feyzal
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 7,683
- 15,128
Naam bila shaka wote wazima.
Mimi sio mwanasiasa hivyo sio mtaalamu sana na siasa ,ila naelewa maisha yangu 100% yanaongozwa na siasa. Siasa ndo inapanga bei ya mkate,mafuta,vyakula nk ,siasa ndo inapanga muda wa kuamka, kulala,usalama wako afya nk hivyo kujiepusha na siasa ni kujidanganya.
Mh Mbowe mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo (CHADEMA) wewe ni mtu tajiri una pesa zako na familia yako ina hela haina njaa ya kupata mkate,unaweza kufanya mambo mengi na kuishi popote maana pesa unayo,kwa miaka kadhaa tangu nimeanza kujitambua nimekua nikikuona na kukusikia namna unavyopigania haki za watu bila kuchoka na ulipoteza vitu vingi sana kwa ajili ya siasa ila bado uko imara hadi leo.
Mh Mbowe siasa ni watu kama hakuna watu hakuna siasa na hapa ndo kwenye eneo muhimu sana. Kwa miaka kadhaa sasa umekua ukijitahidi wewe na chama chako na viongozi wengine wa chama chako kuja na matamko ya kukemea na kutetea watanzania maskini wenye njaa,dhiki na shida mbali mbali lakini tumekuangusha sana kwasababu wengi wetu tuna udumavu wa akili na ubinafsi wa hali ya juu.
Pamoja na serikali za awamu zote za CCM kufanya mambo ya ajabu lakini bado wananchi tumekua mapang'ang'a hatuna ushirikiano wa kuondoa udhalimu huu. Siku zote Mbowe au Lissu hauwezi kuondoa CCM na vibaraka vuao bila nguvu ya wananchi na hili eneo inaonekana wazi kabisa wananchi hatuko tayari kupokea maumivu kwa ajili ya taifa la kesho hivyo nakusihi sana achana na watanzania kuanzia leo wewe na chama chako kaaeni kimya kila kitu kitokee achana navyo wananchi wapate maumivu kila siku naamini itasaidia wenyewe kuamka siku moja na kuanza kujipigania.
ACHANA NA WATANZANIA WANAFKI,WABINAFSI ,WAONGO NA MAMBUMBU UTAPOTEZA MAISHA NA HAKUNA ATAKAYEKUPIGANIA ,LEO WAZI IMEJIDHIHIRISHA NAMNA ULIVYOKAMATWA PALE MAGOMENI KIRAHISI TU HUKU WANANCHI WACHACHE WALIOJITOKEZA WAKIWA WAMEKAA PEMBENI.
Kuwatete wananchi hawa ni kujifedhehesha.
Asalaam alykum.