingereza mwenye makampuni zaidi ya mia tatu.

Jambo la kutia moyo ni kwamba, unaweza kujifunza kufanya hivyo. Kumbuka kuwa hakuna aliyezaliwa anajua kufanya kitu chochote hapa duniani zaidi ya kulia, mara tu tulipozaliwa. Kila tunachokifanya, tumejifunza baada ya kuwa wenyeji hapa duniani. Vivyo vivyo, kila kitu hapa duniani, ukiwa na nia ya kweli, unaweza kujifunza mpaka ukafanikiwa na kuwa mtaalam.

Ni vizuri kufahamu pia kwamba, sio lazima uwe na biashara nyingi ili uwe tajiri. Wapo wajasiriamali wengi mabilionea ambao wanafanya biashara moja tu ambayo utakuta imepanuka na kuwa kubwa katika nchi iliyomo au imefanikiwa kupata masoko mpaka nchi za jirani au hata za mbali.

Lengo la makala haya si kukwambia uwe kama Bill Gates au Warren Buffett (matajiri namna mbili na tatu duniani kwa sasa) au uwe na hela kuliko watu wote barani Afrika au Tanzania, japo hayo yote yanawezekana. Lengo ni kukufundisha namna ya kubuni, kuanzisha, kuendesha na kuipangilia biashara yako mpaka ifike hatua ya kujiendesha yenyewe.

Shauku yangu kama mwandishi wa ujasiriamali ni kukusaidia wewe msomaji kwa kukupa maarifa yatakayokufanya uanze biashara hata bila fedha au kwa mtaji mdogo ili hatimaye uwe na uhuru wa kifedha na muda, uishi upendavyo na usiteseke uzeeni. Nitakufundisha mbinu, mikakati na maarifa ambayo yatakufanya uwe mmiliki hodari wa biashara na mwekezaji mkubwa.


USIKUBALI MTU AKUCHAGULIE KESHO YAKO


Wakati wa uhai wako, kipawa kikubwa kuliko vyote ulivyonavyo ni kipawa cha kufanya uchaguzi wa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo mtindo wa maisha unaotaka kuishi. Baadhi ya mambo mazuri ambayo unaweza kuyafanya unapokuwa na uhuru wa kifedha na muda ni kama vile;
Kusafiri na kuishi kokote ulimwenguni wakati wowote upendapo.
Kujisomesha na kujilipia karo katika chuo chochote popote ulimwenguni.
Kutembelea maajabu mbalimbali ulimwenguni.
Kusoma vitabu vya riwaya, vya maendeleo binafsi au vyovyote uvipendavyo kwa uhuru.
Kutumia muda wako kwa ndugu au marafiki wa muhimu zaidi.
Kwenda kutazama mechi za kimataifa za michezo mbalimbali popote pale ulimwenguni na burudani zingine za aina mbalimbali.
Kujifunza kuimba na kutoa CD yako kwa kuwa una muda na kipato cha kufanya hivyo.
Kuogelea au kujifunza kuogelea na kufurahia uumbaji wa Mungu.
Kuwatembelea wazazi wako mara kwa mara kadiri upendavyo.

Haya na mengine mengi, huwezi kuyafanya kama huna uwezo wa kifedha na muda hivyo ni muhimu kila mmoja akajifunza namna ya kutafuta fedha ili ayafurahie maisha.


Itaendelea baadae
 
MBINU ZA KUPATA UTAJIRI WA KUDUMU-2-

MAFANIKIO YAPO KILA SEHEMU

Wapo wenye dhana kwamba ili ufanikiwe ni lazima ukafanye biashara au kazi nje ya nchi kama Dubai, marekani, Uingereza na sehemu nyingine za Bara la Ulaya. Dhana hiyo ni potofu kwani ukweli kwamba hakuna sehemu ambayo ina fursa nyingi za kukuwezesha kutajirika kwa urahisi kama barani Afrika hususan Tanzania. Hapa kuna kila kitu; watu, malighafi, na fursa za kila aina.

Pia kwa sababu watu wengi sana si wajasiriamali, jambo hilo linakupa fursa ya kuneemeka zaidi. Wajasiriamali wengi waliopo nchini hawaoti ndoto kubwa, kitu kinachomaanisha kuwa kama utaanza kupanga mipango mikubwa, unaweza kuwa mtu wa kushangiliwa na wengine kwa jinsi maisha yako yanavyoweza kuwa bora.

