Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa na mgombea wa nafasi hiyo kwa mara nyingine Freeman Mbowe akizungumza siku ya Ijumaa Januari 17, 2025 katika kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na chaneli ya runinga ya UTV
Soma: Ezekiel Wenje: Lema ndiye aliongoza kumshughulikia Zitto Kabwe mpaka kuondoka CHADEMA
"Mimi watu kutaka kunipindua nimelisikia na ninalisikia, kwasababu sikuwa sehemu ya hao wanamapinduzi sijui ajenda yao walitaka kuibeba vipi! kwahiyo nisingetamani kuingia kwenye mjadala huo, wao ukiwauliza wanaweza kuwa na majibu zaidi. Lakini dunia hii haina siri, vitu vya hila ni suala la muda tu na haki haijawahi kushindwa na uongo haujawahi kutamalaki."
"Mnaweza kusema mambo ya uongo, ya kusingizia watu, kuwashusha watu, kuwatweza watu lakini kwa kiongozi yeyote ambaye unafahamu kazi ya siasa ni mchezo wa timu lazima utambue kuwa tunahitajiana katika siasa, na huwezi kuwa kiongozi ambaye eti unataka kukiongoza chama kwa kuwashusha wenzio, kwa kuwakanyaga wenzako, kwa kuwatweza wenzako."
"Sisi ni binadamu, tuna mapungufu, yawezekana Mwenyekiti Mbowe ana mapungufu yake, Katibu Mkuu wangu ana mapungufu yake halikadhalika Wajumbe wa Kamati Kuu, kila binadamu ana mapungufu yake. Katika taasisi ambayo mnajengana kwenye mazingira ambayo mnaonewa sana, umoja wetu na nguvu yetu ya pamoja ndiyo silaha yetu kubwa."