Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Waiting for the updates
 
Kesi inachelewa kuanza ama kuna nini? Saa 5 na robo sasa. Mliopo mahakamani tuambieni hali iliyopo mahakamani.
 
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) leo Ijumaa amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uujumu Uchumi, Dar es Salaam.
 
Kesi inachelewa kuanza ama kuna nini? Saa 5 na robo sasa.

Mliopo mahakamani tuambieni hali iliyopo mahakamani.
 
 
Ndio shida ya kutumika!Aibu Kwa Jaji Kwa maamuzi aliyofanya!Watu wamebumba ushahidi wakaja kuuleta mahakamani,kila mtu akaona ni ushahidi wa mchongo na hakuna kesi!Jaji akasukumwa kuamua kuwa Wana kesi ya kujibu!Kabla hawajaanza kujitetea DPP anasema hana nia ya kuendelea na kesi maana ushahidi alionao ni crap!

Jaji unajisikiaje huko uliko?Ungeyajua haya,Bado uamuzi wako ungekuwa watuhumiwa Wana kesi ya kujibu?
 
#BREAKING: Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini DPP, amemfutia mashtaka yote ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu kwa sababu hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao hawakufikishwa mahakamani kwa sababu mshtakiwa wa 4, Freeman Mbowe ni mgonjwa kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Magereza.

DPP ameondoa mashtaka hayo mbele ya Jaji Joachim Tiganga ambaye anasikiliza kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021 ambapo washtakiwa hao leo walipaswa kuanza kujitetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…