Mbona Lipuli, Singida Utd, Stend Utd, Ndanda nk hawatembezi bakuli kama Yanga SC?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Kichwa cha habari hapo juu chajinyumbulisha. Katika miaka yangu ya kufuatilia soka sijawahi kusikia popote duniani club ya soka inaendeshwa kwa bakuli style wanayofanya Yanga.

This is too much!

Sisikii kina Lipuli wakizungusha bakuli kama ambavyo wanafanya Yanga mpaka kufikia kiwango cha kuingia na kapu uwanjani. Fikiria Yanga wanacheza na Mbao FC pale Kirumba halafu Yanga timu kubwa na kongwe inaingia na kapu uwanjani,sio kwamba Mbao ndio walipaswa kupitisha kapu?

Ninafahamu kina Stend,Ndanda nk wanaendesha timu kupitia michango ya wadau wao wa karibu kama wafanyabiashara nk. Tulisikia Homonizer aliichangia Ndanda timu ya kwao. Lakini hawajafikia kiwango cha Yanga kutembeza kapu viwanjani.

Yanga wanae mdhamini ambaye ni Sportspesa na dau lake ni zaidi ya bilioni 2 kwa mwaka. Inayo wadau wafanyabiashara kama kina Manji nk. Ina mashabiki wengi ambao wanaweza kuhasishwa kuchangia timu kupitia viingilio na T-shirt.

Ajabu ndio timu pekee iliyogeuka mlemavu na ombaomba.

Nasikitika napowaona kina Ajibu na Kamusoko wakipita kwenyie TV kuomba michango. Huu ni udhalilishaji.

Mmewatia unyonge mashabiki kiasi cha kuwa na wivu kupindukia na mafanikio ya Simba SC badala ya kuwa na wivu wa maendeleo

Umefika hatua Yanga inagombana na wachezaji kila wanapodai chao kwa kisingizio cha nidhamu. Halafu watu hawahawa mnategemea kushindana na mabingwa Simba Sc
 
Matumizi mabaya ya hela,wachezaji wa Yanga wanaishi hotel ya Nefaland, chumba elfu 50 hadi 90 kwa siku, je kwa mwezi wanatoa kiasi gani na wapo wangapi,jioni utakuta wamejazana reception na jopo la viongozi.

Yanga kuna ubadilifu unaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lodge za 30,000 zina ubaya gani?
 
Wadhamini wakuu wa klabu za Simba na Yanga, Kampuni ya SportPesa, imeahidi kutoa kitita cha shilingi za kitanzania, milioni 50 kwa timu ya Simba.

Fedha zinatolewa zikiwa mahususi kwa ajili ya kuipa hamasa Simba kutokana na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wake hapa nchini, Abbas Tarimba, amesema kutinga kwa Simba katika hatua hiyo kubwa ni jambo la kujivunia kwa Simba na taifa kwa ujumla.

"Kufikia hatua ya kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika si jambo dogo, unaweza kuona Simba wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao.

"Hii imeweza kutoa heshima si kwa Simba pekee bali taifa kwa ujumla.

"Sisi kama SportPesa tutatoa kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 50 kwa Simba kuingia hatua ya robo fainali, Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Tunapongeze Simba, wachezaji pamoja wa wanachama wake kwa kuisaidia timu kutinga hatua hii, ni fahari kubwa kwetu kama SportPesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kwa sport pesa ni sahihi kabisa kufanya hivyo kwa sababu tayari simba tayari inaitangaza sport pesa kwenye mataifa mengine kama vile, Zambia, Congo, Algeria, Misri na yawezekana katika hatua hii ya robo fainali wakaitangaza zaidi hadi katika nchi za tunisia na morroco kama simba itapangwa na moja kati ya timu za esparence au raja casabranca.
Lkn majirani wameishia kuitangaza sport pesa kwenye mikoa ya kusini, kaskazini, magharibi, mashariki na ukanda wa pwani na kati. (pima utofauti hapo)
 
nafikiri hata Yanga kufungwa na Iipuli ni sababu ya mgogoro Unaendelea. Haiwezekaji Kocha na mchezaji wawe uwanjani halafu hapo hapo wanasimamia ela lazima italeta maswali kwa wadau wengine. Timu ikiwa na waamuzi wengi kwenye mambo ya ela inakuwa na Walafi wengi inaleta mgogoro. Hii problem isingekuwepo kama manji ni mwenyekiti pengine s sasahivi Yanga angeshatangaza ubingwa.
Angalia Real Madrid au man United wenye hisa kubwa ndiyo ndiyo wenye maamuzi yote.
Migogoro ya Vilabu haileti faida kwa timu ya taifa. Tff ilitakiwa iwaachie Yanga wamalize matatizo Yao wenyewe isiwe ndiyo inakoleza mgogoro.
 
Ukishakuwa na hulka ya kuomba omba huwezi kuacha, ndo maana omba omba wengi mjini unasikia amejenga, ana malori, ana daladala lakini kutwa nzima anaomba hajali kiasi gani hata Sh 10/= anapita nayo na Yanga hata waje wapate mwekezaji kama dangote au hata boss wa man city aje awekeze yanga hawataacha kuomba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…