OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Kichwa cha habari hapo juu chajinyumbulisha. Katika miaka yangu ya kufuatilia soka sijawahi kusikia popote duniani club ya soka inaendeshwa kwa bakuli style wanayofanya Yanga.
This is too much!
Sisikii kina Lipuli wakizungusha bakuli kama ambavyo wanafanya Yanga mpaka kufikia kiwango cha kuingia na kapu uwanjani. Fikiria Yanga wanacheza na Mbao FC pale Kirumba halafu Yanga timu kubwa na kongwe inaingia na kapu uwanjani,sio kwamba Mbao ndio walipaswa kupitisha kapu?
Ninafahamu kina Stend,Ndanda nk wanaendesha timu kupitia michango ya wadau wao wa karibu kama wafanyabiashara nk. Tulisikia Homonizer aliichangia Ndanda timu ya kwao. Lakini hawajafikia kiwango cha Yanga kutembeza kapu viwanjani.
Yanga wanae mdhamini ambaye ni Sportspesa na dau lake ni zaidi ya bilioni 2 kwa mwaka. Inayo wadau wafanyabiashara kama kina Manji nk. Ina mashabiki wengi ambao wanaweza kuhasishwa kuchangia timu kupitia viingilio na T-shirt.
Ajabu ndio timu pekee iliyogeuka mlemavu na ombaomba.
Nasikitika napowaona kina Ajibu na Kamusoko wakipita kwenyie TV kuomba michango. Huu ni udhalilishaji.
Mmewatia unyonge mashabiki kiasi cha kuwa na wivu kupindukia na mafanikio ya Simba SC badala ya kuwa na wivu wa maendeleo
Umefika hatua Yanga inagombana na wachezaji kila wanapodai chao kwa kisingizio cha nidhamu. Halafu watu hawahawa mnategemea kushindana na mabingwa Simba Sc