Elections 2010 Mbio za mwenge zageuka kampeni ya CCM

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,804
Reaction score
10,715
MBIO za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea katika mkoa wa Shinyanga, zimeingia dosari baada ya baadhi ya wakimbiza mwenge huo kitaifa kuonyesha wazi wazi kukipigia kampeni Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Viongozi hao wanawashawishi wananchi kumchagua mgombea urais wa chama hicho,Rais Jakaya Kikwete na kuwaponda wanachama wa chama hicho waliokihama na kujiunga na vyama vya upinzani.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 3:30 asubuhi katika kijiji cha Wigelekelo wilayani humo juzi, wakati wa makabidhiano ya mwenge huo ukitokea Manispaa ya Shinyanga.

Mmoja wa wakimbiza mwenge hao, Mwashibanda Lucas Shibanda, wakati akitoa salamu kwa baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Maswa waliokusanyika kuupokea mwenge huo, alisema wilaya hiyo ni ya kihistoria, lakini imekuwa ikichanganywa na wanasiasa wanaotangatanga kama kumbikumbi wasiokuwa na makazi.

“Watu wa Maswa, mtaonekana kuwa mmepotoka iwapo itaonekana mnampatia uongozi mtu aliyejiunga na kanisa jipya, kwani huyo ana tamaa ya uongozi hakuna aliyezaliwa duniani kuwa kiongozi hadi kufa bali ni kuachiana zamu sasa ni zamu ya mwingine,”alisema Shibanda.

Kauli hiyo, ilionyesha wazi kumlenga aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Maswa kupitia CCM, John Shibuda, aliyejiondoa baada ya kushindwa katika kura za maoni kwa madai ya kutawaliwa na vitendo vya rushwa na kuamua kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Naye Kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Dk. Nassoro Ally Matuzya, aliwataka wananchi kutojali ahadi zinazotolewa na wagombea mbalimbali, bali waangalie sera za wagombea wa chama.

Akizungumzia hali hiyo, Katibu Uenezi wa CHADEMA Wilaya ya Maswa, Mbaraka Manyundo, alisema wakimbiza mwenge hao wameacha kuzungumzia ujumbe wa mwenge mwaka huu na kuanza kuwapigia debe wagombea wa CCM, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.


Source : Tanzania Daima
 
Shibuda kaweka ukweli wazi pale aliposema'mimi ni mlokole na nimeamua kujiunga katika chama cha kilokole ambacho ni Chadema'haya maneno kayasema katika mkutano wa kampeni huko maswa.
Kweli kabisa sasa tumeamini chadema si chama cha siasa bali ni pandikizi kutoka kanisani,wadanganyika mtaendelea kudanganywa hadi lini?Kuweni macho na watu hao msije mkalilia maliwatoni!
 
kiukweli hawa wakimbiza mwenge hata walipokuja huku kwetu waliongea maneno ya kumpigia debe kikwete,especially huyo kiongozi wa mbio za mwenge mpaka binafsi nilijiuliza hizi ni kampeni au?yaani iliboa kabisa

NB: Hilo la Shibuda hata mi mi nililiona ITV nikashindwa kumwelewa kabisa na zaidi ya hilo Chadema haijatoa ufafanuzi kwamba hiyo ilikuwa ni kuteleza au alitumia msemo kumaanisha chama cha waadilifu na si cha kilikole, kitendo cha kukaa kimya hadi leo kimenipa imani kuwa chadema ni chama cha kilokole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…