Mbona Tumesahau Haraka Kiasi Hiki?

Mbona Tumesahau Haraka Kiasi Hiki?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MBONA TUMESAHAU HARAKA KIASI HIKI?

Kitabu hicho hapo chini kiliandikwa kueleza na kuhifadhi yaliyotokea Zanzibar mwaka wa 2001. Nimeweka picha chache labda tutazinduka. Picha nyingine ndani ya kitabu nimejizuia kuziweka hapa.

Hizi ni picha za wale waliouliwa na watoto wadogo mayatima. Inahitaji moyo mgumu kuziangalia usitokwe na machozi. Kitabu hiki alinipa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na aliniandikia maneno haya:

''Dear Mohamed,
Please critically read this book and please make an effort to write your own account by interviewing survivors of the massacre.
I believe you will write even better and more vivid account.''

Signed: Ibrahim Lipumba.

Kipi kinachotafutwa Zanzibar?

Mbona tumesahau haraka kiasi hiki?

IMG-20221113-WA0070.jpg
IMG-20221113-WA0069.jpg
IMG-20221113-WA0068.jpg
IMG-20221113-WA0067.jpg
IMG-20221113-WA0066.jpg
 
Pole kwa walioumia na kupoteza wapendwa wao.

Ila mwisho wa siku Lipumba ameungana na watesi wao, ndio tujue kila mtu anaangalia maslahi yake, haya mambo ya dini /chama ni kisingizio tu.
 
Vishu...
Damu iliyomwagika Zanzibar.
Mtwaŕa ilimwagika damu na maalim jakaya damu ilimwagika na ukatili wa kutisha kama baba kushurutishwa amuingilie mwanae au mtoto amuingilie mama yake kwenye operation tokomeza ,vipi wewe hukuandika ?au kwakuwa wale hawakuwa waislamu ? Au kwakuwa yale yalifanyika kwenye utawala wa muislamu?wewe ni mnafiki sana
 
Mnachihangu,
Unaandika ikiwa umejaa hamaki.

Hapana sikuwa na taarifa za ndani za matukio hayo vinginevyo ningeandika.
 
Mnachihangu,
Unaandika ikiwa umejaa hamaki.

Hapana sikuwa na taarifa za ndani za matukio hayo vinginevyo ningeandika.
Kama unaweza pata taarifa za miaka 70 iliyopita na kuziandika unashindwa vipi kupata taarifa za miaka 10 iliyopita na kuziandika??mzee tunakujua mlengo wako...hata kama chongo utaita kengeza kwa illusion zako za kidini..wewe na wenzako mnatuharibia jamii ya watanzania...Good for nothing...udini mtupu umekujaa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wamefanya nini tena huko siku za karibuni kinachokufanya uone kuwa wamesahau?
James,
Kachaguliwa Mkrugenzi wa ZEC aliyesababisha uchaguzi wa 2020 kuvurugika.

Matokeo yake Wazanzibari waliuliwa.
 
We nchi nzima hii nauli yako imeishia zanzibar tu kutafuta huo umbeya. Mauaji yanayofanywa na majambazi Kigoma na Tabora hayo mbona huyaandiki?

Nchi hii inamatatizo mengi, mojawapo ni huyu mzee anaeleta uongo ili kughilibu umma usononeke kwamba waislam wanaonewa ilhali uovu wa CCM umetapakaa nchi nzima kwa watu wa dini na kabila zote.

Tatizo haliwezi kuwa ccm zanzibar, ni CCM!
 
We nchi nzima hii nauli yako imeishia zanzibar tu kutafuta huo umbeya. Mauaji yanayofanywa na majambazi Kigoma na Tabora hayo mbona huyaandiki?

Nchi hii inamatatizo mengi, mojawapo ni huyu mzee anaeleta uongo ili kughilibu umma usononeke kwamba waislam wanaonewa ilhali uovu wa CCM umetapakaa nchi nzima kwa watu wa dini na kabila zote.

Tatizo haliwezi kuwa ccm zanzibar, ni CCM!
Marashi,
Umetoa hoja za maana ila lugha yako tu.

"Huyu mzee," "uongo,'' na mengine.
Hali kama hii huwa naepusha shari.

Ikiwa unataka mjadala tuwekeane heshima na adabu.
 
Back
Top Bottom