Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji (MwanaHalisi)
Sasa najua kwanini waliliua Azimio la Arusha kule Zanzibar na kulizika bila kuliswalia dua za mwisho wala kulifanyia ibada ya mazishi. Sasa najua kwanini jina lake azimio hilo limefutwa milele kwenye vinywa vyao. Mwenzenu sasa nimetambua ni kwanini kabla ya kuanzisha wizi wao mkubwa wa mali na utajiri wa nchi yetu na kugawana wao kwa wao na watoto wao ilibidi kwanza kabisa wakiondoe kizuizi pekee kilichokuwa kati yao na urithi wa wana na mabinti wa taifa hili. Sasa najua, kwanini vita hii dhidi ya ufisadi ni vita ya kugombania hatima ya taifa letu!
Azimio la Arusha lilipotangazwa lilikuwa na lengo la kuhakikisha kuwa utajiri wa nchi yetu unagawanywa kwa wananchi wa taifa hili. Lengo la Azimio halikuwa kugawana umaskini bali kugawana utajiri. Leo hii, wao wanagawana utajiri sisi tunatakiwa kugawana umaskini. Na wakati wowote tutakapojaribu kutaka kugawana utajiri wetu wao (wetu) ndivyo hivyo hivyo mapambano haya yatakuwa magumu zaidi.
Kinyume na watu wengine wanavyoona, ninaliona sakata la Mengi na wale aliowaita kuwa ni mapapa wa ufisadi kuwa ni mapambano ya kugombania urithi wetu. Alichofanya Mengi na Mwakyembe kabla yake na wale waliochapisha ile taarifa ya Tanzanias Mafia iliyoanzisha sakata hili la kwenye mtandao wa Jamiiforums.com ni kutukumbusha kuwa hatuwezi kamwe kuuachia urithi wa nchi yetu mikononi mwa kikundi cha watu wachache.
Ni kile kile kilichofanywa na Dr. Slaa na kundi la wapinzani pale Mwembe Yanga walipotangaza ile Orodha ya Aibu ya mafisadi. Ni kile kile kilichopigiwa kelele Bungeni na kina mama Kilango na kina Mkumba. Ndiyo, ni sehemu ile ile ya mapambano ya kugombania urithi wetu. Kama watu wanafikiria hili ni suala la Mengi na Manji au Mengi na Rostam basi wanakosa kuiangalia picha nzima. Wanaona sehemu sehemu tu.
Kwani, Mengi akikaa kimya, mama Kilango akifunga kinywa chake na kina Mwakyembe wakisalimu amri, haitakuwa mwisho wa mapambano. Watakuwa wamekubali kama walivyokubali wabunge wengine na watumishi wengine wa serikali kuwa sehemu ya utawala wa himaya ya kifisadi inayoongozwa na watu wanaokula kwa mikono miwili bila kunawa, na wanakula siyo minofu tu ya kuku, bali wanakula miguu na firigisi pia, tena wanakula bila kutaka waulizwe! Tukiwauliza wanatuelekeza kwenye kula utumbo!
Ndugu zangu, yawezekana kuna mgongano wa kibiashara, yawezekana kuna chuki au kinyongo cha mambo fulani lakini hayo yote hayaondoi ukweli kuwa hatima ya taifa letu inashikiliwa na kundi la watu wachache; kundi ambalo halitaki kuulizwa, halitaki kuhojiwa na kwa hakika halitojitolea hata siku moja kutoa majibu zaidi ya kutisha watu na kutufanya tuishi kwa wasiwasi.
Wapo watu wengi na wenye nguvu ambao majina yao yanajulikana, uwezo wao unazidi makisio na nafasi yao katika jamii ni sawa na wana wa mfalme fulani. Watu hawa wamechukulia kuvunjwa kwa Azimio la Arusha kama kibali cha wao kutunyonya kama wana akili fyatu. Na wanatufyonza kama mtu anayefyonza ganda la muwa na kuliacha kapi.
Katika watu ambao wanaunda kundi hilo, kundi ambalo naamini lina nguvu kuliko inavyofikirika wapo wengi. Watu hawa hawana rangi, kabila au dini, ni wanyonyaji wa hali ya juu (nafahamu neno mnyonyaji kwa wengine ni geni). Wamejikita katika siasa na utendaji wa nchi yetu na katika kufanya hivyo wamejitengenezea himaya yao ya ufisadi. Chini yao wana watu ambao nimewaita makuwadi wa ufisadi na hivi karibuni tumeona siyo makuwadi tu wa ufisadi waliopo bali pia wametengeneza vikaragosi vya mafisadi!
