Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
MBINU ZA BIASHARA
JIBU LA KWA NINI WATU WENGINE NI MASIKINI NA WENGINE NI MATAJIRI
Watu wengi wanajiuliza, "Siri ya utajiri ni nini?" Jee ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila
wanayo wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate manufaa ,nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biashara yako ili iwe indelevu.
Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs
1,000 kila siku sawasawa na TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka
itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine
njia hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.
Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama za likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto wako iwapo utawaanzishia hivi mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama upanga wa siku zijazo kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila kusudio lako la baadaye.
Hebu tuangalie njia ya pili.
- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga asilimia 10% ya
mapato yako hadi utakapofikia lengo la TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs 10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapata TShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na
kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs. 63,112,201.43.
Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye kitegauchumi chenye kutoa
faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank" inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika soko la hisa na mitaji.
Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi (10%).
Baada ya kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia zingine ambazo zinaweza kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni njia ya kubahatisha kwani watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto wenye bahati kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo mazuri na kujiajiri mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama ya Uanasheria, Uhasibu na Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendesha ili kupata ziada kubwa.
4. Unaweza kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au msanii wa kulipwa.
5. Unaweza kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa mfano, kama wewe ni mtu uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza kutunga kitabu kinachofundisha watu namna ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi wa vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni kazi unayoweza kuifanya mara moja lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu sana.
6. Unaweza kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia chombo ulichokibuni kukuingizia fedha.
7. Unaweza kucheza bahati nasibu na kushinda. Tatizo hapa soko na wateja wa aina hii ya huduma ni haba. Hiki ni kitu cha kubahatisha na nimekitaja makusudi ili kuwapa onyo wasomaji kwani watu wengi wanapenda sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana. Hivyo, nawashauri wasomaji kuachana na njia hii ya kutafuta utajiri. Nawashauri wachague njia yoyote inayofaa na inawezekana kwa kufuatana na mazingira
yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au mfugaji anaweza kuzingatia fani hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna mipaka, hasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za kuweza kujishughulisha na kuwa tajiri.
Inawezekana kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana na kile tulichojifunza kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini huwaambia watoto wao wajitahidi kusoma sana ili wapate maksi nzuri darasani na ili baadaye waweze kupata kazi nzuri. Wakati wazazi matajiri huwapa watoto wao elimu ya
namna ya kutafuta fedha. Kwa kawaida tukiwa shuleni tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha tunatakiwa kuwa na ripoti yetu ya maisha nayo ni orodha ya mali tulizonazo ikiwa ni pamoja na elimu ya
kuzaliwa na ya kusomea na fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi mbalimbali.
Kwa kufuata tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye kipato chake hakizidi TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao humfanya kutumia kipato chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada wala uwezo wa kuweka akiba hana madeni na hana mali.
Mfumo wa fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya kuwa na mali kama magari,
nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo huwa zinapatikana kwa mikopo na hutumia mshahara kulipia matumizi na madeni, hasa kama madeni ni makubwa, mtu mwenye kipato cha kati anapaswa kumuona mshauri wa maswala ya biashara. Hatua anazoweza kuchukua ili kujikwamua na tatizo la madeni anaweza
kulazimika kuuza baadhi ya mali zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari tu na ambazo hazina umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya kutembelea, anaweza kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na fedha atakayoiokoa kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato.
Mfumo wa mtu tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara yake, kumiliki mali nyingi, kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe ameziwekeza kwenye vitega uchumi vinavyolipa faida kubwa zaidi ya asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha na hisa. Mtu huyu hana wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini vitegauchumi vyake vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya matajiri ni uwezo wa kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.
Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie kazi ili yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika kuchukua hatua. Tajiri hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua hatua kwa kutekeleza kwa vitendo
yale anayojifunza na anayoyaona yanaweza kumuinua kiuchumi. Maskini huwa anajifunza mambo na kuyaacha kichwani bila kuchukua hatua au kuyafanyia kazi aliyojifunza na hivyo fursa ya kupata utajiri inampita hivihivi. Kwa hiyo, kama unataka kuwa tajiri anza mara moja kufanya yafuatayo:-
1. Anza kuweka akiba ya T.Shs 1,000 kila siku. Tengeneza kisanduku na tumbukiza TShs. 1,000 kila siku. Zikifika TShs. 50,000 kafungue akaunti ya TAJIRIKA, kwenye Benki ya "Standard Chatered". Kisha endelea
kuweka TShs. 30,000 kila mwezi. Jinsi mapato yako yatakavyokuwa yanaongezeka tenga asilimia kumi (10%) ya mapato yako uweke akiba kila mwezi. Lengo lako liwe ni kuweka TShs 10,000 au zaidi kila mwezi. Fedha unayoweka ni kama unapanda mbegu. Kumbuka hii ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye
utajiri. Faida katika benki hii ni kubwa. Inaanzia asilimia 6.5% kwa kianzio cha TShs. 50,000 hadi TShs. 5,000,000 na asilimia 10% kwa kiwango kinachozidi TShs. 10,000,000. Fedha utakazoziweka huko
usiziguse mpaka ukiona zimekuwa nyingi ndipo utaamua na kupanga ukaziwekeze sehemu gani.
