Mbona akiwa mbalamwezini huanzisha mazogo?

Mbona akiwa mbalamwezini huanzisha mazogo?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Mdada kuwa mbalamwezini ni kutii amri ya asilia.
Mie sina kinyongo naelewa ni matakwa ya Muumba.
Walakini anapozua mazogo mie huwa nataabika.
Natamani apite mwezini kwa shwari bila kunitaabisha.
Mbona akiwa mbalamwezini huanzisha mazogo?

Naelewa kero za mbalamwezini pengine kumbughudhi.
Khali yake kubadilika na kujiona pengine hapendeki.
Tumbo kumdodosa na hulazimishwa kujichunga na khali.
Akikhofu zege lisim'minike basi hujisitiri kwa nepi.
Mbona akiwa mbalamwezini huanzisha mazogo!

Kabla na baada ya siku zake vicheko humtawala!
Hiyo khali kunisuuza roho yangu na kulifaidi penzi letu.
Lakini akikamatwa na mbalamwezi huwa mkali mithili ya mbogo!
Sijui huhofu nini kwani mie sina mpango wa pembeni.......
Mbona akiwa mbalamwezini huanzisha mazogo?

La ajabu akimaliza siku zake hunitaka yote yaishe!
Mkakati wake ni kunitongoza hatimaye kunikagua!
Bahati njema huwa sijaguswa na huduma safi kumpatia!
Vifijo na nderemo kunishushia lakini msamaha huwa sipewi!
Mbona akiwa mbalamwezini huanzisha mazogo?
 
Ruta siku hizi naona unatoka kishairi zaidi! Kunani nyuma ya hili?


Mimi nafikiri kila mwanamke ana namna yake 'akiwa mbalamwezini'. Wengine wala huwezi jua maana wanabehave normal tu...ikitokea ukaomba mchezo ndio unajua kuwa mambo si shwari siku hiyo!
 
Rutaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,.......................... yaani umenifanye nivunje mbavu but real i admire you i wish...................

lkn ujue hizo ni hormones ambazo huja na effects zake pia.
 
Mie wala siumizi kichwa najua she will face consequences in my turn....................LOL

Miaka ya hivi karibuni imegundulika kwamba hata wanaume hupata hedhi-ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

Kwa karne na karne hakuna mtu aliyekuwa akifikiria kwamba wanaume wangeweza kuwa wanapata nao hedhi kama wanawake. Kama mwanaume akiamua kuweka kumbukumbu zake kwenye dayari na kujiangalia kila siku hali yake inavyobadilikana kuwa ya kusikitika, ya kawaida, furaha na hasira……akiifuatilia hali yake namna hiyo kwa siku zote 28 za mwezi, halafu na mwezi unaofuata, akafanya hivyo hivyo, halafu mwezi wa tatu nao akatenda hivyo, na halafu ailinganishe miezi hiyo mitatu atashangaa.

Kuna siku tatu, nne au tano ambazo zitafanana katika dayari zote tatu, lini ana hasira ana masikitiko, ni mharibifu, na tabia nyingine kama hizo. Hivyo ndivyo vipindi vya hedhi kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake. Zoezi hili anaweza kufanya mwanaume yeyote, akishindwa kupata matokeo anaweza kuwasiliana na mimi na kuuliza ni kwa nini nimeandika uongo.

Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi na sababu ziko wazi: mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi, na mwanaume ana asili ya ubongo zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.

Na kama umejaribu kujichunguza kwa mwaka mzima, utashangaa kwamba, ulikuwa na hasira mgomvi, mwenye huzuni na vingine vya aina hiyo, si hivihivi tu bali ni kwa sababu ulikuwa kwenye hedhi. Kama ukishafanya zoezi nililokwambia la dayari, jiulize, kama ulipokuwa kwenye hali hizo ulikuwa umekerwa na yeyote au chochote. Utagundua kwamba hukuwa umekerwa bali ulikuwa unasumbuliwa na hedhi yako.

Ina maana basi kwamba mwanaume naye ni lazima kila mwezi awe na mabadiliko ambayo yatamfanya aingie mahali ambapo atavutana na mwanamke kimapenzi. Hili ni suala la maumbile ili kufanya kuzaliana kuwepo. Utajuaje kuwa mwanaume ameingia kwenye hali hiyo? Ndiyo pale ambapo wataalamu wamegundua hizo siku nne au tano za mabadiliko ya kiakili kwa mwanaume!



https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/160184-kumbe-wanaume-nao-huingia-katika-hedhi.html

 
Ruta siku hizi naona unatoka kishairi zaidi! Kunani nyuma ya hili?


Mimi nafikiri kila mwanamke ana namna yake 'akiwa mbalamwezini'. Wengine wala huwezi jua maana wanabehave normal tu...ikitokea ukaomba mchezo ndio unajua kuwa mambo si shwari siku hiyo!

SMU uko sahihi.........hapa ninawagusa wale ambao hupatwa na "Mood swings" wakishikwa na mbalamwezi..................
 
Last edited by a moderator:
Ruta wa BK the home of Tibaijuka and msemakweli.

King Kong III you can say that again..................I hope she will ascend to presidency..............not because she is my sister but because she fears God.............
 
Last edited by a moderator:
Most of them wako hivyo.So keep life goes on

Mzinga sijui wako wapi........................naona wameingia mitini baada ya kujua kumbe nasi huwa tunawasoma kama wao wanavyokazana kutusoma......................
 
Last edited by a moderator:
Mie wala siumizi kichwa najua she will face consequences in my turn....................LOL

Mtambuzi................tit for tat never works.....................an eye for an eye is too painfully for both of you.....................best solution is learning how to cope with her swing moods and hoping she may also learn how to endure yours too..........
 
Last edited by a moderator:
Rutaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,..... ..................... yaani umenifanye nivunje mbavu but real i admire you i wish...................

lkn ujue hizo ni hormones ambazo huja na effects zake pia.

gfsonwin.....................You wish what.........................say what you wish and wish what you say...........
 
Last edited by a moderator:
Ruta,kipindi hicho panakua hapatoshi full kutunisha mashavu.

promiseme......tunachotakiwa kufanya ni kufanya jitihada zote kuelewana sababu za mitafaruku ya namna hii ili kuirekebisha au kuivumilia kama tumeshindwa kuirekebisha..........
 
Last edited by a moderator:
RUTA mbavu sina ,zimekatika kwa kucheka, yaan inategemea wengine inakuwa ugonjwa taabani,kitanda unaona ndio starehe yako hahahaaa
 
Back
Top Bottom