UTAFITI WA KITAALAMU UNASEMAJE?

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Profesa Paul Collier kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani umeonesha kuwa katika makampuni 950 ya Kiafrika yaliyofanikiwa miaka ya hivi karibuni, yalirejesha na kukuza mitaji yake kwa asilimia 11 zaidi ya makampuni ya Amerika ya Kilatino (Latin America) na Asia na makampuni haya ya Kiafrika yamepata faida asilimia 70 zaidi ya makampuni ya Kichina yanayofanana nayo.

Kutokana na utafiti wa Collier, kuna matumaini kuwa wawekezaji wanaowekeza kwenye masoko ya nchi zinazoendelea wanaweza kuanza kuwekeza kwa kasi zaidi hapa Afrika, masoko ya hisa ya Afrika kuondoa lile la Afrika ya Kusini yanakuwa kwa kasi ya ajabu huku yakiongeza

mitaji yake maradufu kutoka dola bilioni 11 3.4 hadi dola bilioni 224.7 ndani ya kipindi cha miaka kumi kuanzia 1992 na 2002.

Ninayasema yote hayo msomaji kukuonyesha jinsi ulivyo na nafasi kubwa ya kufanikiwa hapa Afrika kupitia ujasiriamali.

UKITAKA KUWA MJASIRIAMALI, ANZIA HAPA


Baada ya kueleza hayo machache, bila shaka wengi wanataka kufanikiwa kupitia ujasiriamali lakini huenda watu hawajui maana yake na nini cha kufanya ili kufanikiwa kupitia ujasiriamali.
• Fanya utafiti wa bidhaa au huduma unayotaka kuanza kuitoa kwa kuzingatia maeneo uliyopo, upatikanaji wake na upatikanaji wa wateja. Jiulize, ni maeneo gani ambayo wewe binafsi unadhani unaweza kuwekeza/kuanzisha biashara na baadae kuwa bilionea?
•Jitayarishe vizuri kabla hujaanzisha biashara yeyote. Kamwe usikurupuke hata kama faida inaonekana ni nzuri. Matajiri wakubwa na wawekezaji mahiri huangalia kwanza usalama wa mtaji kabla ya kuangalia faida.
•Jiamini na usiwe na hofu ya kushindwa. Kama wewe ni muumini wa dini yoyote, mwamini Mungu kisha jiamini binafsi. Amini kwamba unachofikiria kukianzisha kitafanikiwa na yashinde mawazo ya kufilisika, kuibiwa au kupoteza fedha. Kwa mjasriamali kujiamini binafsi (self-confidence) ni moja kati ya siri kuu za mafanikio.
•Kamwe usikate tamaa katika maisha yako. Watu wengi, kwa sababu ya kutojua, hukata tamaa wakati wako jirani sana na mafanikio. Usiwe kama

wao, ili kushinda maishani itakupasa uwe king’ang’anizi wa kufuata ndoto zako, na uwe tayari kupambana kwa muda mrefu, wakati mwingine hata kama huoni dalili za kufanikiwa! Hii ndiyo namna mabingwa wote walivyoweza kuwa mabingwa.
Kushindwa ni jambo la kawaida sana maishani kiasi kwamba mtaalamu maarufu wa Uongozi duniani John C. Maxwell ameandika kitabu kizima

‘Failing Forward’ (kushindwa kwa kwenda mbele) akielezea namna ya kusonga mbele bila kukata tamaa hata kama unashindwa mara nyingi.

Bila shaka umesikia habari za Thomas Edson aliyewahi kushindwa mara elfu kumi katika juhudi zake za kutengeneza taa ya umeme. Hakukata tamaa na ndio maana leo tuna taa za umeme.

Itaendelea baadae leo jioni.
 

MziziMkavu usichofahamu hakuna mwanadamu anachoweza kukifanikisha nje ya NENO la Mungu na ndiyo maana katuasa ya kuwa ni Yeye to ndiye anaweza kututajirisha :-


Deuteronomy 8:17-18

"Then you say in your heart, 'My power and might of my hand have gained me this wealth.'

"And you shall remember the LORD your God, for it is HE who gives power to get wealth, that He may establish His covenant which He swore to your fathers, as it is this day."

