Mbona Paul Scholes anamchukia Mourinho bure?

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
8,082
Reaction score
17,838
Yani jamaa hafichi chuki zake kwa special one. Hata walivyomfunga juve jamaa bado anamponda tu utadhani alitamani mani wafungwe.

Mimi si shabiki wa Mani ila nawaombea washinde. Tena wawafunge Man City wikendi hii ili huyu red head Scholes akate ngebe
 
Scholes anaongea uhalisia wa mambo jinsi ulivyo. Kwenye soka uliweka ushabiki kando lazima uende na facts.

Hata kama Man United amemfunga Juve ila Scholes hawezi kuwa mnafiki asiponde kuwa team haipo vizuri.

Angalia tokea game na Bournemouth last weekend, Man U imekuwa inashinda kwa ngekewa tu tena same same kind of wins. Leo wamepata magoli mawili yote from set pieces. Juve wame create so many chances ambazo kwa clinical finishers mpaka wakati Man U wa score first goal basi angekuwa labda ashafungwa 3 au 4.

Mpira ni mchezo wa makosa na Man U wanastahili pongezi kwa ushindi vs Juve. Hii haindoi ukweli kwamba bado team ni mbovu na haina mbinu za kushinda mechi kama siku za nyuma. Mourinho anatakiwa ajitathmini maana kundi la wachezaji alionao sio wabaya ni wachezaji wanaojua sana tu.

Mshabiki wa damu wa Liverpool.
 
Zamu yako itafika tu
Vijana wa jose hawawezi kumuacha klop lazima wapite nae
 
Mkuu vipi sasa liver mlivyoaibishwa na vibonde Belgrade na huenda labda umsifuzu next round
 
Mkuu vipi sasa liver mlivyoaibishwa na vibonde Belgrade na huenda labda umsifuzu next round
Kibonde yupo CL? Kuweni na heshima kwa team zinazojua. Kufungwa kawaida tu. Mbona nyie jana mmemfunga Juve bila kutarajia?

We had one off day. That's it.
 
Hao wapiga domo wakikabidhiwa timu wanapata shida sana. Mwenzake Henry hata akirudi kwenye uchambuzi leo hii akili itakuwa imemkaa vizuri.
 
Hao wapiga domo wakikabidhiwa timu wanapata shida sana. Mwenzake Henry hata akirudi kwenye uchambuzi leo hii akili itakuwa imemkaa vizuri.

Hahaha umemsahau na Gary neville alivopewa valencia ilikua ni vipigo tu
 
Wale wachezaji wa zamani wa man united wanaotokea UK huwa wanadhani kama Man united ni timu yao peke yao... Kuna huyo boya scholes, boya giggs, boya Rio Ferdinand, maboya Nevile na wengineo.
Wanajiita the class of '92 maboya sana hawajui dunia imebadilika na soka lake. Kuna mmoja anasema juzi ingalikuwa kipindi cha Ferguson, Pogba hata sifa ya kukaa bench hana. Cha ajabu sijaona chochote cha maana walichofanya ukilinganisha na ile Barcelona ya akina Messi, Iniesta na Xavi ambao Mou aliwafunga na Inter na wakachukua treble. Pathetic!
 
Ana chuki binafsi na Mou....halafu anamng'ang'ania utadhani ana hati miliki ya Man U cha ajabu ukimpa nafasi ya kuwa kocha atapata tabu sana kama mwenzao Thierry anavyopata Monaco.
 
Yani jamaa hafichi chuki zake kwa special one. Hata walivyomfunga juve jamaa bado anamponda tu utadhani alitamani mani wafungwe.

Mimi si shabiki wa Mani ila nawaombea washinde. Tena wawafunge Mancity wikendi hii ili huyu red head Scholes akate ngebe
Scoles amekua mtu wa kusema hovyo siku zote. Makocha wote wanaopita MU anawasimanga .Mwenzake Gary Nevile alipewa timu Spain timu ikamshinda akatinuliwa. MU ina wachezaji wazuri tatizo wachezaji wenyewe ni laini sana yaani karibia wote watoto wa mama. ilijambo lina msumbua sana Josee. inatakiwa MAN U itafute wachezaji wa kuwaambukiza waliopo upambanaji iyo ndio siri ya Furgason.
 
Eti watoto wa mama.. ..ila nyie hama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…