Mbolea ipi ni nzuri kwa kupandia mahindi DAP vs NPK

Asante mkuu ngoja safari hii nitumie DAP pekee ukizingatia mbolea zenyewe sasahiv bei zipo juu

Mkuu kwa viazi mvringo kama unataka matokeo mazuri ni vema uendelee kuchanganya DAP+CAN.
Dap- inafanya vema sana kwenye mazao upande kwa kupandia
Urea- inafanya vema sana kukuzia
Can- inafanya kazi ya kuzalishia

Kwa hiyo ili viazi vizae vema na kuwa vikubwa vinahitaji CAN ndo maana wenyeji wako ambao kimsingi ndo wataalam no.1 wa Kilimo wamekuwa wakifanya hivyo. Amini usiamini mkulima ndiye mtaalam wa kwanza wa Kilimo.
 
Nim
Nimekupata vyema mkuu.
Ubarikiwe
 
Yaani msoto na sapu za SUA,unasema mkulima ndo mtaalamu no Moja??serious[emoji1787][emoji1787][emoji1787] W
 
DAP ni ya kupandia, NPK ya kukuzia. kwenye NPK nitrogen ni specifically kwa kuboresha ukuaji wa majani hizo phosphorus na kalium zote zinahitajika kwenye kusaidia mimea iote vizuri from seeds to seedlings
Sio kweli.mbolea za kupandia ni DAP,NPK,MOP,Minjingu,na nyingine zenye ingredient za phosphorus.
 
NPK ni complete fertilizer hivyo basi ina virutubisho vyote NITROGEN, PHOSPHORUS and POTASSIUM. Basi kwa vigezo hivyo anaweza kuitumia kwa namna yoyote ilimradi kuzingatia asilimia za mbolea husika.
Naam.
 
Miti ya matunda iliyodumaa ikiwa shambani, ambayo inashindwa kukua kwa kasi sawa na mingine naweza kuweka pia mbolea ya kiwandani kuikuza?
Samadi tu inatoshs au mbolea za kwenye majani au mfumo wa maji maji zina NPK ambayo N ni kubwa kwa kuamsha mfumo wa mmea
 
SAMADI kwani ina virutubisho vyote!
Ina virutubishi awali ambavyo ni NPK na hutoa taratibu saba hayo madini na hukaa kwa muda mrefu sana bila kuleta madhara.

KUMBUKA
mbolea iwe kavu kipindi cha kutumia
 
Mbolea ipi ni nzuri kwa kupandia mahindi. Na kwanini iwe X na sio Y
NPK ndiyo mbolea nzuri zaidi kwasababu ni Complete fertilizer,ina Nitrogen,Phosphorus na Potassium.Lakini pamoja na hayo ni muhimu kupima udongo wa shamba lako maabara ili kujua mahitaji sahihi ya shamba lako.Kusema tu kuwa tumia NPK bila upimaji wa udongo,hiyo ni blank recommendations,it's very local not scientific and technical.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…