Mbongo akikuambia Lori ya Tandamu basi elewa kama ifuatavyo...

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Anamaanisha lori lenye double trailers (kama unavyoona hapo pichani. Kwa lugha ya kizungu neno hilo TANDAMU ambalo watanzania wengi hasa kwenye sekta ya usafirishaji hupenda kulitumia linatokana na neno TANDEM.

Neno Tandem hasa lilianzia kwenye baiskeli za TANDAMU (hiyo pichani) ambazo huendeshwa na watu wawili(ni nadra kuziona Afrika aina hii ya baiskeli.

Aidha neno hilo hilo tandem au TANDAMU kama wabongo tunavyopenda kulitamka linaweza kumaanisha vitu pacha vyovyote vinavyoenda kwa kufuatana kwa mfano gari la kukandamiza ardhi hilo hapo pichani ambalo ni TANDEM Vibrator roller au Injini za ndege mfuatano kama hizo ambazo kibongo tutaziita INJINI TANDAMU!

Pia, neno hili TANDAMU kwenye lugha ya kiingereza hutumika kukamilisha senntensi inayomaanisha jambo,vitu au watu fulani vinaenda au wanaenda kwa kufuatana/kuambatana kwa mfano the horses ran in tandem au New Force and Sauli buses moved in tandem.... nk nk Wabongo kwa kutohoa nawapa salyuti!!

!
 
Hilo neno ndio nalisikia kwa mara ya kwanza kutoka kwako
 
Hilo neno ndio nalisikia kwa mara ya kwanza kutoka kwako

Sent from my TECNO B1 using JamiiForums mobile app
Utakuwa wa ushuani wewe sio bure mkuu...hili ni neno maarufu sana kwenye sekta ya usafirishaji tanzania hasa kwenye magereji, masoko makubwa ya mazao kv mahindi nk

Kuna terminologies fulani kama hauko vizuri sana kwenye ku-socialise huwezi zifahamu kabisa!!
 
Asante sie huku chattle mtu akisema tandamu tunajua anamanisha fuso
 
Hayo malori yanayovuta tela yamezoeleka kwa jina la pulingi, ukiliita tandamu watacheka mpaka kesho make huku chattle tushaaminishwa tandamu ni fuso
 
Hii tafsiri yako naona hata double difu linaangukia ktk sifa za tandamu
 

Siyo wa ushuani tu pia atakuwa kula kulala au hujichanganyi kabisa na pengine bado wewe ni mtoto unapewe school fees so akiingia mtaani tu utaijua tandamu, mende etc etc
 
Dah...umenikumbusha...kuna siku nilikaa na madereva wa mabasi ya mkoa...sikuambulia kitu kwenye maongezi yao...kwani maneno kama chips kavu..maini rost..slesi tupu ndiyo aina za mabasi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Dah...umenikumbusha...kuna siku nilikaa na madereva wa mabasi ya mkoa...sikuambulia kitu kwenye maongezi yao...kwani maneno kama chips kavu..maini rost..slesi tupu ndiyo aina za mabasi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Jamaa wana misamiati yao utasikia "mnara" "mahakama" basi we utajua mahakama kweli!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…