Zaydkhan
Member
- Mar 31, 2017
- 33
- 41
UTANGULIZI
Salaam na Amani ziwe nanyi, Karibuni katika mnakasha huu utakaojikita katika mbinu za namna ya kuutengeneza na kukuza uzalendo,
Imani yangu mnakasha huu utaleta fikra chanya za kuujenga uzalendo. Tenga muda wako kuungana na mimi katika huu mnakasha, naamini utajifunza mengi kuhusu uzalendo.
UZALENDO NI NINI?
Uzalendo ni hisia ya mapenzi na kujitolea kwa chochote kwa ajili ya jamii.
Uzalendo unaweza ukawa ni uzalendo wa ukanda(Regionalism), utaifa(Nationalism), Ukabila(Tribalism), dini (Religionism). Ila uzalendo nitakaongelea humu ni uzalendo wa Taifa.
Uzalendo ni tofauti na Uraia "kila raia anaweza kuwa mzalendo lakini sio kila raia ni mzalendo". Kauli hii ndo iliyoleta kichwa cha habari cha mnakasha huu kuwa uzalendo unatengenezwa.
Lakini pia uzalendo una sifa ya kupanda na kushuka, zipo sababu mbalimbali zinazoweza kufanya uzalendo wa mtu upande au ushuke,
Kwa mfano upendeleo(Favouritism) katika taifa hufanya jamii inayopendelewa kuongeza uzalendo kwa nchi yao lakini pia inashusha uzalendo kwa jamii ambayo inaona kuwa wao wametengwa na jamii fulani inayopendelewa. Msingi huu ndo unaofanya niweke anuai ya kukuza uzalendo.
AINA ZA UZALENDO
Nitaelezea aina mbili za uzalendo, uzalendo wa asili (Natural patriotism) na uzalendo wa kutengenezwa (Constructive patriotism).
Uzalendo wa asili huu mtu uzaliwa nao,mfano wa uzalendo wa asili ni mfano wa mapenzi ya mama kwa mtoto, hata mwanae awe mtukutu vipi bado atampenda
Uzalendo wa kutengenezwa huu mtu anafanyiwa vitu ambavyo vitamfanya awe na hisia za mapenzi kwa nchi yake.
Moja ya Sifa ya uzalendo,Uzalendo sio kusifia tu mzalendo atakosoa pale panapostahili kukosoa. Na sio kukosoa tu atakosoa akitoa na jawabu ya nini kifanyike.
MBINU ZITAKAZOSAIDIA KUTENGENEZA NA KUKUZA UZALENDO.
Mbinu izi ni kwa ajili ya kutengeneza na kukuza uzalendo wa kitaifa :
1. Kuitengeneza upya historia ya nchi.
- Asiyejua alipotoka hawezi kujua anapokwenda, historia ina nafasi kubwa sana katika kujenga uzalendo. Historia hujenga ujasiri baada ya kizazi kusoma ujasiri wa wazee wao waliopita.
- Kuna haja ya kufundisha vizazi vyetu historia kwa upana wake. Kuna historia nzuri za nchi yetu lakini hazifundishwi mashuleni na ni wachache wanaojibidiisha katika kuzijua.
- Ili tukuze uzalendo ni lazima tuongeze maudhui mazuri ya historia yetu na kufuta baadhi ya maudhui ambayo hayana faida kwa nchi yetu.
2. Kufuta mikopo na kuwapa ruzuku wanachuo.
- Nchi imefanikiwa katika kuweka elimu bure ngazi za chini ya chuo kikuu. Hii Elimu bure itawejengea uzalendo. Lakini kama nchi isiishie hapa,hapa naomba tuelewane vizuri:
- Mkopo wa riba kwa wanachuo umekuwa ni mzigo mzito kwa wahitimu, hili kundi la wanachuo wachache ndo tunategemea kwenda kuwahudumia watanzania waliowengi.
- Ukweli uliowazi wengi wanazisotea ajira kwa muda mrefu na wakishapata ajira wanakuwa na mzigo wa riba ya mkopo nje ya kodi ya mshahara wake.
- Mwisho wa mwezi atapokea fungu liliopungua sana ili kulijazia na aweze kumudu gharama za maisha ikitokea nafasi ya ubadhilifu au rushwa huyu mhitimu ataweka uzalendo pembeni.Tusiwape sababu ya kukosa uzalendo.
- Pia Kuna haja ya serikali kufuta mkopo na kutoa ruzuku, kwa sababu hii itasaidia serikali kuwawajibisha wahitimu wa chuo kama wataamua kukimbilia kufanya kazi nchi nyingine hali ya kuwa nchi inawahitaji.
Kama nchi itakuwa na nguvu ya kisheria ya kumkamata uko alipo na kumrudisha nyumbani sababu ametumia kodi ya wananchi katika elimu yake.
3. Kuweka Sheria kali za kusimamia uzalendo.
- Ni asili ya kila binadam ukimpa uhuru usio na sheria huutumia vibaya, matendo ya binadam lazima yadhibitiwe na sheria.Sheria ina mchango wa zaidi ya 70% katika kujenga uzalendo.
- Kuwe na sheria kali kwa mtu atakeyeonesha vitendo ambavyo si vya kizalendo kama kuhujumu uchumi, kuzua machafuko ya kisiasa na kijamii.
- Ningependekeza kama mtu amefanya matendo si ya kizalendo na ameshaonywa kujirekebisha na hajirekebishi, ifikie mahali tuwe na sheria ya kumfutia mtu uraia.
- Mtu akifutiwa uraia kwa kukosa uzalendo na akakosa nchi ya kuhamia, tutamhukumu kwa kosa la mhamiaji haram. Akitumikia kifungo cha uhamiaji haram na akiahidi kubadilika atachiwa huru chini ya usimamizi maalum wa kuchunguza mwenendo wake.
4. Kutumia alama za taifa katika maisha yetu ya kawaida.
- Sijui kisheria ipoje lakini kuna hofu mitaani mtu kuvaa nguo zenye rangi ya bendera ya nchi.Ni vizuri Kutumia bidhaa zenye alama za taifa kwa mfano nguo, penseli, peni, madaftari n.k yenye rangi za bendera ya nchi huongeza fikra za kizalendo.
- Inawezekana ikaonekana ni kitu kidogo lakini kikawa na athari kubwa kiakili. Ni rahisi kumkuta mmarekani, mwiingereza ana bendera ya nchi yake katika gari ila ni watanzania wachache watakaoweka bendera ya nchi yake ndani ya gari lake.
- Inawezekana ikaonekana ni kitu kidogo lakini inaonesha huyu aliyeweka bendera ndani ya gari yake anajivunia utaifa wake. Kutumia alama za taifa katika shughuli zetu za kila siku kutachochea kukuza uzalendo.
Mwisho, nchi hujengwa na watu na uzalendo hujengwa na viongozi. Kila mtu ni kiongozi tofauti ni nafasi, uongozi unaanzia ngazi ya familia hadi taifa. Na kila mtu ana familia anayotoka, kila mtu anajukumu la kujenga kizazi kitakachokuwa na mapenzi kwa nchi yake.

Upvote
2