Mbona madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake wengi wao ni wanaume kulikoni!?

Mbona madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake wengi wao ni wanaume kulikoni!?

Dumelambegu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
1,052
Reaction score
257
Ni kajiswali kakizushi tu! Naona kama kuna marupurupu fulani wanayoyakimbilia wanaume. Ingependeza zaidi endapo madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake wangekuwa wanawake wenyewe.
 
Elimu ya udakitari ni ngumu, inahitaji watu wenye uelewa mzuri wa masomo ya sayansi na inachukua muda mrefu kuipata. Wanawake wengi hawapendi masomo ya sayansi kutokana na changamoto zake na hii ni kwa mataifa yote duniani japo kwenye nchi masikini hali ni mbaya zaidi.
 
Umeenda mbali sana cha kujiuliza ni kwamba kwa nini wasichana wanaochukua masomo ya sayansi A level ni wachache ? Then jibu litumie kwenye swali lako.
 
Dada zetu wanataka kuwa Ma-First Lady, Ma-Miss, na kufanya kazi kwenye mabenki.
Na sasa limeshaongezeka la WABUNGE WA VITI MAALUM . . .

Utajisikiaje pale mkeo anapokusisitiza kwamba CPU ndio daktari mzuri wa kumtibu maradhi yake, mpole, msikivu, mkarimu, muelewa na anaijua kazi yake vizuri. Na akakushauri umpeleke kwa CPU akatibiwe tena???
 
Masomo hayo wanawake wengi twayakimbia, ila wapo wachache kama mama masawe pale moroco
 
Dada zetu wanataka kuwa Ma-First Lady, Ma-Miss, na kufanya kazi kwenye mabenki.
Na sasa limeshaongezeka la WABUNGE WA VITI MAALUM . . .

Utajisikiaje pale mkeo anapokusisitiza kwamba CPU ndio daktari mzuri wa kumtibu maradhi yake, mpole, msikivu, mkarimu, muelewa na anaijua kazi yake vizuri. Na akakushauri umpeleke kwa CPU akatibiwe tena???

dah! kaazi kweli kweli!
 
Ki ukweli wanawake wengi hupenda kutibiwa magonjwa yao 'ya kike' na madaktari wanaume, huwa free sana kujieleza kwa wanaume kuliko wanawake wenzao. Nadhani hii ni ya kisaikolojia zaidi......
 
Back
Top Bottom