Jeremiah 27:5

"I have made the earth, the man and the beast that are on the ground, by My great power and by My outstretched arm, and have given it to whom it seemed proper to Me."

Proverbs 10:22

"The blessing of the LORD makes one rich, and He adds no sorrows with it."

tatizo letu huwa ni kufikiri tunaweza kwa jitihada zetu kuwa matajiri na utajiri tunaouthamini ni ule ambao unapita badala ya kuthamini utajiri wa mileel ambao ni busara...........................ya khofu kwa Mungu.
 
Mzizi mkavu umekuwa expert wa biashara tena? Watanzania wana kazi ,wewe unatunga hadithi,wewe mshauri wa biashara aka expert,,haya tueleze mafanikio yako kwanza, mwenzangu hapo juu ameongea ukweli,,
'thou shalt remember the Lord thy God because ,he is who gives thee power to get wealth'
hahhaahhahahahahaahhahaah
 
Last edited by a moderator:
mkuu sina budi nikupongeze kwa kutumia muda wako mwingi kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara humu JF hakika nimeguswa sana na makala yako kwani nimejaribu au nimefanya biashara zaidi ya mara tatu ingawa sikufanikiwa sana lakini nimejifunza vitu vingi sana ambavyo kimsingi ndivyo ulivyoviongelea katika makala yako hakika nakupongeza sana.
 
Mkuu Rutashubanyuma Tusipende

kila kitu kumtupia Mungu. Mungu ametupa akili Mungu ametupa mikono miguu, macho, vidole na kila kitu kinachomfanya bidamu

aweze kuitwa Binadamu tujitahidi kwa akili zetu huku tuna muomba Mungu atusaidie. Sio tu tuende Makanisani na Misikitini tukiomba

eti Mungu atuteremshia chakula kutoka mbinguni haitowezekana. Mungu anasema Jisaidie na huku una niomba nikusaidie nitakusaidia

tu. Wenzetu wazungu wanaendelea sisi Waafrika tupo bado nyuma na mambo ya Uchawi,Kuuwa Maalbino, Kunywa pombe

Uvivu,wizi,Ufisadi, na ujinga na Uzinzi Tutaendelea kweli?Huku kila kitu tunamtupia Mungu? Tutaendelea kweli sisi Waafrika? Tujitahidi

kuvumbuwa kila kitu kinachowezekana huku tukimuomba mungu atusaidie tutafanikiwa ninakuacha hapo kwaleo mkuu.
 
Mbinu za kupata utajiri wa kudumu-3..

Muda ulipita tulijadili kwa kina namna unavyoweza kupata mafanikio katika sekta mbalimbali kama ukiamua kuwa mjasiriamali. Tulifafanua kwa kina nini cha kufanya unapoamua kuwa mjasiriamali. Leo tunaendelea na mada yetu...

NINI CHA KUFANYA BIASHARA YAKO INAPOKWAMA?
Inapotokea umekwama kwa namna yoyote ile katika biashara yako, hutakiwi kukata tamaa bali jiulize maswali yafuatayo:
Umewahi kushindwa mara ngapi katika maisha yako? Nini ulijifunza uliposhindwa, iwe ni kwenye biashara, ajira au mambo yoyote ya kimaisha?
Je, unamfahamu mjasirimali/wajasiriamali gani ambao wamefanikiwa kuliko wewe na unaweza kujifunza kutoka kwao? Hata kama ni maarufu na wako juu sana, panga mpango wa kuonana nao na kuomba ushauri. Usiogope, wengi huwa hawana shida na wanapenda kuwasaidia watu kwa kutoa ushauri ili mradi tu ukiomba kwa heshima na usionyeshe kwamba unataka kuchezea muda wao.
Unafikiri ni jambo gani limesababisha ukakwama katika biashara yako? Ulikosea wapi na nini cha kufanya ili yaliyotokea yasijirudie?
Ukijiuliza maswali haya, bila shaka utaanza kuona kuwa unayo nafasi ya kuinuka kutoka pale ulipokwama na kuendelea na biashara yako.


