SoC02 Mbivu na mbichi katika elimu ya Tanzania

SoC02 Mbivu na mbichi katika elimu ya Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Mbundaereneus

Member
Joined
Dec 3, 2019
Posts
38
Reaction score
10
Elimu ya Tanzania kwa miongo mingi imekuwa ikizalisha wahitimu maelfu kwa maelfu na kufanya Taifa lenye wahitimu katika ngazi mbalimbali wasiojua kesho yao kama vile astashahada,stashahada,na shahada.Hali ya elimu inafanya wasomi katika kisiwa hiki kutojua hatima Yao mbeleni katika maisha yao,sabuni ya kutakasa na kufuta hili tatizo ndugu,ambalo linazidi kuota mizizi katika nchi hii ya maziwa na asali ipo.

Elimu ya nchi yetu imepelekea, kuwepo wataalamu mbalimbali katika sekta mbalimbali ambazo ni muhimu katika maisha ya binadamu Katika sayari hii ya tatu.mambo yanayoweza kutia chachu Ili Elimu yetu iwe yenye manufaa ni kama haya yafuatayo:

Kufundishia na kujifunzia
Elimu yetu kwa miaka mingi kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu,imekuwa ikibadirika,kutoka shule ya msingi hadi chuo,hususani kwa shule za sekondari na msingi mwanafunzi huanza na lugha ya kiswahili katika kujifunza na baada kuja sekondar au chuo kikuu isipokuwa Somo la kiswahili,hutumia kingereza ambapo humpa mwanafunzi ugumu kuelewa masomo mbalimbali.

Mitaala
Mitaala inayotumika katika nchi yetu humpa mwanafunzi kazi ya kusoma masomo mengi, ambayo kwa kiwango kikubwa hushindwa kumudu masomo yote na kuweza kufaulu katika masomo yote,Kwani mwanafunzi huweza kusoma masomo hadi Tisa,ambapo ni tofauti na nchi zilizoendelea.

Stadi za maisha
Ujuzi katika elimu inayotolewa nchini Tanzania,hauwajengi wanafunzi katika kutenda katika mazingira halisi watakayoyaishi,kwa kutumia elimu wanayoipata shuleni,Kwani elimu imekuwa ikitolewa kwa ajiri ya maisha ya darasani tu.

Umbali
Wanafunzi wanachofundishwa shuleni,ni tofauti na maisha watakayoenda kuyaishi,Kwani elimu wanayoipata shuleni hubaki imejitenga kati ya wafundishaji na wafundishwaji.

Vitabuni
Wahitimu wa ngazi mbalimbali hupata elimu ambayo hushindwa kuitumia katika maisha yao,Kwani maarifa ya shuleni huyaacha humo kwenye vitabu,Kwani hushindwa kubadiri ujuzi walioupata shuleni kuzalisha kitu Fulani kwa ajiri ya jamii.

Kikoloni
Wakoloni walitoa elimu kwa ajiri ya kuwatumikia wao,na sio kutumika kwa ajiri ya kujiletea manufaa yetu binafsi,hivyo basi elimu hii imekuwa ikiwatayarisha wahitimu kwa ajili ya kuajiriwa tu, kuliko kujiajiri.

Kukariri
Mafunzo katika shule zetu yaliyo mengi ni kukazana, kuweka vitu vingi kwa pamoja kichwani,
bila hatakuelewa Ili mradi kufaulu mtihan tu,vitu hivyo ambavyo ni vingi,havina faida maishani mwao,kwa mfano mwanafunzi hukaririshwa makao makuu ya Japani ambako Hana ndoto za kufika huko.

Ubunifu
Mamia ya wahitimu katika ngazi mbalimbali,hawawezi kuunda kitu chochote kutokana na maarifa waliyopata shuleni,kutokuwa na manufaa,au kukosa uwezo wa kubuni /kuunda kitu chochote kidogo kama vile vijiti vya kuchokonolea meno.

Mazingira
Mazingira ya utolewaji wa elimu yetu,sio mazuri kwa kuwezesha elimu kuwa nzuri, kwa upande wa vifaa vya kufundishia ni duni,pia miundombinu kama madarasa,maabara,ni duni,nyumba za kuishi walimu,hivyo hupelekea elimu kutokuwa Bora.

Kutumikia
Elimu yetu haimtayarishi mhitimu kujiajiri Bali,inamtayarisha baada ya kumaliza elimu aweze kuajiriwa,ndio maana wanaomaliza elimu wanakosa uwezo wa kujitumikia,wanataka kutumikia zaidi.Hivyo basi inatakiwa kufanya hivi:

Maboresho
Serikali haina budi kubadiri,sera ya elimu, mitaala,vyombo vya ukuzaji wa mtaala,vinatakiwa kuchunguza elimu yetu,Ili wanajamii waweze kunufaika na elimu itolewayo pamoja na kugeua mazingira ya utoaji wa elimu.

Mawasiliano 0763827083,0627727595
 
Upvote 2
Ahsante kwa makala nzuri, kura yangu nimekupatia. Karibu pia katika makala yangu, kwa maoni na ushauri
 
Back
Top Bottom