Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
MBIO za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea katika mkoa wa Shinyanga, zimeingia dosari baada ya baadhi ya wakimbiza mwenge huo kitaifa kuonyesha wazi wazi kukipigia kampeni Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi hao wanawashawishi wananchi kumchagua mgombea urais wa chama hicho,Rais Jakaya Kikwete na kuwaponda wanachama wa chama hicho waliokihama na kujiunga na vyama vya upinzani.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 3:30 asubuhi katika kijiji cha Wigelekelo wilayani humo juzi, wakati wa makabidhiano ya mwenge huo ukitokea Manispaa ya Shinyanga.
Mmoja wa wakimbiza mwenge hao, Mwashibanda Lucas Shibanda, wakati akitoa salamu kwa baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Maswa waliokusanyika kuupokea mwenge huo, alisema wilaya hiyo ni ya kihistoria, lakini imekuwa ikichanganywa na wanasiasa wanaotangatanga kama kumbikumbi wasiokuwa na makazi.
Watu wa Maswa, mtaonekana kuwa mmepotoka iwapo itaonekana mnampatia uongozi mtu aliyejiunga na kanisa jipya, kwani huyo ana tamaa ya uongozi hakuna aliyezaliwa duniani kuwa kiongozi hadi kufa bali ni kuachiana zamu sasa ni zamu ya mwingine,alisema Shibanda.
Kauli hiyo, ilionyesha wazi kumlenga aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Maswa kupitia CCM, John Shibuda, aliyejiondoa baada ya kushindwa katika kura za maoni kwa madai ya kutawaliwa na vitendo vya rushwa na kuamua kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).
Naye Kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Dk. Nassoro Ally Matuzya, aliwataka wananchi kutojali ahadi zinazotolewa na wagombea mbalimbali, bali waangalie sera za wagombea wa chama.
Akizungumzia hali hiyo, Katibu Uenezi wa CHADEMA Wilaya ya Maswa, Mbaraka Manyundo, alisema wakimbiza mwenge hao wameacha kuzungumzia ujumbe wa mwenge mwaka huu na kuanza kuwapigia debe wagombea wa CCM, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.
Source : Tanzania Daima