HATUA TATU MUHIMU
Siri za mafanikio ya biashara siku zote zimekuwa na zitaendelea kuwa rahisi na zimepangwa katika hatua tatu muhimu:
Hatua ya Kwanza: Mtafute mtu wa kumuuzia bidhaa au kutoa huduma.
Hatua ya Pili: Ukipata mteja, hakikisha unamhudumia vizuri ili arudi tena kwako kwa mara nyingine.
Hatua ya Tatu: Hakikisha bidhaa au huduma unayotoa ina ubora wa kumfanya mteja mmoja akawashawishi wenzake kuja kwako.
Watu wengi hawana fedha kwa sababu hawana kitu chochote wanachouza kwa watu wengine. Wengi wetu tunajua zaidi kununua kuliko kuuza hivyo tunatoa fedha nyingi kuliko tunazoingiza. Kama huna kipato cha kutosha, unapaswa kuanza kujiuliza swali hili: Je, unataka kuuza nini? Utamuuzia nani?
Usumbue ubongo wako mpaka ukupe majibu matano, halafu chukua muda kufikiria ni biashara gani unadhani unaweza kuwa unaielewa vizuri na unaweza kuifanya kwa bidii au unaweza kumpata mtu anayeielewa vizuri akusaidie. Ukipata majibu tayari utakuwa umeianza safari ya kuelekea kwenye mafanikio.


MAKUNDI MATANO YA MABILIONEA
Kuna milango mitano ya watu kuwa matajiri wakubwa ambayo mabilionea duniani wanatokea:


1. WATAALAMU WANAOLIPWA VIZURI
Kundi la kwanza ni wanataaluma wanaolipwa vizuri (well paid professionals) kama wanasheria wazuri, madaktari bingwa na wahandisi. Wengi waliofanikiwa katika kundi hili wanajua jinsi ya kuweka akiba na kuwekeza akiba zao kwenye maeneo yenye marejesho mazuri. Mabilionea wanaotokea kundi hili ni asilimi 10 tu ya mabilionea wote.


2. WAKURUGENZI WA MAKAMPUNI MAKUBWA
Kundi lingine la mabilionea ni wakurugenzi wanaolipwa vizuri na makampuni makubwa (well paid executives). Hawa ni asilimia 10 ya mabilionea wote pia. Mara nyingi hawa huwa wametoka na kampuni mbali na wamekua nayo wakipandishwa cheo baada ya cheo mpaka kufikia hatua ya juu. Mara nyingi, watu wachache katika kundi hili huwa na uwezo mkubwa wa kuzishikilia fedha zao na kutozifuja na hiyo huwafikisha kwenye ubilionea.


3. MAAFISA MAUZO
Kundi la tatu ni maafisa mauzo au mameneja wa idara za mauzo. Hawa huwa ni takriban asilimia 5 ya mabilionea wote na kinachowafanya wawe mabilionea ni kwa sababu ya nafasi ya kupata kamisheni kutokana na mauzo wanayoyafanya. Wengi wao huwa ni waajiriwa wa makampuni ambayo wamekuwa wakifanya nayo kazi kwa muda mrefu na kuzifahamu vizuri na baadaye kuja kuwa na milango mingi ya mafanikio.


4. WATU WENYE VIPAJI MAALUM
Kundi la nne ni watu wenye vipaji maalumu kama wanamichezo, wanamuziki, watunzi wa filamu na vitabu na kadhalika. Hawa ni wachache sana 1%, lakini huonekana wengi sana kwa sababu ya kelele zinazoendana na umaarufu wao.


5. WAJASIRIAMALI

Hili ndiyo kundi kubwa kuliko mengine yote, asilimia 74% ya mabilionea wote ni wajasiriamali. Hii inamaanisha kuwa nafasi ya mtu yeyote kuwa bilionea ni kubwa zaidi kupitia ujasiriamali kuliko kitu kingine chochote.

Itaendelea
 
UJASIRIAMALI MBINU ZA KUPATA UTAJIRI WA KUDUMU-4..


UNAWEZA KUACHA KAZI NA KUJIAJIRI

HUENDA wengi wakashtushwa na mada hii lakini ni ukweli usiopingika kuwa kuiajiri ni bora kuliko kuajiriwa. Kama wewe umeajiriwa, unaweza kuacha kazi na kujiajiri mwenyewe. Ni rahisi na kamwe hutajutia uamuzi wako.

Wengine hufananisha suala la kuacha kazi na tukio la kuruka kwenye dirisha la ndege ukiwa na parachuti ukitegemea kama litafunguka ili utue salama. Kama utajiandaa vyema, utakuwa sawasawa na mtu ambaye ameelekezwa vizuri namna ya kutumia parachute na amejiandaa barabara kiakili na kihisia.

