nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
na Mwandishi wetu
KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amembana Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kutaka alieleze Bunge kwamba zoezi la ubomoaji wa nyumba za wananchi, linazingatia sheria au linatokana na utashi wa viongozi wa nchi.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aliomba ufafanuzi huo wakati akiuliza swali la nyongeza.
Alisema kumekuwa na kauli zinazotofautiana za viongozi kuhusu ubomoaji wa nyumba zilizoko eneo la barabara kiasi kwamba wananchi wengi hawajui zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa sheria au linafuata matamko ya viongozi.
Tuhahitaji kufahamu kuhusu zoezi la bomoabomoa, maana hatuelewi linafanyika kwa mujibu wa sheria au matamko ya viongozi kwani hali hiyo inawafanya wananchi wa kawaida washindwe kutambua haki zao kwa mujibu wa sheria, sasa ni wakati muafaka kwa serikali kutoa ufafanuzi, alisema Mbowe.
Akijibu swali hilo, Waziri Magufuli alisema zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizo maeneo ya barabara, linatekelezwa kwa mujibu wa sheria namba 4 mwaka 1999, 5 mwaka 1999 na mabadiliko ya sheria ya barabara ya mwaka 2008, 2007 na 2013, ambazo zinaelekeza utekelezaji wa sheria hiyo.
Alisema kama waziri mwenye dhamana, atatekeleza na kusimamia sheria hiyo kwani hata alipoapa alisema atailinda sheria na aliomba Mungu amsaidie.
Alisema sheria hiyo ndiyo inayosimamia na kutekelezwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kinachoongoza serikali.
Hata hivyo Waziri Magufuli, hakuwa tayari kuzungumzia mgongano wa kauli za viongozi wa juu ambazo zinatofautiana na kauli yake (Magufuli).
Hivi karibuni, Waziri Magufuli aliagiza ubomoaji wa nyumba zote zilizojengwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara, lakini Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Jakaya Kikwete kwa nyakati tofauti, waliingilia kati kusitisha zoezi hilo kwa madai kuwa litaathiri wananchi ambao wengi wamejenga nyumba zao kwa shida.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa, alisema wakazi 1050 wa Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam, hasa wa mitaa ya Kizani na Mwera, watalipwa fidia ya mali, usumbufu, malazi, upotevu wa faida na usafiri kwa nyumba 249.
Aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Philipa Mturano, aliyetaka kujua kiasi cha fedha watakazolipwa wakazi wa mitaa ya Kizani na Mwera. Waziri Majaliwa, alisema zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi hao, linatarajia kuanza rasmi Aprili 18. Alisema serikali imetenga sh bilioni 7.5 kwa ajili ya malipo hayo.