Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Baada ya upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wao na kuialika Mahakama kutoa hukumu ndogo na kisha mahakama kuwakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu mnamo Februari 18 2022. Leo 04, Machi 2022 ni siku ya watuhumiwa kuanza kujitetea kutokana na tuhuma wanazotuhumiwa nazo.

Awali Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka 5 kati ya 6 katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Kujua kesi ilipoishia fungua kiunganishi hiki: Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea


=========

UPDATES

Jaji anaingia Mahakamani Muda huu Saa 4 na Dakika 52

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili Wa Serikali Waandamizi Tulimanywa Majige
Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Gaston Garubindi
Iddi Msawanga
Evaresta Kisanga
Maria Mushi
Nashon Nkungu
John Mallya
Jeremiah Mtobesya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata Ni hayo tu mh Jaji.

Jaji: Shauri lilikuwa lina kuja kwa Utetezi, Je Mnazo habari zozote za Wateja wenu?

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Shauri lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Utetezi Kwa Upande wangu tulifanya Maandalizi Mazuri Mimi John Malya, Dickson Matata, Fredrick Kihwelo na

Kibatala: wengine Juzi na Jana tulikuwa Ukonga na Segerea. Tulionana nao wakiwa na Bashasha kabisa, Kwamba Leo tunaendelea na Utetezi Lakini Leo Asubuhi tumepata Taarifa Kutoka Kwa Askari Magereza Kwamba Mbowe amepata Matatizo ya Ki Afya. Kwa hiyo hatuwezi Kuendelea,

Hivyo, Tunaweza Kupanga Kuendelea Jumatatu

Jaji: Jumatatu itakuwa Tarehe ngapi

Wakili Peter Kibatala: Tarehe 07 March 2022

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Utetezi, na tumewasikia Wenzetu Maombi Waliyo Wasilisha Sasa tusingependa Kujibu Hoja hiyo, Kwa sababu na sisi tuna Maombi Mengine Kwa hiyo Kujibu Hoja hiyo haitokuwa na Maana sana

Mheshimiwa Jaji tunaomba Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili

Na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai

Jeremiah Mtobesya: Tumesikia Taarifa ya Notes hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka, na Kwa Bahati Mbaya hatuwezi Kusema lolote zaidi ya Kusema tunaichia Mahakama, sababu Kifungu Kinatoa Maelezo Yote Kwamba Baada ya Kusema hivyo tunaichia Mahakama dhidi ya Amri zake za Mwisho

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Taarifa Hii tunaiwasilisha kwa Njia ya Maandishi, Kwa Maombi hayo ya Kifungu cha 91(1) tunaomba Kuondoa Mashitaka Yote dhidi ya Washitakiwa Wote Sababu zote zipo katika Noel Prosecui ambayo tumeiwasilisha

Wakili wa Serikali Robert Kidando: anapeleka Nyaraka Mbele ya Karani wa Jaji, na Karani anampatia Jaji

Jaji: Je umezungumza kwa niaba ya Defense Wote..?

Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba kila Mmoja aseme

John Malya: Mheshimiwa Jaji notes iliyotolewa inayushuka Mikono wote, pamoja na Kujiandaa kwa ajili ya Kujitetea, Mikono yetu imefungwa na hatuwezi Kusema lolote, Tulitaka sana Warudishe Gharama zetu na Mengine lakini wacha Tusubiri Maamuzi ya Mahakama

Fredrick Kihwelo: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Tumesikia Taarifa iliyotolewa, Tunaichia Mahakama iweze Kutoa Amri

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Na sisi tunaichia Mahakama, Sheria inajielezea wazi.. Mahakama ipo Kimya Kidogo na Jaji Bado anaandika

Kule Nje ni Kelele za Shangwe na Fifijo watu Wanaimba, Imebidi Mahakama Kufunga Vioo Vya Madirisha ili Kuzuia Kelele Kuingia Mahakamani, Wewe furaha yako ni Kiwango gani? Onyesha emoji ya furaha hapa Chini.. Au picha yako ukiwa na furaha kubwa..