Utafiti unaonyesha kuwa katika kila biashara zinazoanzishwa, asilimia 95 huanguka ndani ya miaka mitano na 5% huendelea. Lakini baada ya hapo asilimia 95% ya biashara ya asilimia hii huanguka ndani ya miaka 5 ifuatayo. Kwa nini kiwango cha biashara kuanguka ni kikubwa hivi? Kwa nini watu wengi huwa wanafilisika? Zifuatazo ni baadhi ya sababu:

1. Mjasiriamali kukosa uzoefu wa biashara
2. Mjasiriamali kukosa ujuzi na maarifa ya masoko
3. Kukosa nidhamu ya pesa
4. Kukosa mtaji
5. Mauzo kuwa chini
6. Kushindwa kuendana na baadhi ya wafanyakazi wake
7. Kuchukua mkopo mwingi bila matumizi sahihi
8. Kukosa stadi za mafanikio katika ujasiriamali
9. Kukosa msukumo binafsi wa kufanya mambo sahihi
10. Kujaribu kufanya biashara nyingi sana au mambo mengi ambayo yote yanahitaji muda na umakini (lack of focus)
11. Kukosa ndoto na shauku ya kufanikiwa
12. Magonjwa na afya mbovu
13. Tabia ya kuahirisha mambo mra kwa mara
14. Kukata tamaa kwa urahisi mambo yanapoonekana magumu
15. Mtazamo hasi (negative mental attitude)
16. Hali ya kutaka kitu bila kitu.
17. Marafiki au washirika wasio sahihi katika biashara yako (mkeo au mumeo aweza kuwa kikwazo)
18. Hofu na kutokuthubu
19. Kushindwa kufikiri kwa makini na kupenda kukisia mara kwa mara.

NATAKA KUACHA KAZI, NIFANYE BIASHARA GANI?

Mara nyingi hilo ndio swali ambalo huwa ninaulizwa sana. Watu hunipigia simu wakisema kuwa wamenisikia

kwenye vipindi vyangu vya ujasiriamali (huwa naendesha vipindi vya redio vya ujasiriamali) na hivyo huomba ushauri wa waanze vipi na wafanye biashara gani
Hilo ndiyo swali la muhimu sana kwa mtu anayetaka kuwa mjasiriamali na linaweza kumsaidia mtu kupata majibu sahihi ya kitu atakachokifanya na kumletea mafanikio maishani.

Watu wengi wakiulizwa ni biashara gani inaweza kukupatia fedha kwa urahisi, hujibu kwa kuangalia watu waliofanikiwa kupitia biashara mbalimbali na kuzitaja biashara hizo kama ndiyo zina faida kubwa. Ukweli ni

kwamba biashara yeyote inaweza kufanikiwa ikiwa itapata wateja wengi wakutosha. Hivyo suala la msingi, sio biashara gani ya muhimu, bali ni vigezo gani vya msingi.
KABLA HUJAACHA KAZI ZINGATIA YAFUATAYO:

• Chunguza siri za biashara zinazofanikiwa na mifumo iliyopo nyuma yake. Jaribu kuziangalia biashara za Wahindi na Waarabu zinazofanywa. Watu wengi huwa na wazo la bidhaa ya kuuza au hata kutengeneza kama vile mshumaa, rangi, shampoo nk lakini mara nyingi huwa hawana ujuzi wa kutengeneza mfumo mzuri wa uletaji wa faida.

• Pata mlezi au mshauri (Mentor) atakayekusaidia katika safari ya ujasiriamali. Neno mentor linamaanisha mtu ambaye amefanikiwa kwenye jambo fulani na ana uwezo wa kuwasaidia/kuwaelekeza watu wengine wafanikiwe kama yeye.

• Fanya kazi kwenye biashara ya mtu aliyefanikiwa na ambaye unataka kuja kuwa kama yeye. Wakati mwingine, njia ya mkato ya kujifunza biashara ni kukubali kutumika chini ya mtu mwingine ili ujionee moja kwa moja uendeshaji wa biashara kabla hujaamua kuingia moja kwa moja.

