Mbona sioni habari yoyote kuhusu Somaliland?

Mbona sioni habari yoyote kuhusu Somaliland?

Abdi hussein

Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
19
Reaction score
15
Habari za Mda huu,

Nimeona Habari nyingi za kimataifa lakini sijawahi kukutana na taarifa za Somaliland.

Somaliland ni jamhuri kamili ambayo ilikua ndani ya Somalia lakini muda Sasa imejitenga na kuwa na Serikali yake na bendera yake na ninaona kwenye taarifa zingine za habari ni nchi yenye Amani sana na watu wake ni wakarimu sana
 
Tatizo ni kwamba haitambuliwi kimataifa (haitambuliwi na Umoja wa Mataifa) kama nchi huru. Hilo tu. Mengine yako poa. Kwa mfano kuna siku nilifuatilia documentary moja ya BBC.

Mwandishi alikwenda kwenye soko la kubadilisha fedha. Hakuwakuta baadhi ya wafanyabiashara- walikuwa msikitini kuswali, na sehemu zao za biashara hazikuwa na mwangalizi yoyote na zilikuwa wazi na hakuna mtu wa kuiba.
 
Tatizo ni kwamba haitambuliwi kimataifa (haitambuliwi na Umoja wa Mataifa) kama nchi huru. Hilo tu. Mengine yako poa. Kwa mfano kuna siku nilifuatilia documentary moja ya BBC, mwandishi alikwenda kwenye soko la kubadilisha fedha. Hakuwakuta baadhi ya wafanyabiashara- walikuwa msikitini kuswali, na sehemu zao za biashara hazikuwa na mwangalizi yoyote na zilikuwa wazi na hakuna mtu wa kuiba.
Ni kweli lkn Kuna harakati kubwa za kutambuliwa kimataifa zinafanyika, japo Kuna mataifa tayari yanatambua na pia uwizi ni mdogo sana watu Wana wacha Mali zao kwa kwenda Kuswali na kukuta salama.
 
Tatizo ni kwamba haitambuliwi kimataifa (haitambuliwi na Umoja wa Mataifa) kama nchi huru. Hilo tu. Mengine yako poa. Kwa mfano kuna siku nilifuatilia documentary moja ya BBC, mwandishi alikwenda kwenye soko la kubadilisha fedha. Hakuwakuta baadhi ya wafanyabiashara- walikuwa msikitini kuswali, na sehemu zao za biashara hazikuwa na mwangalizi yoyote na zilikuwa wazi na hakuna mtu wa kuiba.

Hakuna mtu wa kuiba au hakuna wizi?
 
Kuna; Puntland, Somaliland na Somalia ya akina Alshabaab.🤣
 
Back
Top Bottom