2. Jifunze pia mbinu za kutafuta fedha. Njia rahisi ni ya uhakika ya kukuwezesha kufanikiwa kiuchumi katika maisha ni kutafuta mshauri au mtaalamu anayejua mbinu za uongozi wa biashara ili akushauri vizuri juu ya yale unayonuia kutekeleza.
3. Inawezekana pia bado hujawa na biashara ya aina yoyote. Kama ndivyo anza kufanya utafiti kuona utafanya biashara gani. Mawazo ya biashara gani ufanye unaweza kuyapata katika sehemu ya pili ya
kitabu hiki. Kila mara hakikisha unatenga asilimia 10% ya mapato yako na kuweka kwenye akaunti yako ya TAJIRIKA. Kumbuka kwamba kuwa na biashara yako ni siri ya pili ya kuelekea kwenye kupata utajiri.
Kama unayo biashara yako unaweza kumtafuta mtaalamu wa biashara kuangalia jinsi unavyoweza kuiboresha au kuipanua.
4. Panga malengo ya muda wa mwaka mmoja miaka mitano na miaka ishirini ili kuhakikisha kwamba unajikomboa kiuchumi. Malengo yako makuu yawe ni:- kuwa na akiba ya fedha za kutosha katika akaunti yako , kuwa na biashara yako, na vitega uchumi vya aina tofauti ambavyo unaweza kuvisimamia vizuri.
5. Kama wewe ni mwajiriwa, kipimo chako cha mafanikio kiwe ni kujiuliza swali, kama utaacha kazi yako ya mshahara utaweza kuishi kwa kutumia kipato chako cha pembeni kwenye biashara yako kwa muda gani? Mafanikio yako yatakuja pale utakapoweza kutumia kipato chako cha ziada bila kutegemea
mshahara, na hapo ndipo unaweza kuacha kazi na kwenda kuimarisha biashara zako au kuendelea na kazi huku pia ukijiimarisha kibiashara.
6. Kama utafuata mpango wa namna hii na kujituma kwa juhudi na maarifa kwa muda wa miaka mitano
(5) unaweza kuwa tajiri na maisha yako yanaweza kuwa mazuri.
CREDIT: CHARGE YOUR BRAIN@FB
WAKO MCHUMI FARAJA MMASA
*************TAFUTA MAFANIKIO KAMA UTAISHI MILELE LAKINI MWABUDU NA KUMTUMIKIA MUNGU WAKO KAMA LEO NDIO SIKU YAKO YA MWISHO KUWA KATIKA DUNIA HII**********************************FARAJA MMASA BLOG: MBINU ZA BIASHARA
hongera kwakemkuu sina budi nikupongeze kwa kutumia muda wako mwingi kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara humu JF hakika nimeguswa sana na makala yako kwani nimejaribu au nimefanya biashara zaidi ya mara tatu ingawa sikufanikiwa sana lakini nimejifunza vitu vingi sana ambavyo kimsingi ndivyo ulivyoviongelea katika makala yako hakika nakupongeza sana.
Usikatishe aisee endeleaBILA shaka ukiulizwa leo kama unataka kuwa tajiri, jibu lako litakuwa ni NDIYO! Lakini je, tunaelewa maana ya utajiri na namna ya kuwa tajiri? Hili ni swali ambalo majibu yake yanawasumbua wengi. Mada hii itakusaidia kupata mwanga wa maana na namna ya kuutafuta utajiri.
Wengi wanaamini kuwa ili mtu awe tajiri lazima awe na bahati ya kipekee. Watu wengi hudhani kuwa hawawezi kuwa matajiri mpaka watumie mizizi ya Bagamoyo, Tanga au Sumbawanga. Wengine huamini kwamba ili uwe tajiri, ni lazima uoe au uolewe na tajiri. Zipo imani nyingi juu ya utajiri, wengine wanaamini lazima uwe na &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];zali', ufanye biashara ya magendo, ukwepe kodi, uibe, utoe uhai wa mtu au utumie njia nyingine haramu ndiyo uupate utajiri.