• Jenga tabia ya kuwauliza maswali ya msingi wajasiriamali waliofanikiwa. Kila unapopata nafasi ya kuwa na mtu tajiri, jipe moyo mara kwa mara halafu uliza swali hili: “Je siri ya mafanikio yako ni nini?”Utashangaa jinsi ambavyo watu wengi si wachoyo wa siri zao za mafanikio ili mradi tu uulize katika mazingira mazuri yenye heshima na hekima.

5. Jijengee uwezo wa kuuza. Uwezo wa kuwashawishi watu waweze kununua bidhaa yako au kutumia huduma yako ndiyo uweze kusimama katika ujasiriamali.
 
Naendelea kujifunza kwa kuwa ninafanya biashara, tena nimechukua mkopo benki (mimi ni mtumishi wa serikali).
Japo nimefungua biashara mbili, sijaanza ona mafanikio (huu ni mwezi wa tisa sasa), lakini kupitia post kama hizi, naamini siku moja nitakuja kusimulia ushuhuda wa mambo ya kijasiria.
Kwa kweli kuna kipindi hali inakatisha tamaa, hasa nikilinganisha salary slips za kipindi hiki nilichochukua mkopo na kabla. Ila najipa matumaini kuwa kushindwa ni kujifunza, kwani always akili yangu inafocus mafanikio, na inakuwa active.
 
Maalim MziziMkavu, umekuja wakati muafaka kwani mwaka huu nimepangilia kuaga sector ya kuajiriwa na kuelekea kujiajiri, hii ni baada tu yakufanya utafiti mdogo na nikagundua Rais Obama amabaye analitumikia taifa kubwa kiuchumi duniani ana mshahara wa take home usiofikia hata nusu ya pato la mjasiriamali Tony Ferdnandes, Mmiliki wa low cost carrier maarufu sana Air Asia, na mmiliki wa klabu ya soccer QPR.
 

Mkuu Safi sana, Pamoja sana, ni uamuzi mzuri kabisa, na huko kwa Obama ni Mbali sana mifano ni huku huku Bongo, Ni maamuzi yanayo weza fanywa na watu wachache sana, Tunaita KUCHOMA MELI MOTO
 

Mkuu hautakiwi kukata tamaa kwani Mara nyingi watu hukata tamaa bila kujua ni kiasi gani ilikuwa imebakia wafanikiwe, Kilichopo ni kuhakikisha unatibu Magonjwa yote yanayo sababisha biashara zako zisiende mbele zaidi, Ila Bado muda wa kuafnikiwa upo kwa sbabau kwa Mjasirimali mara zote mwanzo huwa mgumu sana na ukisoma Story za waliofanikiwa wengi wao mwanzo ulikuwa ni mugumu sana

 

mashaallah,Mungu akubariki kaka Mzizimkavu
 
Mkuu Safi sana, Pamoja sana, ni uamuzi mzuri kabisa, na huko kwa Obama ni Mbali sana mifano ni huku huku Bongo, Ni maamuzi yanayo weza fanywa na watu wachache sana, Tunaita KUCHOMA MELI MOTO

Konda na dereva wa daladala hata wa bodaboda wanauwakika wa kupeleka nyumbani is chini ya 30 Elfu kwa siku, kwa mwezi ni 900,000. Hii. Watu wengu walio ajiriwa hata wakiweka na posho hawafiki take home hiyo.
 

MziziMkavu hata kuchukia uvivu na tabia mbaya ni lazima akuongoze.....................ukiwaangalia maskini wanaomba barabarani utafikiri ya kuwa wamejitakia/........................lakini ni busara za Muumba ndizo zimewaweka pale.............ili awapime wale aliowapa vipaji kama kweli wanamwogopa Mungu kwa kuwasaidia wenye uwezo mdogo..........
 
Hahahahaha hapo unazidi kudanganya watu,,kwanza ni copy and paste,,pili hakuna katika biblia sehemu ilipoandikwa jisaidie nami ntakusaidia,ukiipata hiyo sehemu ntakupatia 10000 ya muda wa maongezi,neno linasema nisogelee nami ntakusogelea,,,
kuandika hicho kitu sio kwamba unajua kila kitu MziziMkavu na hata mtu akisoma akienda kujaribu anaweza asifanikiwe coz kama biashara ingekuwa inaangalia unayoyaandika basi hata wewe sa hv ungekuwa tajiri mkubwa wa kupindukia.




 
Last edited by a moderator:
Utabakia hivyohivyo. Shame on you

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…