Mbinu za 'T.M.K' ninazotumia kupiga hela kipindi hiki( "kigumu" )

The List

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2017
Posts
1,732
Reaction score
4,924
Salaam Wakuu,

Ni dhahir shair bila chembe ya kumung'unya kuwa uchumi umedorora, biashara zinafungwa na hali ya uchumi imekuwa ngumu kuitabiri

Sabab mjasiriamali sio mwanasiasa ayo mengine tunawaachia wao. Upande wa pili kazi yetu ni kutizama ni namna gani tunaokoa biashara zetu, tunajua wote kila nyakati aidha iwe nzuri au mbaya ni nafasi ya kutengeneza pesa, mtizamo wako ndio kila kitu, Mentor wng husema 'weather the glass is half full or half empty, it all depends on your percetion'

Sasa binafsi baada ya hali kuwa ilivo hivi, nilikuja na kampango mkakati kuona ni namna gani nitaokoa/kuzivusha biashara zangu lakin nikaendelea kupiga hela . Na baada yakuanza kuzitumia mbinu za T.M.K nathubutu kusema vyuma viendelee kukazwa ivoivo.

Wakati watu wanabana matumizi, mjasiriamali lazima uangalie namna ambazo zitakuwezesha ku-maintain lifestyl ako na vyanzo vya mapato. Kumbuka ktk biashara kuchukua hatua au kutochukua hatua yote ni maamuzi, yaani ukikubar kuendelea kulia tu kwmb hali ni mbovu basi jua utakua kundi la 'mwafaa' tehtehteh

Oke nisikunyweshe kahawa nyingi, ngoja nikupe nawe THE LIST ya mbinu chokozi ili kulingana na aina ya biashara zako aidha utaboresha au kupaste kulingana na uhitaji na chanagamoto ya biashara husika

Toroka uje, haka ka mbinu nikakuongeza wateja wapya pia kufanya biashara ifahamike. Apa utahitaji moyo mgumu kidogo maana itakubid ubaki na bei ya zamani wenzako wakiongeza au ushushe kidogo. Tehtehteh apo patamu, oke bei ya vitu imepanda na hivo pia wafanyabiashara wengi wameongeza bei ya bidhaa zao. Ni sawa sote tunaangalia faida, lakini kwenye biashara lazima uwe na malengo marefu na biashara yako zaid ya pesa tu refer uzi wng wa 'uzushi na upotoshaji kuhusu ujasiriamali'

Kufakufaana, apa wakuu ni kwamb kilio chako ni furaha ya mwingine, iko hiv kipind kama hiki sio lazima wote tulie njaa sasa kuna biashara ya mtu ilikuwa inafanya vizur lakin ktk wakat huu mwenzio katikiswa kidogo anataka kukimbia, unachokifanya uza biashara yako uliyoichoka na ununue ya jamaa. Maana kama umejiridhisha na biashara iyo na mapungufu unayajua basi ni nafas nzuri kwako kutoboa.

Tumbua vijipu, apa nina maana kuna watu ktk biashara ako wanaofanya kazi zisizo za lazima sana kiviiile. Yaani zilikuwepo kama nyongeza au kivutio fulani. Hao ni vijipu na pengine ungewapunguza basi ungeokoa vijisent kadhaa ata vya kulipia bili ya umeme. Makampuni makubwa dunian kote hufanya hivo,T.B.L na Airtel ni mifano tu kwa apa kwetu.. sembuse ww mwenzang na mm na kigenge chako.

Mgeni Njoo Mwenyeji Apone, iko hivi mfanyakazi mfano ulikuwa ukimlipa elfu 10 kwa siku ukimpunguzia ata buku unavunja morali ake. Lakini ukileta mpya na ukawa unamlipa elfu 7000 ata ridhia tu sabab hana namna. Apa lazima uangalie umuhimu wa mfanyakazi na ujuzi wake, ningeshauri angalia wale viburi au aliyekuwa na chokochoko, huu ni wakat muafaka wa kutengua ndoa nae.

ANGALIZO; chochote utakachofanya usipunguze kipimo au thamani ya huduma au bidhaa yako.

Pia mbinu hizo si lazima ziwe applicable kwenye biashara yako lakini pengine zinaweza kukupa mwanga kuona ni namna gani utakavozi manipulate ili ziendane na matakwa ya biashara yako.

Mwisho niseme tu guarantee ya kufanya vizuri ni kubwa sabab matunda ake nayaona.

NA VIENDELEE KUKAZA
 
Napitia sana sema sijawepo jukwaani kwa muda kidogo.hongera thread zako zote ni elimu kwangu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…