Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Katika ufuatiliaji mdogo wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, nimeona mapungufu makubwa ambayo niliwahi kuelezea humu ndani. Wengine walisema sijui kitu na kwamba ile ilikuwa tu kesi ndogo na kuwa wanaenda kuiangusha serikali. Nikasema tusubiri tuone.
Leo nitagusia njia mojawapo inayoweza kuipa Serikali mwanya wa kumuachia huru Mbowe na kulinda sura zao. Tukumbuke siku zote Serikali haipendi kuumbuka.
Kabla sijaelezea hilo ngoja niwakumbushe kidogo kesi moja iliyokuwa inamkabili producer wa muziki wa Marekani Sean Combs, maarufu kama Puff Daddy pamoja na msanii wake aliyekuwa anajulikana kama Shyne. Ilikuwa ni kesi ya kurusha risasi ndani ya club ya usiku.
Baada ya kugundua kuwa ni lazima kuna mtu inabidi afungwe katika kesi ile (nadhani kuna mtu alikufa na majeruhi kadhaa) alichofanya Wakili wa Sean Combs, ilikuwa ni kuwatenganisha Sean Combs na Shyne. Kila mmoja akawa anawakilishwa na Wakili wake. Ilikuwa kama ni kumtoa kafara Shyne.
Nashangaa sana mpaka sasa kwa Mawakili wa CHADEMA kutochukua tahadhari za kutosha kumlinda Mbowe. Hili nililielezea vizuri huko nyuma. Katika hatua hii, njia mojawapo wanayoweza kuchukua ni hii ya kuwa na mawakili tofauti kwa Mbowe na wale walinzi wake. Ikiwezekana Mawakili wa walinzi wapunguzwe sana.
Mbowe ni mtu mkubwa sana kupewa uwakilishi sawa na wale walinzi wake hata kama mashitaka dhidi yao yanafanana.
Pia hii itaipa mwanya Serikali kujua pa kuangukia kama wakiona kabisa kuwa lazima afungwe mtu (hata kama ili tu waepuke aibu). Kafara ya wale walinzi siyo kubwa sana kwa uhuru wa Mwenyekiti Mbowe.
Nawasilisha hoja.