Quartz360
Senior Member
- Mar 27, 2023
- 133
- 317
Bima ya afya ni nyenzo muhimu inayomweesha mtu kuweza kupata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya kama vile zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, mikoa na kadhalika. Bima za afya huweza kuokoa maisha ya watu wengi sana duniani, kwa sababu ugonjwa huweza kutokea mda wowote ule bila hata maandalizi, hivyo uwepo wa bima humsaidia mtu kupata huduma hasa kipindi cha ugonjwa na pale hali yake ya kiuchumi inapokuwa haiko vizuri.
Mnamo mwaka 2021, wizara ya afya ilitoa ripoti iliyoonesha kuwa ni asilimia 15% tu ya watanzania walikuwa na bima ya afya, hii si ishara nzuri kama taifa hasa tunapoelekea kwenye kipindi cha kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kama vile mpamgo mkakati wa sekta ya afya wa mwaka 2021-2026 unavyosema (Health Sector Strategic Plan V 2021-2026).
MBINU ZINAZOWEZA KUTUMIKA KUHAKIKISHA KILA MTU ANA BIMA YA AFYA
1. Serikali kupitia wizara ya afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waandae mikakati maaalumu ya utoaji wa elimu kwa jamii. Watu wengi wanaona bima ya afya haina umuhimu kwa sababu ya kukosa elimu sahihi juu ya faida za bima ya afya, kuandaliwe programu maalumu kwenye kila kijiji itakayosimamiwa na kituo cha afya katika eneo husika, programu hii ya utoaji elimu iendane na utoaji wa vipeperushi juu ya masuala ya bima ya afya, vilevile kwenye kila shule ya msingi na sekondari kuanzishwe vikundi maalumu (HEALTH INSURANCE CLUBS) vyenye lengo la kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia bima ya afya, pia katika mikutano yote ya vijiji ihusishe pia wataalamu wa afya wataokwenda kusisitiza matumizi ya bima ya afya kwa umma.
2. Kuanzishwe mfumo wa kuchangia bima kupitia simu za mkononi. Badala ya kuwaambia watu walipe kiasi flani cha pesa kwa wakati mmoja, ni vyema kuwepo na akaunti maalumu za bima kwenye simu za mikononi zitakazowasaidia watu kuchangia kidogo kidogo kwa mda maalumu na pale kiasi kinapotimia mara moja mchangiaji aweze kukatiwa bima yake. Mfumo huu wa uchangiaji kupitia simu za mkononi uwe ni kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa, Halo Pesa, Airtel Money, Azam Pesa na hata njia ya kibenki iwape uhuru watu kuchangia kiasi flani (kidogo kidogo) kulingana na vipato vyao, kwa kutumia njia hii mtu anapofungua akaunti ya bima na kuanza kuchangia kidogo kidogo itampa hamasa ya kuweza kukamilisha malipo yake ya bima ndani ya mda rafiki na hivyo kumsaidia kupata bima yake ya afya. Vile vile mfumo huu uwape nafasi wachangiaji kuweza kupata jumbe fupi za maneno zitakazo wakumbusha na kuwatia moyo wa kuendelea kuimarisha kiwango cha pesa kwenye akaunti zao.
3. Wizara ya afya kupitia Bohari ya Dawa (Medical Store Department) ihakikishe kuna upatikanaji wa dawa muhimu nchini kwenye kila kituo cha kutolea huduma za afya. Watu wengi wanaona si lazima kukata bima ya afya kwa sababu hata wakienda kwenye vituo vya kutolea huduma wanaambiwa hakuna dawa, hii huwapunguzia hamasa ya kuona umuhimu wa kutumia bima ya afya na hivyo kuwafanya wemgi wao watumie pesa moja kwa mioja kutoka mifukoni mwao ili kuweza kupata huduma. Hivyo, mikakati ya upatikanaji wa dawa kama vile kuundwa kwa mfumo maalumu wa kielektroniki utakaounganishwa moja kwa moja na mfumo wa bohari ya dawa kuonyesha mwenendo wa dawa katika vituo vyote vya afya, mfumo huu utaweza kuonyesh dawa zinazotumika sana na dawa gani zinahitajika kwa mda husika na ni kundi gani linalotumia sana dawa hizo. Mfumo huu utatoa mawasiliano ya moja kwa moja kwenda Bohari ya Dawa nahivyo kupunguza ukosefu wa dawa vituoni, jambo litakalovutia wananchi kukata bima ya afya.
4. Serikali iandae mpango maalumu utakao wafanya wafanyabiashara wote wawe na bima ya afya. Mpango huu utafanywa kupitia kodi wanazolipa wafanya biashara kwenda TRA, mfano kodi ya mfanyabiashara ni shilingi 200,0000/= kwa mwaka, ndani ya hiyohiyo kodi bila kuongezeka kwa gharama yoyote ile itengwe asilimia kidogo itakayompa fursa mfanyabiashara huyo kupata bima ya afya kupitia kodi anayolipa, hivyo mfanyabiashara atachangia uchumi wa nchi kwa kulipa kodi, vilevile atafaidika na bima ya afya bila kuathiri kiwango chake cha kulipa kodi. Hivyo wafanyabiashara wengi hawatakwepa kulipa kodi kwani watajua fika ya kuwa faida wanayoipata kupitia kodi zao ni kubwa, hivyo afya za watu zitaimarika na uchumi wa nchi pia utaongezeka kupitia ulipaji wa kodi kwani wengi watavutiwa na mfumo huu.
5. Wizara ya afya iandae mpango mpya wa makubaliano na hospitali binafsi. Watu wengi wanaona si muhimu kwenda kukata bima kwa sababu hospitali nyingi ambazo si za serikali zimekuwa hazipokei wagonjwa wa bima za afya hasa wale wa NHIF, na hii inafanya kuwe na wanachama wachache katika mfuko huo wa bima kwani watu hawako tayari kukata bima kwa kuhofia ufinnyu wa huduma za afya. Hivyo wizara ya afya ikae upya mezani na hospitali zote za binafsi pamoja na taasisi zote zinazotoa huduma ya afya, ili wakubaliane namna gani wataweza kushirikiana katika kutoa huduma za afya kwa kutumia bima ya afya hasa NHIF. Wizara iandae sera rafiki zenye faida shindani itakayoweza kutoa fursa kwa pande zote mbili kuweza kutoa huduma za afya kwa wanachi bila tatizo lolote lile. Hospitali za serikali pekee haziwezi kuhudumia watanzania zaidi ya milioni 60, hivyo wizara waunde sera madhubuiti zitakazo wavutia wotoa huduma za afya katika sekta binafsi kupokea wagonjwa wa bima ya afya. Kwa kufanya hivi itatoa hamasa kwa watanzania walio wengi kukata bima ya afya kwa ustawi wa maisha yao.
Hivyo basi, Ni jambo la msingi kuhakikisha matumizi ya bima za afya kwa watanzania wote yanafikiwa kwa kiwango cha juu, taifa lolote lenye watu wenye afya njema ni taifa lililo katika hatua nzuri ya kuimarika katika nyanja zote ikiwemo kijamii, kisiasa na kiuchumi, na kwa sababu hiyo upatiakanaji wa bima za afya kwa watu wote itakuwa ni chachu la kuwa na taifa lenye afya lililo na watu hodari wanaojitoa katika kulijenga taifa lao kwa kufanya shiughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Bima yako, afya yako.
Asante kwa kusoma andiko hili, tushirikiane kujenga ustawi wa taifa letu.

Upvote
0