Miongoni mwa watu hao ambao wamechota utajiri wetu kama kutoka kisimani huku wakiturishia vimifupa kama mwizi anavyomrushia mbwa nyama ili asibweke sana wapo watumishi wa umma, wanasiasa na wafanyabiashara. Watu hao wana mtandao unaotisha, mtandao ambao ni imetengeneza pembetatu ya ufisadi (the triangle of corruption). Pembetatu hiyo inahusisha wafanyabiashara, wanasiasa na watendaji serikalini.
Katika pembetatu hiyo kuna watu watatu ambao ni lazima niwataje hapa, yupo Sir. Andy Chande, yupo Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na yupo Mbunge na mfanyabiashara maarufu Mhe. Rostam Abdulrassul Aziz (Igunga CCM). Hawa watatu ndio naamini wanaunda mhimili wa ufisadi Tanzania (the axis of corruption). Chini yao kuna makumi na mamia ya watu ambao wanatekeleza majukumu yao mbalimbali kuhakikisha kuwa pembetatu hiyo ya ufisadi haivunjiki.
Chini ya hawa watatu wapo ambao tunaweza kuwaita makuwadi wa ufisadi. Hawa ni watendaji serikalini ambao wamekubali kuuza haki yao na utu wao na uhuru wa Taifa letu kwa bei. Hawa ni wasomi waliokubuhu na watu wazito tu lakini kutokana na ahadi ya utajiri wa haraka haraka wamekubali kupinda sheria, kuvunja sheria na wakati mwingine kuiharibu sheria ili kurahisisha uporwaji wa mali za taifa letu. Ndiyo hawa waliorahisisha wizi wa Benki Kuu, ndiyo hawa waliofumba macho wakati nchi inabakwa na ndiyo hawa hawa ambao leo hii wengine wamefikishwa kizimbani. Lakini wengi bado wapo katika maofisi na taasisi mbalimbali.
Hawa si watu wenye vyeo vya chini bali ni Wakurugenzi, Wenyeviti wa Bodi na watu wazito kwenye baadhi ya taasisi zetu nyeti. Wengi wa hawa waliteuliwa na kupewa nafasi zao za juu kutokana na maamuzi au mapendekezo ya mhimili wa ufisadi. Hawa sasa hivi wameshibishwa neema ya nchi yetu.
Pamoja na hawa serikalini kuna makuwadi wengine kwenye siasa ambapo baadhi ya Watanzania wenzetu walikubali kununuliwa kwa bei ya chini ili waweze kupewa nafasi ya kushinda uchaguzi. Wengi wa hawa ni wanasiasa walionufaika kwa namna moja au nyingine na fedha za Mhimili.
Katika kuwafikia watu hawa hakuna mtu mwenye nguvu kubwa kama Rostam. Rostam ametoa ufadhili kwa wanasiasa mbalimbali na kuwasaidia kushika nafasi zao walizonazo sasa. Katika kufanya hivyo amejihakikishia kundi kubwa la watu watiifu kwake. Watu hawa ambao amewasaidia wengi wamesainishwa misaada hiyo (kama alivyomfanyia Mtikila) na hivyo kujikuta hawana uwezo wala ubavu wa kusema kitu chochote dhidi ya Rostam.
Katika kufanya hivyo utaona kuwa Rostam amepanga mojawapo ya safu ya makuwadi wake ambao siyo tu wana nafasi lakini pia wana nguvu kubwa mno. Tukumbuke kuwa aliyekuwa Meneja wa kampeni ya Urais wa Rais Kikwete ni Bw. Rostam Aziz (wakati huo akiwa pia mweka hazina wa CCM).
Kwa nafasi yake hiyo Rostam alijua kila senti iliyokuwa inaingia na kutoka kwenye kampeni ya Kikwete. Ni yeye ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa katika kuchangisha fedha za kampeni hiyo. Tunapojiuliza fedha za kampeni za Urais wa Rais Kikwete zilizotoka wapi jibu analo Rostam!
Kwa watu wanaokumbuka (kama mzee wenu hapa) Rostam alihusishwa na kutajwa na gazeti maarufu la Africa Confidential kuwa alipokea kiasi cha dola milioni 2 kutoka Oman kwa ajili ya kampeni ya uchaguzi. Kiasi hicho ni kingine ya kila kilichotajwa na Christopher Mtikila kuwa kilitoka Iran (kupitia kwa Rostam) na ambacho kilitumiwa katika mchakato wa kumtafuta mgombea wa CCM.
