WrestlerRSF254
JF-Expert Member
- Jan 30, 2023
- 1,196
- 2,012
Habari wana jf,
Diwani wa kata ya Ikunguigazi, iliyo Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita, ndugu Paulo Lutandula, ameshindwa uzalendo na kuamua kutumia maneno ya vitisho na chuki dhidi ya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Ikunguigazi (jina tunalihifadhi).
Diwani huyo ametoa siku kumi na tano toka leo, kama Mwalimu huyo hatohamishwa atahamasisha jamii kwenda kumvamia Mwalimu huyo, tumewasiliana tayari na Mbunge wa Jimbo la Mbogwe na amesema taarifa hiyo ya Diwani analijua.
Mwalimu hausiki na tuhuma dhidi yenu viongozi, tatizo kwa wananchi ni nyie viongozi na sio Mwalimu unayemtishia kwa maneno makali hii haikubaliki. Nitafute mimi Amnbueogeblezz niliyefichua maovu yenu na sio Mwalimu huyo, najua mabaya yote ya viongozi wa Ikunguigazi na nitazileta hapa
Kila kitu unakijua mh Diwani, hivyo basi usijifiche na kutaka kukwepa tuhuma dhidi yenu, sauti yenu ninazo zenye kila kitu, na naahidi kuja kuziachia hadharani, chochote kikimkuta Mwalimu wetu au familia yake kuanzia leo ni wewe ndiye mhusika namba moja.
Tunaomba serikali yetu ya halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, na serikali yetu ya Mkoa wa Geita ichukulie hili suala kwa uzito, lakini pia Mwalimu aliyetishiwa na diwani ni vyema abadilishiwe kituo cha kazi.
Wananchi adui wetu sio Mwalimu bali ni wale viongozi wanaoficha ukweli na kuzuia haki, adui wa Ikunguigazi ni yule aliyepewa dhamana ya kusimamia maendeleo lakini ameshindwa badala yake ana kimbizana na Mwalimu wakati sisi nzengo tunajua kila kitu.