Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 144
KIONGOZI wa Dini Padri Lucian Malamsha wa Kanisa Katoliki Zanzibar amemfananisha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Rais (Muungano) Mohamme Seif Khatib na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Padri huyo amesema Khatib ndiye kiongozi hasa anayefuata muongozo na nyayo za baba wa taifa, Mwalimu Nyerere katika utumishi wake wa kulitumikia taifa la Tanzania.
Tamko hilo amelitoa jana katika mkutano wa hadhara alipokuwa akihutubia wananchi katika hafla ya kukabidhi nguzo za umeme zinazotarajiwa kutumika kusambaza huduma hiyo katika vijiji vya wilaya ya kati katika Jimbo la Uzi Kisiwani Unguja.
Padri Malamsha alisema Waziri Khatib ametoa mchango mkubwa katika kutumikia taifa la Tanzania na ni miongoni mwa viongozi wachache walioonesha uadilifu wa kujiepusha na vitendo vya ufisadi katika jamii na hasa wakati huu ambao viongozi wengi wamekubwa na kashfa hiyo.
Alisema kwamba viongozi wengi wamekuwa wakitoa ahadi, lakini baadaye hushindwa kuzitekeleza, kitendo ambacho hakileti sura nzuri na kusema kitendo cha kukabidhi nguvu za umeme ni ukombozi mkubwa katika kuwasogezea maendeleo wananchi katika vijiji hivyo.
Padri huyo alimsifia Waziri Khatib ambapo alisema ameanza kumfahamu miaka mingi tokea alipokuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM taifa na ni miongoni mwa viongozi waliotoa mchango mkubwa katika kulitumikia taifa na kudumisha muungano wa tanganyika na zanzibar.
Ndugu wananchi mliokusanyika hapa mnamuona mheshimiwa khatib hata umbo lake linafanana la Mwalimu Nyerere, amekuwa hanenepi kutokana na harakati nyingi alizonazo kutumikia wananchi, alisema Padri huyo.
Kiongozi huyo wa dini alisema hivi sasa Tanzania kuna viongozi wengi lakini ni wachache ambao wamekuwa wakifuata misingi ya baba wa taifa ya kuwa karibu na wananchi na kujua matatizo yao jamo ambalo limesababisha wananchi wengi kukosa imani na serikali yao kutokana na na tabia za viongozi hao.
Aliema kwamba Waziri Khatib pamoja na kukabidhiwa wizara nzito ya muungano lakini ameweza kuiongoza kutokana na kufuata misingi ya uongozi ya baba wa taifa na kuweka mbele maslahi ya taifa tofauti na wenzake.
Kutokana na uwezo wake wa kudumisha Muungano ndio maana wananchi kutoka Bara leo hii wanaishi bila matatizo yoyote Zanzibar na wale wa Zanzibar wanaishi Bara kwa utulivu kabisa, alisema Padri.
Askofu huyo alisisitiza Nakuombeni wananchi zingatieni ule msemo wa Kiswahili, Usiache mbachao kwa msala upitao na Zimwi likijualo halikuli likakwisha kwa hivyo wenyewe mna hiari yetu tena hapo, alisema na kuibua shangwe za wananchi hao.
Kwa upande wake akitoa shukurani zake kwa wananchi hao, Waziri Khatib amesema mradi huo wa umeme utasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo iwapo wananchi watatumia nishati hiyo kwa kubuni miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Alisema mradi huo utawasaidia wananchi wote bila ya kubagua kwani kitu kizuri ni kuishi kwa mashirikiano bila ya kujali itikadi za kisiasa wala kidini huku akiwataka wananchi hao kufahamu kwamba msingi mkuu wa taifa hili ukiwa ni usawa katika kupata haki.
Katika hatua nyengine Waziri Khatib aliwataka wananchi kukamilika masharti ya sifa wajitokeza kujiandikisha katika zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura linaloendelea hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Pia aliwataka wafuasi wa CCM na CUF waache tafauti zao na washirikiane katika miradi ya maendeleo kwa vile maendeleo hayawezi kupatikana bila ya kuwepo mashirikiano ya pamoja ya wananchi katika maeneno husika.
Waziri Khatib alikabidhi nguzo 100 za umeme na kukagua vituo vya afya katika vijiji vya Ghana, Mpapa ambayo imekuwa ikijengwa kutokana na mchango mkubwa wa viongozi wa jimbo hilo.
SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.