Mbona hawa Askari wanatamba nchi nzima?

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2021
Posts
484
Reaction score
545
Hivi Kingai, Godluck, Mahita, D/C Msemwa, Afande Jumanne, Minja na Afande AZIZI, Hawa ni askari huru wa polisi wakuzunguka nchi nzima na kukamata?

Maana hata wakuu wa Vituo wanakowapeleka hao walio kamatwa hawana sauti.

Je, tuseme mikoa haijajitosheleza kuwa na askari wapelelezi?

Mbona hawajamaa wanatamba nchi nzima. Imekaaje hii. Napata Kigugumizi. Na huo ukamataji ni wa kisheria au wao ndio wenye nchi?
 
Swali hili nimejiuliza muda mrefu sana,

Na hili linaleta ukakasi kwenye hii kesi

Anyway,pengine ni mpango maalumu
Ujue kila mahala,Mdude kawataja,kwenye hii kesi wanalalamikiwa,hatujui kuna wengine watakuja na kuwataja,Namuomba Mkuu wa Polisi Tanzania,ajaribu kuwapunguzia hawa mabwana majukumu,hawa ni binadamu,wana familia,watajengewa chuki na hao walio watesa nakufanyiwa visa.

Wao ndio Askari lakini familia zao sio askari,huwezi kuwalinda wote kwenye familia yako wakiamua kulipiza visasi.Chonde chonde Mkuu, hebu wapunguzie majukumu.

Pia mkuu hebu wape heshima makamanda wa Vituo vya mikoani,just kuwaambia wanatafutwa fulani na fulani,tunaomba muwakamate, sio mpaka mumtume Mahita au Kingai.
 
Tanzania Bila Serikali inaweza kujitawala tu na mambo yakaenda ilmradi uwepo wa Mungu uendelee kutamalaki na mabeberu wasiache kutusaidia baas we will survive.
 
Huo ndio utawala wa Siro. Polisi wamekosa credibility ya kuwa chombo cha kulinda raia na mali zao.

Hat haya mambo sijui majambazi wameuawa mara kakamatwa na bangi huu wote ni kugushi. Polisi ni kikosi cha majambazi.
 
Hao ni Mashujaa, yaani Polisi ukisikia mtu anaitwa shujaa jua huyo ni katili aliye tayari kuumiza/kuua bila kujali utu.
 
Hao nahisi ni kama vile vikosi maalum vya Bashite.
 
Ujue kila mahala,Mdude kawataja,kwenye hii kesi wanalalamikiwa,hatujui kuna wengine watakuja na kuwataja,Namuomba Mkuu wa Polisi Tanzania,ajaribu kuwapunguzia hawa mabwana majukumu...
Kama siro ndio kawatuma je utajuaje
 
Huyu Azizi huwa kama Shombe Fulani hivi!
 
Hicho ni kikosi kazi cha CCM
 
Hii kesi ilipangwa na kusukwa kule moshi na kundi la jambazi sabaya akishirikiana na wahuni flani wakati wa mwendazake!

Iliwekwa kapuni na mwendazake baada kuonekana ushahidi ni wa hovyo! Awamu ya 5 wakampachika mama nae akalivaa kwani sio mtu wa kuhoji ndio kinachoendelea huku wao 'watunga kesi' na mawakili wao wakila per diem na posho kibao kodi za walipa kodi kwa uhuni wa kutisha.
 
Kama ulikuwa hujui hawa ndo Wale 'wasiojulikana'
 
Hao vijana walikuwa wanatekeleza ilani ya yule hayati wa Chato ya kuumaliza upinzani kabla ya 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…