Mbona tunatishana sana kuliko kujadili rasimu ya Katiba Mpya?

Mbona tunatishana sana kuliko kujadili rasimu ya Katiba Mpya?

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,395
Reaction score
1,112
Salaam wana JF, Bila shaka kwa asilimia kubwa Watanzania wana kiu kubwa ya kuishi chini ya mwamvuli wa katiba mpya itakayotokana na mawazo yao, kwa ajili yao na sheria mama itakayoamua hatma yao miaka kadhaa ijayo. Cha kushangaza ni pale vitisho vya kidini na itikadi za vyama vinapotawala mchakato wa katiba mpya.Kuna watu hata humu JF wanaogopa kabisa kujadili vipengele kadhaa vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa hofu ya kutokwenda kinyume na chama. Imekuwa bahati mbaya kwamba chama tawala (CCM) kimekuwa mstari wa mbele kuwatisha wananchi badala ya hoja mahsusi.Kuna kile kinaitwa MSIMAMO WA CHAMA, kura ya maoni imepigwa lini kuupata huo msimamo wa chama? Imekuwaje leo, Nape na CCM mnatukana raia wema wenye maoni tofauti kuwa hawana akili kisa wanaunga mkono mfumo wa muungano uliopendekezwa tume? Kwanini mnatisha watu kuwa mfumo huo ni bomu linalongoja kulipuka badala ya kujenga hoja?
 
Back
Top Bottom