SIRI YA UTAJIRI HII HAPA
Siri kubwa ya mtu kuufikia utajiri wa kweli na wa kudumu, ni kuanzisha biashara yenye faida ambayo utakuwa na uwezo wa kuimiliki na siyo biashara ikumiliki wewe. Ukifanikiwa kuanzisha biashara yako, jambo la muhimu kuliko yote ni kuhakikisha unaipangilia ili iweze kujiendesha au kuendeshwa na watu wengine bila wewe kuhusika nayo moja kwa moja lakini kila kitu kiwe chini ya usimamizi na udhibiti wako.
Ukiwa na biashara inayojiendesha yenyewe, utakuwa na uwezo wa kuanzisha biashara nyingine zaidi, yaani ya pili. Hii ya pili ikifikia uwezo wa kujiendesha kama ile ya awali, sasa utakuwa na uwezo wa kufungua biashara ya tatu n.k.
Biashara ni kama mchezo fulani unaosisimua na inatakiwa ufurahie mchezo huo. Hivyo ndivyo wafanyavyo wajasiriamali wakubwa duniani kama akina Salim Bhakhresa na Reginald Mengi kwa hapa Tanzania, Aliko Dangote wa Nigeria, Mukhesh
Dhirubai Ambani wa India, Carlos Slim wa Mexico au Richard Brandson wa Uingereza mwenye makampuni zaidi ya mia tatu.
Jambo la kutia moyo ni kwamba, unaweza kujifunza kufanya hivyo. Kumbuka kuwa hakuna aliyezaliwa anajua kufanya kitu chochote hapa duniani zaidi ya kulia, mara tu tulipozaliwa. Kila tunachokifanya, tumejifunza baada ya kuwa wenyeji hapa duniani. Vivyo vivyo, kila kitu hapa duniani, ukiwa na nia ya kweli, unaweza kujifunza mpaka ukafanikiwa na kuwa mtaalam.
Ni vizuri kufahamu pia kwamba, sio lazima uwe na biashara nyingi ili uwe tajiri. Wapo wajasiriamali wengi mabilionea ambao wanafanya biashara moja tu ambayo utakuta imepanuka na kuwa kubwa katika nchi iliyomo au imefanikiwa kupata masoko mpaka nchi za jirani au hata za mbali.
Lengo la makala haya si kukwambia uwe kama Bill Gates au Warren Buffett (matajiri namna mbili na tatu duniani kwa sasa) au uwe na hela kuliko watu wote barani Afrika au Tanzania, japo hayo yote yanawezekana. Lengo ni kukufundisha namna ya kubuni, kuanzisha, kuendesha na kuipangilia biashara yako mpaka ifike hatua ya kujiendesha yenyewe.
Shauku yangu kama mwandishi wa ujasiriamali ni kukusaidia wewe msomaji kwa kukupa maarifa yatakayokufanya uanze biashara hata bila fedha au kwa mtaji mdogo ili hatimaye uwe na uhuru wa kifedha na muda, uishi upendavyo na usiteseke uzeeni. Nitakufundisha mbinu, mikakati na maarifa ambayo yatakufanya uwe mmiliki hodari wa biashara na mwekezaji mkubwa.
USIKUBALI MTU AKUCHAGULIE KESHO YAKO
Wakati wa uhai wako, kipawa kikubwa kuliko vyote ulivyonavyo ni kipawa cha kufanya uchaguzi wa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo mtindo wa maisha unaotaka kuishi. Baadhi ya mambo mazuri ambayo unaweza kuyafanya unapokuwa na uhuru wa kifedha na muda ni kama vile;
Kusafiri na kuishi kokote ulimwenguni wakati wowote upendapo.
Kujisomesha na kujilipia karo katika chuo chochote popote ulimwenguni.
Kutembelea maajabu mbalimbali ulimwenguni.
Kusoma vitabu vya riwaya, vya maendeleo binafsi au vyovyote uvipendavyo kwa uhuru.
Kutumia muda wako kwa ndugu au marafiki wa muhimu zaidi.
Kwenda kutazama mechi za kimataifa za michezo mbalimbali popote pale ulimwenguni na burudani zingine za aina mbalimbali.
Kujifunza kuimba na kutoa CD yako kwa kuwa una muda na kipato cha kufanya hivyo.
Kuogelea au kujifunza kuogelea na kufurahia uumbaji wa Mungu.
Kuwatembelea wazazi wako mara kwa mara kadiri upendavyo.
Haya na mengine mengi, huwezi kuyafanya kama huna uwezo wa kifedha na muda hivyo ni muhimu kila mmoja akajifunza namna ya kutafuta fedha ili ayafurahie maisha.