Vyanzo vyangu vya karibu kabisa vimenidokeza kuwa kiasi kilichotoka Oman kilitolewa na mfanyabiashara maarufu aitwaye Gen. Suleiman Al-Adawi ambaye alikuwa ni kigogo na msaidizi wa karibu wa Sultani wa Oman. Gen. Al-Adawi ni mzaliwa wa Zanzibar ingawa si raia wa Tanzania.
Wakati huo Kikwete alitishia kulifungulia mashtaka gazeti hilo lakini hakufanya hivyo. Ukweli ni kuwa Kikwete hakujua fedha zimetoka wapi kwani alimuamini Rostam na hivyo hakukuwa na kesi siyo dhidi ya hilo gazeti tu bali hata Mtikila hakushtakiwa na hivyo kuwapa nguvu kuwa madai yao ni ya kweli.
Hata baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani tunawaona watu mbalimbali waliohusiana na Rostam wakishika nafasi mbalimbali za utendaji na tena kwenye sehemu nyeti. Aliyetaka kugombea jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM ambaye alikuwa ni mtumishi wa Wizara ya Nishati na Madini Dr. Peter Kafumu aliyekuwa anaonesha kutoa ushindani mkubwa kwa Rostam alijikuta anakaa pembeni na kumpisha Rostam kwenye kiti hicho. Inadokezwa kuwa kwa kufanya hivyo atakumbukwa katika awamu mpya. Rostam akawa hana mpinzani kwenye kura za maoni!
Baada ya kuchaguliwa Rais, Kikwete alimkumbuka Bw. Kafumu kwa kumteua kuwa Kamishna wa Madini. Hili inadaiwa lilikumbushwa na Rostam.
Barua iliyotoka kwa Salva Rweyemamu (alikuwa mhariri wa Habari Corporation) kwenda kwa Rostam ilivujishwa karibu wiki mbili zilizopita. Katika barua hiyo ambayo imewafungua watu wengi macho inaonesha ni jinsi gani Rostam (RA kwa kifupi) amekuwa na nguvu mno. Katika barua hiyo ambayo sehemu kubwa ni jinsi gani Rostam aliacha kampuni aliyoinunua kufanya kazi kinyume cha sheria (bila kusajiliwa)) ilikuwa na sehemu ya mambo binafsi pia ambapo kimsingi Salva anaonekana akimkumbusha Rostam juu ya ahadi yake/zake kwake.
Inaonekana katika barua hiyo Salva alikuwa hajakumbukwa na awamu hiyo mpya na akawa anashangaa inakuwaje baada ya jitihada zote (kwenye vyombo vya habari wakati wa kampeni) yeye hajakumbukwa. Akamhoji Rostam kama ndivyo wanasiasa wanawatenda wale watu walio karibu nao na waliowasaidia kushika madaraka. Wiki chache baadaye Salva Rweyemamu akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Rostam alimkumbuka tena.
Aliyekuwa Wakili wa Vodacom (Mkuu wa kitengo cha sheria) na ambaye alisaidiwa na Rostam kuingia kampeni ya uchaguzi wa Ubunge kule Sengerema ni Bw. William Ngeleja. Wakati akiwa Vodacom mmoja wana hisa wa kubwa alikuwa (bado ni) Bw. Rostam Aziz. Baada ya uchaguzi wa 2005 ambapo Ngeleja alishinda Sengerema, Kikwete hakumsahau kwani alikumbushwa na Rostam. Kwanza kama Naibu Waziri na baada ya matukio ya mwaka jana kuupata Uwaziri kamili.
(Hadi hapa tunawaona watu wawili wanaohusiana na Rostam wakiwa wizara moja).
Mtu mwingine ambaye tunamkuta ni Bi. Badra Masoud ambaye aliwahi kuwa mhariri wa Habari Corporation (pamoja na kina Salva). Huyu alitoka Habari na kupata ajira kule DAWASCO na baadaye Tanesco kama Afisa Mawasiliano. Akiwa DAWASCO wengi watakumbuka ndiye aliyetangaza kukatiwa maji kwa wadeni sugu akiwemo Dr. Mwakyembe. Habari hizo zilikuja wiki chache tu baada ya ripoti ya Richmond Bungeni. Lengo lilikuwa kumchafua Dr. Mwakyembe kitu ambacho kilishindwa baada ya kuonekana kuwa jaribio hilo limeshindwa.
