SoC02 Mbolea yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha zaidi ya magunia 150 ya mazao mbalimbali kwa Ekari moja

SoC02 Mbolea yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha zaidi ya magunia 150 ya mazao mbalimbali kwa Ekari moja

Stories of Change - 2022 Competition

Esak

Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
9
Reaction score
10
Kutokana na kupungua kwa rutuba kwenye udongo imesababisha upotevu wa madini mbalimbali ambayo ni muhimu katika ukuaji na afya ya mmea mfano wa madini hayo ni fosfeti, naitrojeni, chuma, potasiamu, fosforusi na kalsium, hali hii imepelekea uzalishaji wa mazao ya biashara na kilimo kuwa duni na ukizingatia kilimo ni sekta muhimu nchini Tanzania na Asilimia kubwa ya watu waishio nchini wanategemea kilimo katika kuingiza kipati Chao cha kila sku

Katika kukabiliana na changamoto hii, jibu lake au suluhisho ni kama ifuatavyo
KUANZISHA MATUMIZI YA MBOLEA YENYE VIUMBE HAI WADOGO SANA( BAKTERIA) , kwa lugha ya kibailojia ni Biofertilizers.

Biofertilizers ni nini? Inatengenezwaje? Mahtaji yake ni yapi? Kwa kutumia teknolojia ipi? Kwa mazao gani na kivip inafanya kazi? umuhimu wa kipekee ni upi? na MATUMIZI yake ni yapi?

Ili kujibu hayo maswalii yote ungana NAMI kufuatilia Uzi huu muhimu sana
Biofertilizers ( mbolea bacteria) ni mbolea ambazo Zina viumbe hai wadogowadogo ndani yake mfano BAKTERIA, virusi na fangasi ambazo zinasaidia katika ukuaji wa mimea kwa kuongeza upatikanaji wa chakula au madini muhimu katika ukuaji na afya ya mimea, mbolea hii ni mahususi li kukabiliana na matokeo hasi yatokanayo na MATUMIZI ya mbolea za kikemikali mfano kuacha qsidi na chumvichumvi shambani , kwa hiyo mwendelezo wa matumizi ya mbolea hizi huongeza rutuba na upatikanaji wa chakula muhimu katika ukuaji wa mimea

UTENGENEZAJI
Mbolea hii hutengenezwa maabara kwa kutumia bayoteknolojia ambayo kwa lugha nyepesi ni teknolojia inayohusisha UTENGENEZAJI wa bidhaa mbalimbali kutoka kwa viumbe hai ambazo ni za muhimu kwa matumizi ya binadamu katika sekta ya afya, kilimo, viwanda na mazingira kiujumula. UTENGENEZAJI wa mbolea hizi inahtaji uwepo wa wataalamu wa biyoteknolojia na maabara za kisayansi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa hii adhimu.

Hatua katika UTENGENEZAJI wa mbolea hizi ni kama ifuatavyo

1. Uoteshaji wa Bakteria ambao ni muhimu katika teknolojia hii mfano wa hao Bakteria ni kama Rhizobium, Azotobacter, pseudomonas, Azospirillium na Bakteria wenye uwezo wa kuvunja vunja au kubadlisha fosfeti na potasiamu, kuotesha kwa lugha ya kitaalam tunaita culturing of bacteria.

2. Utenganishaji wa Bakteria baada ya kuotesha Ili kupata Bakteria husika kwani katika kuotesha wanaweza wakaota Bakteria wa aina nyingi ambapo wengine so muhimu katika kutengeneza mbolea hii.

3.uwekaji wa Bakteria kwenye vifaa maalumu viitwavyo fermenter ambavyo vinasaidia upatikanaji wa Hali na Mazingira katika ukuaji wa Bakteria hao Ili wasife.

NB: mbolea hizi zinaweza kutengenezwa katika Hali mbili ambazo ni katika yabisi na kimiminika itategemeana na aina ya mazao, Hali ya hewa na gharama za utengenezaji.

4. Upakiaji na ujazaji wa mbolea hizi hutumia mashine maalumu ambayo hujaza na kuacha nafasi kwa ajili ya hewa ( kwa mbolea za kimiminika zinazowekwa kwenye chupa ) na zilizo katika yabisi huwekwa kwenye pakiti maalumu Ili kubaki muda mrefu( long shelf life) bila kuharibika.

5: kukaguliwa kwa mbolea Bakteria kwa kuangalia viwango na ubora kutoka mamlaka husika mfano kwa TANZANIA ni kupitia shirika la viwango na ubora Maarufu kama Tanzania Bureau of Standards ( TBS).

AINA ZA MBOLEA BACTERIA
# Mbolea zinazosaidia upatikanaji wa naitrojeni( nitrogen fixing bacteria fertilizer),
Hizi husaidia upatikanaji wa naitrojeni kwenye udongo kwani Bakteria waliopo kwenye mbolea hii hubadlisha nitrites kuwa nitrates ambazo ni muhimu katika kurefusha na kutengenezwa kwa protin zinazosaidia kwenye ukuaji wa mme.

Mfano wa Bakteria katka kundi hili ni Rhizobium ambayo hutumika kwenye mimea jamii ya mikunde, Azotobacter ambayo hutumika kwenye alizeti, maua, nyanya , miwa na matunda ya aina zote, Azospirillium hutumika kwenye mazao yote ya nafaka.

#Mbolea zinazosaidia upatikanaji wa potassiamu na fosfeti
Kikawaida fosfati na potasiamu zilizopo kwenye udongo zipo katika Hali ya yabisi na hivyo ni ngumu kutumiwa na mmea hivyo Bakteria kama pseudomonas, Azospirillium na bacillus hufanya kazi ya kubadlisha madini hayo yawe katika Hali ya kimiminika Ili yaweza kusharabiwa na mmea na hatimaye kutumika katika ukuaji na maendeleo ya mmea.

NAMNA YA KUTUMIA
Hapa nimeeleza mifano michache ya mazao Maarufu na namna ya kutumia mbolea Bakteria
# matumizi kwenye mbegu za nafaka:
Gram 200 za mbolea Bakteria zinachanganywa na Mls 40 za maji na kuweka kilogram 10-12 kwenye mchangangiko huo, na kusubiri dakika 30 tayari kwa kupandwa,

#matumizi kwenye mazao kama miwa
Andaa vipande vya miwa kwa ajili ya kupanda, gram 200 ya mbolea Bakteria na maji Lita 15 changanya na uweke vipande vya miwa kwenye mchangangiko huo.

#Matumizi kwenye mazao ya kupandikiza mfano nyanya:

Changanya kilogram 1 ya mbolea Bakteria na Lita 15 za maji na uweke maotea hayo kwa dakika 15

#Matumizi kwenye udongo

Changanya Gram 700 za mbolea Bakteria na kilogram 80-120 za samadi, udongo unakuwa tayari kwa kupandwa mazao

UMHUHIMU WA MBOLEA BAKTERIA
1: Kuongeza uzalishaji wa mazao kwa Asilimia 20-40%
2.Inatumika kama mbadala wa mbolea za kikemikali ambazo Zina matokea hasi
3. Zinarudisha au kuongeza rutuba kwenye udongo
4. Zinaepusha uchafuzi wa mazingira.

Ahsante sana 🙏🏼
Naomba Kura yako na Mungu akubariki
 
Upvote 14
Sawa mwanasayasii, naona una content nchi iwatumie VIJANA kama ninyi
 
Back
Top Bottom