Itaendelea baadae
Jioni imeshafika lianzishe tena kiongoziMBINU ZA KUPATA UTAJIRI WA KUDUMU-2-
MAFANIKIO YAPO KILA SEHEMU
Wapo wenye dhana kwamba ili ufanikiwe ni lazima ukafanye biashara au kazi nje ya nchi kama Dubai, marekani, Uingereza na sehemu nyingine za Bara la Ulaya. Dhana hiyo ni potofu kwani ukweli kwamba hakuna sehemu ambayo ina fursa nyingi za kukuwezesha kutajirika kwa urahisi kama barani Afrika hususan Tanzania. Hapa kuna kila kitu; watu, malighafi, na fursa za kila aina.
Pia kwa sababu watu wengi sana si wajasiriamali, jambo hilo linakupa fursa ya kuneemeka zaidi. Wajasiriamali wengi waliopo nchini hawaoti ndoto kubwa, kitu kinachomaanisha kuwa kama utaanza kupanga mipango mikubwa, unaweza kuwa mtu wa kushangiliwa na wengine kwa jinsi maisha yako yanavyoweza kuwa bora.
UTAFITI WA KITAALAMU UNASEMAJE?
Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Profesa Paul Collier kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani umeonesha kuwa katika makampuni 950 ya Kiafrika yaliyofanikiwa miaka ya hivi karibuni, yalirejesha na kukuza mitaji yake kwa asilimia 11 zaidi ya makampuni ya Amerika ya Kilatino (Latin America) na Asia na makampuni haya ya Kiafrika yamepata faida asilimia 70 zaidi ya makampuni ya Kichina yanayofanana nayo.
Kutokana na utafiti wa Collier, kuna matumaini kuwa wawekezaji wanaowekeza kwenye masoko ya nchi zinazoendelea wanaweza kuanza kuwekeza kwa kasi zaidi hapa Afrika, masoko ya hisa ya Afrika kuondoa lile la Afrika ya Kusini yanakuwa kwa kasi ya ajabu huku yakiongeza
mitaji yake maradufu kutoka dola bilioni 11 3.4 hadi dola bilioni 224.7 ndani ya kipindi cha miaka kumi kuanzia 1992 na 2002.
Ninayasema yote hayo msomaji kukuonyesha jinsi ulivyo na nafasi kubwa ya kufanikiwa hapa Afrika kupitia ujasiriamali.
UKITAKA KUWA MJASIRIAMALI, ANZIA HAPA
Baada ya kueleza hayo machache, bila shaka wengi wanataka kufanikiwa kupitia ujasiriamali lakini huenda watu hawajui maana yake na nini cha kufanya ili kufanikiwa kupitia ujasiriamali.
Fanya utafiti wa bidhaa au huduma unayotaka kuanza kuitoa kwa kuzingatia maeneo uliyopo, upatikanaji wake na upatikanaji wa wateja. Jiulize, ni maeneo gani ambayo wewe binafsi unadhani unaweza kuwekeza/kuanzisha biashara na baadae kuwa bilionea?
Jitayarishe vizuri kabla hujaanzisha biashara yeyote. Kamwe usikurupuke hata kama faida inaonekana ni nzuri. Matajiri wakubwa na wawekezaji mahiri huangalia kwanza usalama wa mtaji kabla ya kuangalia faida.
Jiamini na usiwe na hofu ya kushindwa. Kama wewe ni muumini wa dini yoyote, mwamini Mungu kisha jiamini binafsi. Amini kwamba unachofikiria kukianzisha kitafanikiwa na yashinde mawazo ya kufilisika, kuibiwa au kupoteza fedha. Kwa mjasriamali kujiamini binafsi (self-confidence) ni moja kati ya siri kuu za mafanikio.
Kamwe usikate tamaa katika maisha yako. Watu wengi, kwa sababu ya kutojua, hukata tamaa wakati wako jirani sana na mafanikio. Usiwe kama
wao, ili kushinda maishani itakupasa uwe kinganganizi wa kufuata ndoto zako, na uwe tayari kupambana kwa muda mrefu, wakati mwingine hata kama huoni dalili za kufanikiwa! Hii ndiyo namna mabingwa wote walivyoweza kuwa mabingwa.
Kushindwa ni jambo la kawaida sana maishani kiasi kwamba mtaalamu maarufu wa Uongozi duniani John C. Maxwell ameandika kitabu kizima
Failing Forward (kushindwa kwa kwenda mbele) akielezea namna ya kusonga mbele bila kukata tamaa hata kama unashindwa mara nyingi.
Bila shaka umesikia habari za Thomas Edson aliyewahi kushindwa mara elfu kumi katika juhudi zake za kutengeneza taa ya umeme. Hakukata tamaa na ndio maana leo tuna taa za umeme.
Itaendelea baadae leo jioni.