Elections 2010 Mbowe Afanyiwa Fujo Kubwa Hai

Kamende, kwanza nakushukuru kwa taarifa hii, pili poleni kwa maswahibu hayo, huo ni mwanzo tuu au rasharasha, fainali ni October 31. Nimesema hiyo ni rasharasha tuu kwa sababu sikio la kufa, halisikii dawa, na mfa maji haachi kutapatapa, hii ni dalili ya maji ya shingo, hongereni.

Pia nina ushauri tuu kuwa inapotokea serious issue kama hii, wewe kama muhabarishaji, tuhabarishe facts tuu bila kuonyeshea wewe uko upande gani. Kwenye taarifa hii, wewe umejitanabaisha na Chadema. Hata kama ni kweli wewe ni Chadema, bado ungeweza kutuhabarisha kwa kutumia fairness, balance, objectivity na impartiality hivyo kuipa taarifa hii more credibility, otherwise itageuka sehemu ya campaign machinery.

Kamende, kama ulivyonisaidia Busanda na Biharamulo, nitahitaji msaada wako siku ya Jumatano, nakuja kunyooshea miguu kidogo hapo Moshi na Arusha.
 
Hii sumu inayomwagwa sisi m inaanza kututafuna kwa kasi zaidi. Hivi baada ya 31/10 wataongea nini wakati wanaishi eneo moja au wanasahu kuwa visasi na chuki vikikomaa ni balaa
 
sasa Jk aeleze anayemwaga damu ni nani. Huu ni ufedhuli wa hali ya juu. Eti anajifanya vyama vinataka kumwaga damu huku anatuma green guards.
 
Acid, sometimes tit for tat does work!. Kuna wakati wa kutumia ustaarabu kuepusha shari lakini pia kuna wakati wa kutumia shari kuzima shari, yaani you beat them on their own game.
 
CHADEMA waombe kibali cha kutrain green guard wao na wenyewe. Wauambie umma namna ambavyo wanaumizwa na waeleze nia yao ya kujilinda kwa njia ya kutrain walinzi wao. Kwa kuwa CCM imetrain 5000 CHADEMA wanaweza kutrain hata 10000, wiki mbili hizi zinatosha kabisa kutoa mafunzo kamili kujiandaa na vita ya tar 1/11 yatakapotangazwa matokeo. Vinginevyo CCM watatumaliza na hatutakuwa na namna ya kujitetea.
 
Hivi wewe magazeti yote yanayoripoti kila siku taarifa za wafuasi wa CCM kuwashambulia wafuasi wa CHADEMA hujayaona? Watu wengine bwana, wana macho lakini hawaoni, wana masikini lakini hawasikii, wana pua lakini hazinusi. Unataka hadi upigwe kibao ndiyo utaelewa kwamba CCM imeanzisha vita? Hebu jaribu kuwa mzalendo kwa nchi yako kuliko kushikilia ushabiki usio na kichwa wala miguu.
 

wanaccm kwa spin bana, eti amesikitishwa na mbowe. Mbowe angekosea sana kumuacha mmoja wa wafanyakazi wa kampeni yake kwenye mikono ya green guards. These are trained killers.
 

hi ndo tz bwana ya ccm
 
wanataka power kwa gharama yoyote ile
watanzania wajiandae sana tarehe 31, ccm wamepanga kufanya chinja chinja kama ya somalia
 
Umeweka post makini sana.
Ni kweli Green Guards wamefanya uhalifu lakini MBOWE naye kama alifight back basi imetia doa sana demokrasia nchini.
Sasa hapo nani atamlaumu mwenzake? Ina maana kama siasa za CCM ni kuteka nyara wapinzani wao basi tuwaachie vyombo vya dola wawanyooshe na siyo jukumu letu kuchukua sheria mkononi.
Mungu ibariki Tanzania
Kura zetu kwa CHADEMA
Slaa for president
 
Acid, sometimes tit for tat does work!. Kuna wakati wa kutumia ustaarabu kuepusha shari lakini pia kuna wakati wa kutumia shari kuzima shari, yaani you beat them on their own game.

Asante umenikumbusha ule wimbo wa Kenny Rogers, 'sometimes you have to fight to be a man' - unaitwa nini, Coward of ?
 
Acid, sometimes tit for tat does work!. Kuna wakati wa kutumia ustaarabu kuepusha shari lakini pia kuna wakati wa kutumia shari kuzima shari, yaani you beat them on their own game.
I agree, lakini angalia Mbowe, mwenyekiti wa chadema, na kibaka anayejiita grin gad!!! Rationale....??? Hakuna

Angetuma vijana mia abaki na amelfu wanamsikiliza
 
Asante umenikumbusha ule wimbo wa Kenny Rogers, 'sometimes you have to fight to be a man' - unaitwa nini, Coward of ?
pole sana... dont compare apples and oranges

namlinganisha mbowe, lipumba na kikwete... national leaders... not street bangers!!
 
Kamende, kitendo tuu cha Kikosi cha ulinzi cha CHADEMA kilimdhibiti huyo kijana na kumhifadhi katika gari moja kwa lengo la kupisha mkutano uendelee hii abduction na illegal deteintion, hicho kikosi cha ulinzi cha Chadema kilipata wapi uwezo huo?.

Kumdhibiti mfanya fujo its a right move hatua iliyotakiwa kufuata ni kumkabidhi kwenye vyombo husika na sio kumhifadhi katika gari, suppose anything fatal ingemtokea huyo kijana, Chadema ingeweka wapi sura yake?.

Kumbukeni mnagombea kisu chenye makali kuwili huku wenzenu wameshika kwenye mpini!.
 
wanaccm kwa spin bana, eti amesikitishwa na mbowe. Mbowe angekosea sana kumuacha mmoja wa wafanyakazi wa kampeni yake kwenye mikono ya green guards. These are trained killers.
usiwe haambiliki... na naomba uchukue sekunde kusoma post zangu, au muandikie MS atakuambia... he went even offiline kupambana na mimi

Lakini hatuwezi kuwa na blind love na kushangilia hata mtu akijisaidia sebuleni eti mtemi... hayo mambo ni ya kitoto

Mbowe made a huge mistake, he is carrying Dr Slaa kama partner kwenye siasa... unadhani image gani inakuja??

tuwe wakweli, anapokosea mtu aambiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…