Mbona walimu hawathaminiwi na serikali?

bbukhu

Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
58
Reaction score
1
Walimu walioajiriwa mwaka huu walikaa mitaani kwa muda wa miezi nane yaani tangu wahitimu vyuo mwaka jana mwezi wa tano. Sababu ya walimu hao kukaa mitaani kwa muda mrefu baada ya kuhitimu vyuo ni serikali kutokuwa na pesa ingawa katika bajeti ya mwaka jana kulikuwa na pesa zilizotengwa kwa ajili ya ajira mpya. Je, pesa zilienda wapi? Walimu hao waliajiriwa mwaka huu mwezi wa pili lakini wengi tangu waajiriwe bado hawajlipwa pesa zao za kujikimu na wengine waliolipwa walilipwa kiwango ambacho hakikuwa stahili yao. Mfano wale walimu wa diploma walipaswa kulipwa sh elfu thelathini na tano kwa siku kwa muda wa siku saba lakini badala yake katika halmashauri nyingi nchini walimu hao baadhi waliolipwa walilipwa sh elfu thelathini kwa muda wa siku nne. Na katika baadhi ya halmashauri wamelipwa sh elfu tisini kwa muda wa siku tatu. Halmashauri zingine chache ndio wamelipwa kiwango halali cha pesa za kujikimu isipokuwa bado hawajlipwa pesa za nauli na mizigo. Kwa hiyo halmashauri nyingi pesa za kujikimu zimechakachuliwa na wakurugenzi huku wizara nayo ikikaa kimya. Na walimu hao inasemekana hawatalipwa mshahara wa mwezi wa pili ingawa walisaini mkataba kuanzia tarehe moja mwezi februari. Hii inaonesha ni jinsi gani serikali isivyowathamini walimu. Kwa nini? Sababu watoto wa wanasiasa hawasomi katika shule hizi za kata ambazo zimepelekewa walimu wengi. Kwa hiyo wala haiwaumi.Kwa mantiki hiyo siasa imeshaua elimu nchini kwa kujenga matabaka katika jamii.
 
hao walimu wao hawajui kiwango wanachopaswa kulipwa? na kama wanajua kwann walipokea? kwa mtndo huu wataendelea kuwaonea koz hawa-react
 
Niligundua walimu baadhi mnaishia kuongea tu bila vitendo...watu wanadai stahili zao bila ya waraka..kuhusu mshahara wa mwezi feb.anzeni kuhesabu malimbikizo kwani serikali ishatenga fedha kwa ajili uchaguzi mdogo Arumeru mashariki..vuta subira hadi mwezi April mambo yatakuwa sawa waalimu!!
 
Bwana,ualimu ni wito.hutaki acha.
 
Bwana,ualimu ni wito.hutaki acha.

Kuacha hatuachi.. Ila matokeo ya necta mtayaona.. Mwl kufaulisha nao ni wito
In some few years to come raisi atakuwa mwanamke tena mwanaasha makamu wake jesca magufuli
 
Bwana,ualimu ni wito.hutaki acha.

Nani kakudanganya kuwa ualimu ni wito? ualimu sasa hivi ni kazi kama kazi zingine. Lazima wathaminiwe la sivyo elimu bora haitapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…