Mbowe anaona kila ampingae anamtukana

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Alianza Lisu kuchukua fomu na kutoa hoja zake ni nini atakifanyia chama endapo atachaguliwa , Mbowe katoka hadharani na kudai kuwa Lissu anamtukana.

Amekuja John Heche , pamoja na kueleza mbele ya press kuwa Mbowe ni baba yake kisiasa , amemlea na anamheshimu , bado Mbowe anadai Heche anamtukana.

Amekuja Lema , kumuunga mkono Lisu tu, Mbowe anadai Lema anamtukana.

Sasa Ndugu Freeman Mbowe, ni matusi gani unatukanwa unayoyasikia wewe tu na wengine hatuyasikii wala kuyaona ?

Mwisho, Ndg Mbowe, punguza kulialia kwenye press unazozifanya, jenga hoja kwa nini upewe miaka mingine mitano ? Na kwa nini miaka 21 unaona haijakutosha?
 
Mzee Mbowe mnamuonea bure ,kwa kiwango chake cha Elimu ni lazima awe defensive kwa kila anachoambiwa hata kama ni ukweli mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…