Wakuu
Yaani salamu za shikamoo zimekuwa nyingi sana, wakati nikijiangalia kwenye kioo bado najiona Handsome.
Ni mnyamwezi fulani hv najipenda muda wote nanukia, kipato si haba. Nina O moja matata. Nywele zangu ni kama za kiarabu kwahiyo kinyozi anakula angle hatari. Ila Dah shikamoo zimekuwa nyingi sana.
Wakuu nishaurini kama sitaki kupokea shikamoo niwe najibu nini ? Mimi huwa nikiambiwa shikamoo najibu mambo binti. Sijui nyie huwa mnafanyaje.