Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kupitia vyanzo vyangu vya uhakika, naweka hapa namna CCM inavyoingilia kuchafua zoezi la uandikishaji daftari la Wakazi watakaopiga kura hapo Novemba 2024 kuwachagua viongozi wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Tujulishe hapa endapo kuna mbinu inqyotumika eneo lako kuchafua zoezi la uandikishaji
- Baada ya kuumbuliwa kwa kuwaandikisha wanafunzi ambao hata umri wa kupiga kura hawajafikia, sasa waalimu wakuu wa shule wameelekezwa kuwasilisha majina ya wanafunzi waliomaliza shule hizo na yanaingizwa kwenye daftari la wakazi.
- Kambi za miradi ya ujenzi ambazo zipo chini ya Wachina, zimekuwa zinatembelewa kipindi hiki na watendaji wa mitaa na vijiji kufanya uandikishaji wa vibarua na wafanyakazi Watanzania ndani ya kambi hizo... zoezi hili linafanywa kwa usiri mkubwa.
- Waandikishaji wanapewa roaster ya majina kutoka viongozi wa CCM na yanaingizwa kwenye daftari la wakazi. Wajumbe wa mashina wqmeandaliwa kuwatambua hao watu wasiojulikana ndani ya maeneo yao
Tujulishe hapa endapo kuna mbinu inqyotumika eneo lako kuchafua zoezi la uandikishaji