Siyo yeye tu pale Tanesco bali pia Mkurugenzi wa Tanesco Dr. Idris Rashid ambaye naye ametoka huko Vodacom. Tukumbuke kuwa huko Vodacom Rostam ana hisa kubwa tu na hivyo kuwa na mtu kule Tanesco pia ni jambo la kuangalia sana kwa karibu.
Katika sakata la Richmond na Dowans jina la Rostam linatajwa. Kinyume na taarifa yake ya juzi kuwa ripoti hiyo haikumtaja kwa jina. Tukumbuke vizuri kuwa katika mkutano wake wa waandishi wa habari mwaka jana Bw. Rostam alizungumza kana kwamba haijui kabisa kampuni ya Dowans na kuwa aliacha tu kadi yake tu na kuwa alienda tu kuomba kazi.
Alinukuliwa kusema Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi.. Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani Maneno yake ya wakati ule yaliwaaminisha watu wengine kuwa Rostam haijui Dowans!
Ukweli (ambao sasa tunaujua zaidi) ni kuwa Rostam ndiye aliyefanikisha ujio wa mmiliki wa Dowans na kumsaidia kuweza kuanzisha kampuni hewa ya Dowans Holdings SA ya Costa Rica. Mmiliki huyo ambaye nyaraka za BRELA zinamuonesha si mwingine bali ni rafiki wa karibu na mshirika wa karibu wa Rostam Gen. Suleiman Al-Adawi ambaye ana undugu na mahusiano ya karibu ya kifamilia na Watawala wa Falme za Kiarabu. Rostam hakuwa mkweli wakati ule na kama angetaka kuwa mkweli angesema wazi mapema mahusiano yake na watu wa Dowans!
Naweza kuendelea kuandika mifano mingine mingi na watu wengine ambao Rostam amewasaidia katika kampeni za uchaguzi (nina majina karibu ya wabunge 40 ambao wako mfukoni mwake). Wabunge ambao ninawaita kuwa ni makuwadi wa ufisadi. Hawa msitegemee hata siku moja kuwaona wanapiga vita ufisadi au kupiga kelele juu ya uporaji wa mali zetu.
Jinsi ya kuwagundua wabunge hawa ni pale wanapozungumzia ufisadi. Wao wanasikika wakisema vita ya ufisadi ni vita yetu sote. Utawasikia wakisema mtu asitumie vita ya ufisadi kujinufaisha kisiasa. Kamwe hata hivyo hutawasikia wakipigia kelele Kagoda, EPA au kutaja majina ya watu ambao wanahusika na ufisadi. Watasikika kwa haraka kumlaani Mzee Mengi kwa jina lake lakini hawatasika kumtuhumu Rostam au vigogo wengine kwa majina yao.
Chini ya hao (makuwadi wa ufisadi) utawakuta vikaragosi vya ufisadi. Hili ni kundi kubwa la waandishi wa habari, na watendaji wa ngazi za chini wa CCM na wapambe wengine au mashabiki ambao kila mabwana zao wanapoguswa hufanya haraka kuwasafisha na kuwatetea. Wengine hufunga safari toka mikoa ya mbali ili waje wasikike. Vikaragosi hawa wapo hadi kwenye timu zetu za mpira na ambao mfadhili wao akiguswa wanakuja na kelele kuwa anaonewa ingawa wengine tunajua yaliyotokea Mbagala wiki iliyopita yawezekana kabisa kuhusishwa na biashara za mfadhili huyo!
Vikaragosi hawa wa ufisadi ni wale ambao bila haya wala soni wako tayari kuuza utu wao, hadhi yao na heshima yao ili wafadhiliwe. Ndiyo watu wa hatari pia katika mapambano haya kwani bei yao inajulikana. Ujumbe wetu kwa hawa wote (Pembetatu ya ufisadi, Mhimili wa ufisadi, makuwadi wa ufisadi na vikaragosi vya ufisadi) ni kuwa sasa imetosha iachieni nchi yetu! Mmeishikilia vya kutosha na sasa mnataka kututumikisha milele. Mmeuza urithi wetu na utajiri wetu mmegawana; leo mnataka sisi tugawane umaskini wetu wakati nyinyi mnamegeana utajiri wetu. Sasa yatosha!
Labda niwakumbushe mbiu ile ya Azimio la Maskini!
Tumeonewa kiasi cha kutosha, Tumenyonywa kiasi cha kutosha,
Na tumepuuzwa kiasi cha kutosha; Unyonge wetu ndio umetufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge wetu ili tusionewa tena, tusinyonywe tena!
Ni mimi: Mwanakijiji@mwanakijiji.com