kuzaliwa kwenye kahawa si kigezo pekee cha kufahamu kilimo cha kisasa juu ya kahawa.
kama anataka kujifunza kilimo cha mazoea basi anaweza kuwauliza wenzake lakini kama anahitaji kilimo cha kisasa na chenje tija watalamu waliosomea juu ya hayo maswala wapo anaweza kuchukua ushauri toka kwao.
Nikuhakikishie tu uwezekano wa kufaulu katika kilimo hicho ni mdogo sana akiwasikiliza hao watampa elimu ya kwenye karatasi isiyokuwa na uhalisia na mavuno hewa ambayo hatayapata kamwe.
Nachosema Mimi na uhakika nacho 100% otherwise akutane na Bw kilimo anayelima na analijua zao husika!!
Nimetoka kulima nyanya Hivi karibuni na mtaalamu(Afisa kilimo) aliyesomea Tena SUA alikuwa na shamba lake. Jirani mwendo kama wa dk27 kulifikia shamba lake Kwa mguu.
Kipindi tunaandaa shamba aliletwa na mzee Ili atupe ushauri kuanzia space ya mashimo nk
Upande wa mbegu pia alitushauri Kwa kutusisitiza tutumie mbegu 1 anayo ijumaa yeye na aliyoilima yeye.
Lakni katika ushauri wote alioutoa nilikuja kuchukua 1 namna ya ufungaji na wenyewe anadai aliona mtandaoni
Tukija kwenye mavuno nilimuacha mbali mno yaani Hadi akawa hafiki Tena shamban kuja kunishauru kitu tangu tu nyanya umeanza kubeba!
Wateja wake walimuhama wote japo Mimi nilikataa kuuza rejareja.
Itoshe kusema wataalamu wetu hawana uzoefu hata wenye kulima Bado wanalima Kwa kuangalia kwenye daftari alicho kopi chuoni kwake ndo anakileta shambani.
Nyanya zake zilipigwa bottom vibaya mno matunzo hafifu elimu ya kilimo Dunia ya kwenye makaratasi na Tena zilibanana mno (cm30 shimon na shimon na cm40 mstari na mstari) na alitukomalia mno tuchimbe umbali huo huku akitupa mifano kadhaa akichimba mwenyew!!!
Kwenye kuku pia niliwahi kukutana na kimeo huyu yeye anadai ana diploma yake kwenye mifugo.
Mbaya zaidi Hana hata kuku mmoja Wala mbuzi ama mbwa kwakwe magonjwa anayajua tu kupitia kwenye notice alizoandika shuleni hajawahi kuona inakuwaje!!
Nilifika nikamwelezea jinsi kuku wangu wanavyoumwa hata sijamaliza Tyr kashanipa dawa katumie hii hapa
Nikamuuliza inatibu nn? Akajibu ugonjwa fln nikamwambia mbona kuku haumwi ugonjwa huo na dalili za ugonjwa na nilizotaja ni tofauti akaanza kujikanyaga.
Mwisho nikagundua hakuna ajuacho huyu jamaa.
Nikamuuliza una dawa inaitwa × na Y akajibu ndio nikamwambia naomba hizo ndo zinatibu ugonjwa niliokuambia.
Naomba usome pia zimeandikwa hivyohivyo Tena Kwa kiswahili na dwa uliyonipa inatibu kipindupindu Cha kuku Wala sio kuhara damu na mafua!!!
Visa ni vingi mno na siwaamini kabisa kwani mwanzo walinitia hasara kubwa mnoo heri niende Kwa mfugaji/mkulima mwenzangu aliyefanikiwa zaidi akiwa Hana kinyongo lazima anipe Siri hii.