Ndugu zangu naomba ushauri kwenu maana mimi sasa nashindwa nitumie mbolea ipi. Kwa kifupi mwaka juzi nilitumia Dap ilinipa matokeo mazuri, mwaka jani nikaambiwa Yaraceitirio nikatumia sikupata mafanikio mazuri ingawa na mvua ilikuwa changamoto.
Sasa msimu umeanza ndio nataka kuingiza trekta sasa sijajua nitumie mbolea ipi kwa kupandia huku Kanda ya Kati kuna Cap, Yara Otesha,Yara Mila, Yara Ceitrio, Yara Java nk.
Mbegu natumia Zamseed.