Jaji: Baada ya Mahakama Kusikiliza Hoja iliyoletwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya Kuendelea na Kesi, na Upande wa Pili wakaridhia

Mahakama inasema Shauri hili lililo kuwa linawakabili Washitakiwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa nakiondosha Mahakamani na Washitakiwa Wanaachiwa huru bila Masharti, sababu Kuna Vielelezo vililetwa Mahakamani, naandaa Amri ya Kuviachia

Jaji: Na hivyo naelekeza Mkuu wa Magereza Kuwaachiwa Mara Moja, Leo na si Vinginevyo Natoa Amri Jaji anatoka Mahakamani Mahakama inaridima Kwa Shangwe.

=======
Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu, wameaachiwa huru leo, na Mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Baada ya DPP Kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo, leo 4.3.2022. Hivyo, Freeman Aikaeli Mbowe

1646383138857.png
 
Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Leo kuna Ibada ya Njia Ya Msalaba aliyopitia Bwana wetu Yesu Kristo kuelekea kwenye ukombozi wa Wana wa Mungu.

Ni imani yangu Simon wa Kirene atatuongoza!

Updates;

Nawatakia Chadema wote Ibada njema ya Njia ya Msalaba.

Mungu ni MWEMA wakati wote.

Jumaa kareem.

The End.
 
Mkuu Nyendo asante kwa taarifa.

Mungu atasimama na haki ya watu wake....iwe leo au kesho atafanya tu.

Kamwe dhuluma isingeweza kushinda Haki na pia giza halijawahi kuwa na nguvu zozote mbele ya NURU.

Tunaungana na Mh. Mbowe na Makomandoo kumshukuru Mungu kwa wema wake.
 
Naona kila dalili ya DPP kuikacha hii kesi!
Yeah lakini with conditions kitu ambacho Mh.Mbowe hawezi kukifanya kabisa hata mwanasiasa yoyote makini.

Yaani utendewe kosa wewe afu upige goti kuomba msamaha..inakuja kweli hiyo.

Yaani ni kwamba ukiomba msamaha ina maana ulifanya hicho kitendo na busara za DPP anakuachia lakini kuna makubaliano mtaafikiana wewe na mahakama tena ya kisheria ndipo unaachiwa. Wengi wanadhani unatoka tu as simple as that hapana.

Baada ya hapo utarudi mtaani bila nguvu ya kisiasa maana wewe mi muharifu mwenye msamaha wa DPP...muda wowote akijiskia anaifufua kesi.
 
Tuko pamoja,najua kuna moshi mweupe utapeperuka leo mbowe ataachiwa na wenzake
Sipendi Mbowe na wenzie waendelee kuwa mahabusu, lakini pia sipendi kusikia ameachiwa kwa MSAMAHA! Kama ni hivyo, basi kesi iendelee tuzijue mbivu na mbichi!

Na nina imani, kwa ushahidi uliotolewa, bila UJAJI WA MCHONGO, kulikuwa hakuna KESI hapo!
 
Yeah lakini with conditions kitu ambacho Mh.Mbowe hawezi kukifanya kabisa hata mwanasiasa yoyote makini.

Yaani utendewe kosa wewe afu upige goti kuomba msamaha..inakuja kweli hiyo.

Yaani ni kwamba ukiomba msamaha ina maana ulifanya hicho kitendo na busara za DPP anakuachia lakini kuna makubaliano mtaafikiana wewe na mahakama tena ya kisheria ndipo unaachiwa. Wengi wanadhani unatoka tu as simple as that hapana.

Baada ya hapo utarudi mtaani bila nguvu ya kisiasa maana wewe mi muharifu mwenye msamaha wa DPP...muda wowote akijiskia anaifufua kesi.
Mbowe alishakataa kuomba msamaha na nionacho DPP anaenda kuikacha kesi!
 
Nasikia wameanza michezo,magereza hawajawaleta watuhumiwa mahakamani!
 
Shitaka lililoondolewa ni lipi mkuu? Na hayo matano ni yapi?
 
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tunaombi Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako

Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili

Na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai
 
Back
Top Bottom