Walimu walioajiriwa mwaka huu walikaa mitaani kwa muda wa miezi nane yaani tangu wahitimu vyuo mwaka jana mwezi wa tano. Sababu ya walimu hao kukaa mitaani kwa muda mrefu baada ya kuhitimu vyuo ni serikali kutokuwa na pesa ingawa katika bajeti ya mwaka jana kulikuwa na pesa zilizotengwa kwa ajili ya ajira mpya. Je, pesa zilienda wapi? Walimu hao waliajiriwa mwaka huu mwezi wa pili lakini wengi tangu waajiriwe bado hawajlipwa pesa zao za kujikimu na wengine waliolipwa walilipwa kiwango ambacho hakikuwa stahili yao. Mfano wale walimu wa diploma walipaswa kulipwa sh elfu thelathini na tano kwa siku kwa muda wa siku saba lakini badala yake katika halmashauri nyingi nchini walimu hao baadhi waliolipwa walilipwa sh elfu thelathini kwa muda wa siku nne. Na katika baadhi ya halmashauri wamelipwa sh elfu tisini kwa muda wa siku tatu. Halmashauri zingine chache ndio wamelipwa kiwango halali cha pesa za kujikimu isipokuwa bado hawajlipwa pesa za nauli na mizigo. Kwa hiyo halmashauri nyingi pesa za kujikimu zimechakachuliwa na wakurugenzi huku wizara nayo ikikaa kimya. Na walimu hao inasemekana hawatalipwa mshahara wa mwezi wa pili ingawa walisaini mkataba kuanzia tarehe moja mwezi februari. Hii inaonesha ni jinsi gani serikali isivyowathamini walimu. Kwa nini? Sababu watoto wa wanasiasa hawasomi katika shule hizi za kata ambazo zimepelekewa walimu wengi. Kwa hiyo wala haiwaumi.Kwa mantiki hiyo siasa imeshaua elimu nchini kwa kujenga matabaka katika jamii.