Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Nchini Kenya muswada wa fedha ulizua balaa huku wachumi wakiuchambua kila kipengele na kuelezea athari zake kwenye uchumi wa Taifa na mwananchi mmojammoja.
Huku kwetu wametuita Dodoma tena wametupa siku mbili, hamna anayeuongelea. Mwendo wa HS code kwenye muswada, wachumi wetu wako wapi kutusaidia kuelewa umemaanisha nini, athari na faida zake!
Nimeona wafanyabiashara wa Kariakoo wameuweka kwenye madai yao matano japo wamepigwa siasa wakaonane na kamati ya kuchukulia maoni, wananchi hawana madai!
Nimepitia umeleta kodi na tozo tele ikiwemo kwa watengeneza maudhui mtandaoni lakini wameshindwa hata kutengeneza maudhui na kueleza athari zake kwenye mitandao, eneo ambalo wanalimudu vizuri, pia nimeona tozo kwenye gesi asilia na nyinginezo.
Tunasubiri July mosi ukianza kutumika tulie lie mitandaoni huku maamuzi yashafanyika na ngumu kuyabadilisha na maandamano yanayobadilisha maamuzi ndio kitu tumeshindwa, labda wafanyabiashara watoneshe njia.
Pia Soma=> Serikali yaandaa Mkutano wa Siku 3 kwa Wadau kutoa Maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2024