Mboto: Siwezi kuingia mapenzini na msanii wa bongo movies, wengi wapo kimaslahi

Mboto: Siwezi kuingia mapenzini na msanii wa bongo movies, wengi wapo kimaslahi

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Haji Salum aka Mboto amesema kuwa hawezi kuanzisha uhusiano wa mapenzi na wasanii wa Bongo Movie kwa kuwa anaogopa kuchafuliwa jina na kuumizwa kimapenzi.

Mboto alifunguka kupitia mahojiano maalum na Zourha Malisa, ambapo amedai kuwa wasanii wengi wa kike wa filamu za kitanzania (Bongo Movies) hawana mapenzi ya kweli na kwamba wengi wanaangalia maslahi zaidi.

Hata hivyo, alieleza kuwa hatamani kuwa na uhusiano na baadhi ya wasanii hao, bali inamlazimu kuzuia hisia zake ili kuepuka mambo mbalimbali yatakayoyumbisha maisha yake.

"Unajua mimi pia nina tamani na pengine wao wananitamani ila najizuia na wala sitaki kuruhusu majaribu kwani najua ninachokifanya huku kwenye tasnia yetu tunakijua hivyo ni lazima ujiepushe na mambo mengine." Alisema Mboto.

Ameeleza kuwa kuna waigizaji wengi wa kike ambao ni rafiki zake wa karibu na wanashirikiana vizuri kwenye kazi.
 
AisEee huyu jamaa namkubali sana,kwa comedians ninaowakubali bongo huyu atakuwa after mzee majuto kwangu
 
Best comedian ever kwa bongo haitaji ma makeup wala kujibadili badili he can stand hivyohivyo alivyo and big up kwakuwa na hekima kuhusu maisha yako.
 
nani anaujua ukweli wake?

kumbukeni kuna ambao hawakuonwa mchana...!

mwacheni tu ajitafutie kiki...
 
Back
Top Bottom