Mbona naona kama M23 ndio mkombozi wa wananchi na Kagame ni shujaa?

Mbona naona kama M23 ndio mkombozi wa wananchi na Kagame ni shujaa?

felakuti

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
659
Reaction score
1,207
Leo katika pitapita zangu mahali nikakuta documentary inayoelezea machafuko ya huko Congo, kuanzia chimbuko

Kwa kifupi nilichokuja kugundua baada ya muda mrefu kuwaza kua sababu ni nini huko mbona damu inamwagika sana, inakuaje wanajeshi wa nchi husika (Congo) wanaua wananchi wake na kubaka akina mama na mabinti, na wazee?

Je uhasama wa wanaosemekana ama kuitwa waasi na jeshi ni nini Hadi jeshi wawaue wananchi na kusingizia kua ni "waasi"? Je hao waasi wameasi nini Hadi jeshi la Congo liwaue wananchi na kusingizia ni waasi?

Hata baadhi ya magenerali waliohusika na machafuko ya kuua raia, kubaka, kulawiti, wamepandishwa vyeo huko jeshini Congo, namuona hapa mmojawapo wamemuonesha kwenye documentary hio

Baada ya haya yote Sasa sauti zinaanza kupazwa na familia za waliouawa na jeshi la Congo kudai na kutaka Haki, wengi wanaishi na majeraha makubwa sana moyoni na makovu ambayo hayatawahi kufutika kirahisi

Ndio hapa wanapokuja M23, Hawa wamekuja ama walianzishwa kwa ajili ya kulinda wananchi wa maeneo husika yaliyokumbwa na mauaji kipindi Cha nyuma, Cha ajabu sisikii kama wanaua watu, unasikia Kuna vifo vya watu na wao ndio wanasingiziwa kua wameua, ila ukweli ni jeshi..je kwanini..kama.ni kweli bwana Kagame anawafadhili kwa nilichoona na kugundua nasema Kagame ni shujaa na mzalendo wa kweli.

Bado naendelea kuchimbua kwamba ni nini ambacho jeshi wanalinda ama kukitaka ambacho wako tayari kuua raia wake, na ni kitu Gani M23 wanalinda kwa ajili ya wananchi wake.
 
Zaidi ya kukata mauno na kupaka mkorogo Wacongo hakuna kingine wanachoweza
 
Back
Top Bottom